settings icon
share icon

Kitabu cha Wafilipi

Mwandishi: Wafilipi 1: 1 inatambua mwandishi wa kitabu cha Wafilipi kama mtume Paulo, pengine pamoja na msaada wa Timotheo.

Tarehe ya kuandikwa: kitabu cha Wafilipi huenda kiliandikwa mnamo 61 BK.

Kusudi la Kuandika: Waraka kwa Wafilipi, moja ya nyaraka za Paulo gerezani, iliandikwa katika Roma. Ni katika Filipi, ambapo mtume alitembelea katika safari yake ya pili ya umishonari (Matendo 16:12), kwamba Lidia na mlinzi wa gereza la Filipi na familia yake waliweza kubadilika kwa Kristo. Sasa, miaka michache baadaye, kanisa lilikuwa limeimarika, kama inavyoweza kuhitimishwa kutokana na anwani yake ambayo ni pamoja na "maaskofu (wazee) na mashemasi" (Wafilipi 1: 1).

Hafla ya waraka ilikuwa kukiri zawadi ya fedha kutoka kwa kanisa la Filipi, iliyoletwa kwa mtume na Epafrodito, mmoja wa washirika wake (Wafilipi 4: 10-18). Hii ni barua ya suala nyeti kwa kundi cha Wakristo waliokuwa hasa karibu na moyo wa Paulo (2 Wakorintho 8: 1-6), na kulinganisha machache yalisemwa kuhusu makosa ya mafundisho.

Mistari muhimu: Wafilipi 1:21: "Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida."

Wafilipi 3: 7: "Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo."

Wafilipi 4: 4: "Furahini katika Bwana siku zote; tena nasema , Furahini "!

Wafilipi 4: 6-7: "Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusalina kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijilikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. "

Wafilipi 4:13: "Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu."

Muhtasari kwa kifupi: Wafilipi kinaweza kuitwa "Nyenzo kupitia Mateso." Kitabu kinahusu Kristo katika maisha yetu, Kristo katika akili zetu, Kristo kama lengo letu, Kristo kama nguvu zetu, na furaha kupitia kwa mateso. Kiliandikwa kipindi ambacho Paulo alikuwa amefungwa katika Roma, karibu miaka thelathini baada ya Kristo kupaa na karibu miaka kumi baada ya Paulo kuhubiri huko Filipi kwa mara ya kwanza.

Paulo alikuwa mfungwa wa Nero, lakini bado Waraka kwa haki unatoa sauti kwa kishindo, maneno "furaha" na "furahini" yanaonekana mara kwa mara (Wafilipi 1: 4, 18, 25, 26; 2: 2, 28; Wafilipi 3: 1, 4: 1 , 4, 10). Uzoefu mzuri wa Kikristo ni kushinda, hata hali zetu na ziweje, za maisha, asili, na akili ya Kristo iishiyo ndani yetu (Wafilipi 1: 6, 11; 2: 5, 13). Wafilipi kinafikia mnara wake katika 2: 5-11 na utukufu na tangazo kubwa kuhusu fedheha na furaha ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Wafilipi kinaweza kugawanywa kama ifuatavyo:
Utangulizi, 1: 1-7
I. Kristo Maisha ya mkristo: Kufurahia Licha ya Kuteseka, 1: 8-30
II. Kristo mtindo wa mkristo: kufurahia katika huduma za chini, 2: 1-30
III. Kristo lengo la imani ya mkristo, mahitaji, na matarajio, 3: 1-21
IV. Kristo nguvu za mkristo: Kufurahia kwa hamu, 4: 1-9
Hitimisho, 4: 10-23

Mashirikisho: Kama ilivyo kwa barua zake nyingi, Paulo alionya waumini wapya katika kanisa la Filipi kujihadhari na mwelekeo kwa kushika sheria ambayo iliendelea kukua katika makanisa ya awali. Hivyo ndivyo Wayahudi walivyofungwa kwa sheria za Agano la Kale hadi kwamba kulikuwa na juhudi imara kwa upande wa Wayahudi kurudi katika mafundisho ya wokovu kwa matendo. Lakini Paulo alirudia kwamba wokovu ni kwa imani pekee katika Kristo peke yake na kuwapa Wayahudi jina baya kama "mbwa" na "watu watendao maovu." Hasa, washika sheria walikuwa wakisisitiza kwamba waumini wapya katika Kristo wanapaswa kuendelea kutahiriwa kulingana na mahitaji ya Agano la Kale (Mwanzo 17: 10-12; Walawi 12: 3). Kwa njia hii, walijaribu kumpendeza Mungu kwa juhudi zao wenyewe na kujiinua wenyewe juu Wakristo wa Mataifa ambao hawakuwa wanashiriki katika kaida za dini/taratibu ya ibada. Paulo alieleza kwamba wale ambao walikuwa wamesafishwa kwa damu ya mwana-kondoo hawakupaswa tena kufanya kaida za dini ambazo ziliashiria haja ya moyo safi.

Vitendo Tekelezi: Wafilipi ni moja ya barua za Paulo za kibinafsi zaidi, na kama hivyo ina matekelezi kadhaa binafsi kwa Waumini. Kwa kuandikwa kipindi cha kufungwa kwake katika Roma, Paulo anahimiza Wafilipi kufuata mfano wake na " kutiwa moyo kulisema neno la Mungu kwa ujasiri zaidi na bila woga" (Wafilipi 1:14) katika wakati wa mateso. Wakristo wote wamepitia, kwa wakati mmoja au mwingine, uadui wa makafiri dhidi ya injili ya Kristo. Hili lazima litarajiwe. Yesu alisema kwamba dunia ilimchukia na itawachukia wafuasi wake pia (Yohana 5:18). Paulo anatuhimiza kuvumilia katika mateso, na "kusimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili" (Wafilipi 1:27).

Utendaji mwingine wa Wafilipi ni hitaji kwa Wakristo kuwa na umoja katika unyenyekevu. Tumepatanishwa na Kristo na tunahitaji kujitahidi kuwa na umoja kati yetu vile vile. Paulo anatukumbusha kuwa "na nia moja, wenye mapenzi mamoja,wenye roho moja mkinia mamoja" na msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno, "bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake" kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine (Wafilipi 2: 2-4). Kungekuwa na migogoro chache sana katika makanisa siku hizi ikiwa zote tungechukua ushauri wa Paulo moyoni.

Utendaji mwingine wa Wafilipi ni ule wa furaha na kufurahia ambao unapatikana katika barua nzima. Anafurahia kwamba Kristo anatangazwa (Wafilipi 1: 8); anafurahia kwa mateso yake (2:18); anahimiza wengine kufurahia katika Bwana (3: 1); na anarejelea ndugu Wafilipi kama "furaha na taji yake" (4: 1). Anahitimisha kwa himizo hili kwa Waumini: "Furahini katika Bwana siku zote; tena, nasema furahini "(4: 4-7). Kama waumini, tunaweza kufurahia na kuwa na amani ya Mungu kwa kuweka mahitaji yetu yote kwake, ikiwa "katika kila neon kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zetu na zijulikane na Mungu" (4: 6). Furaha ya Paulo, licha ya mateso na kufungwa, inakuja iking’aa kupitia kwa waraka huu, na tumeahidiwa furaha sawa na aliyokuwa nayo wakati tunalenga mawazo yetu kwa Bwana (Wafilipi 4: 8).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Wafilipi
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries