settings icon
share icon

Kitabu cha Wakolosai

Mwandishi: Mtume Paulo alikuwa mwandishi wa kimsingi wa kitabu cha Wakolosai (Wakolosai 1:13). Timotheo pia anadaiwa kukiandika (Wakolosai 1: 1).

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Wakolosai huenda kiliandikwa kati ya 58-62 BK.

Kusudi la Kuandika: kitabu cha Wakolosai ni nusu mfumo wa maadili, kinachoshughulikia kila hali ya maisha ya Kikristo. Paulo anakua kutoka kwa maisha ya kibinafsi hadi kwa ukoo na familia, kutokana na kazi hadi kwa jinsi tunapaswa kuwatendea wengine. Dhamira ya kitabu hiki ni ukamilifu wa Bwana wetu, Yesu Kristo, katika kutimiza mahitaji yetu katika kila hali.

Mistari muhimu: Wakolosai 1: 15-16, "Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake ".

Wakolosai 2: 8, "Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo."

Wakolosai 3: 12-13, "Kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi vivyo na ninyi. "

Wakolosai 4: 5-6, "Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu."

Muhtasari kwa kifupi: Wakolosai kiliandikwa waziwazi kwa uasi ulioshindwa ambao ulikuwa umechipuka katika Kolosai, ambao ulihatarisha kuwepo kwa kanisa. Wakati sisi hatujui kile ambacho Paulo aliambiwa, barua hii ni majibu yake.

Tunaweza dhani kulingana na majibu wa Paulo kwamba alikuwa anashughulikia mtazamo wa kusalitiwa kwa Kristo. (Uhalisi na ukweli wa ubinadamu wake na kutokubali uungu wake kamili.) Paulo anaonekana pia kupinga msisitizo wa "Wayahudi" kwa tohara na mila (Wakolosai 2: 8-11; 3:11). Usaliti ulioshughulikiwa unaonekana kuwa kama uasi wa Wayahudi au mchanganyiko kati ya kujinyima raha kwa Wayahudi na falsafa ya Kigiriki (Stoiki?). Yeye anafanya kazi kubwa katika kutuangazia ukamilifu wa Kristo.

kitabu cha Wakolosai kina maelekezo ya kimafundisho kuhusu uungu wa Kristo na falsafa za uongo (1: 15-2: 23), kama vile mashauri tekelezi kuhusu mwenendo wa Kikristo, ikiwa ni pamoja na marafiki na usemi (3: 1-4: 18).

Mashirikisho: Kama ilivyo kwa makanisa yote ya awali, suala la kufuata sheria la Wayahudi katika Kolosai lilikuwa la kujalisha sana kwa Paulo. Hivyo kiini kilikuwa ni dhana ya wokovu kwa neema kando na matendo ambayo kwamba wale waliobobea katika sheria ya Agano la Kale walipata ni vigumu sana kufahamu. Kwa hivyo, kulikuwa na msukumo ulioendelea miongoni mwa washika sheria kuongeza mahitaji fulani kutokana na sheria kwa imani hii mpya. Kimsingi miongoni mwao ni matakwa ya tohara ambayo ilikuwa bado inatekelezwa miongoni mwa baadhi ya waumini Wayahudi. Paulo alikabili dosari hii katika Wakolosai 2: 11-15 ambapo alitangaza kwamba tohara ya mwili haikuwa muhimu tena kwa sababu Kristo alikuwa amekuja. Yake ilikuwa tohara ya moyo, si mwili, na kufanya sherehe rasmi za kanuni za Agano la Kale kutokuwa muhimu tena (Kumbukumbu 10:16, 30: 6; Yeremia 4: 4, 9:26, Matendo 7:51; Warumi 2 : 29).

Vitendo Tekelezi: Ingawa Paulo anazungumzia maeneo mengi, tekelezo la kimsingi kwetu siku hizi ni utoshelevu kabisa na kamili wa Kristo katika maisha yetu, kwa wokovu wetu na utakaso wetu. Lazima tujua na kuelewa injili ili tusipotoshwe na aina za kutatiza za sheria na uasi. Lazima tuwe macho kwa kupotoka kwa aina yoyote ambao kutaweza kupunguza umuhimu wa Kristo kama Bwana na Mwokozi. "Dini" yoyote ambayo inajaribu kujilinganisha yenyewe na ukweli kwa kutumia vitabu ambavyo vinadaiwa kusimama kwa mamlaka sawa na ya Biblia, au ambayo inachanganya juhudi za kibinadamu na utakatifu kamilifu wa wokovu lazima iepukwe. Dini zingine haziwezi kujumuhishwa pamoja na au kuongezwa kwa Ukristo. Kristo anatupa viwango kamili vya mwenendo adilifu. Ukristo ni familia, njia ya maisha, na uhusiano-si dini. Matendo mema, unajimu, mizungu na buruji havituonyeshi njia za Mungu. Kristo pekee ndiye anatuonyesha. Mapenzi yake yametimizwa katika neno lake, upendo wake barua kwetu, tunapaswa kupata kuijua!

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Wakolosai
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries