settings icon
share icon

Kitabu cha Waebrania

Mwandishi: Ingawa wengine wanajumlisha kitabu cha Waebrania miongoni mwa maandishi ya mtume Paulo, utambulisho halisi wa mwandishi bado umebakia kuwa fumbo. Salamu za Paulo za kawaida haziko ambazo ni kawaida kwa kazi zake zingine. Aidha, pendekezo kwamba mwandishi wa waraka huu alitegemea maarifa na habari zilizotolewa na wengine ambao walikuwa mashahidi halisi waliojionea wenyewe wa Kristo Yesu (2: 3) kuufanya uandishi wa kipaulo kuyiwa wasiwasi. Baadhi hudai Luka kama mwandishi wake; wengine wanapendekeza kwamba Waebrania huenda kiliandikwa na Apolo, Barnaba, Sila, Filipo, au Akila na Prisila. Bila kujali mkono wa binadamu ambao ulishika kalamu, Roho Mtakatifu wa Mungu ndio mwandishi mkuu wa Maandiko yote (2 Timotheo 3:16); Kwa hivyo, Waebrania kinaongea kwa mamlaka ya sheria za kanisa kama vitabu vingine sitini na tano vya Biblia.

Tarehe ya kuandikwa: Baba wa kanisa la kale Kilementi alinukuu kutoka kwa kitabu cha Waebrania mnamo 95 BK. Hata hivyo, ushahidi wa ndani kama vile ukweli kwamba Timotheo alikuwa hai wakati waraka uliandikwa na kukosekana kwa ushahidi wowote unaonyesha mwisho wa mfumo wa kutoa dhabihu wa Agano la kale ambao ulitokea na uharibifu wa Yerusalemu mnamo 70 BK, inaonyesha kitabu kiliandikwa karibu 65 BK.

Kusudi la Kuandika: Marehemu Daktari Walter Martin, mwanzilishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kikristo na mwandishi wa kitabu kilichouzika bora zaidi Ufalme wa Madhehebu, alikejeli katika tabia yake ya kawaida ya kufanya utani kwamba kitabu cha Waebrania kiliandikwa na mmoja wa Waebrania kwa Waebrania wengine akiwaambia Waebrania kuacha kujifanya kama Waebrania. Kwa kweli, wengi wa waumini wa kiyahudi wa awali walikuwa wakiteleza na kurudi katika kanuni na kaida za dini za kiyahudi ili kuepuka mateso yaliyokuwepo. Barua hii, basi, ni mawaidha kwa wale waumini walioteswa kuendelea katika neema ya Yesu Kristo.

Mistari muhimu: Waebrania 1: 1-2: "Mungu ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi anasema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. "

Waebrania 2: 3: "Sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii?"

Waebrania 4: 14-16: "Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. "

Waebrania 11: 1: "Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana"

Waebrania 12: 1-2: "Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. "

Muhtasari kwa kifupi: kitabu cha Waebrania kinanenea makundi matatu tofauti: waumini katika Kristo, wasioamini ambao walikuwa na maarifa ya na kukubali kiakili kwa ukweli wa Kristo, na kwa makafiri ambao walivutiwa kwa Kristo, lakini waliomkataa hatimaye. Ni muhimu kuelewa ambayo kundi ni kuwa kushughulikiwa katika ambayo kifungu. Kwa kushindwa kufanya hivyo kunaweza kutufanya kuchora hitimisho zizizowiana na maandiko mengine.

Mwandishi wa Waebrania anaendelea kutaja ukuu wa Kristo katika utu wake na katika kazi za huduma yake. Katika maandiko ya Agano la Kale, tunaelewa kanuni na sherehe za kiyahudi mfano ulioashiria kwa kuja kwa Masihi. Ina maana kwamba, kanuni za kiyahudi zilikuwa tu ishara za vitu vijavyo. Waebrania inatuambia kwamba Kristo Yesu ni bora kuliko kitu chochote dini tu inaweza kutoa. Fahari na hali zote za dini zina mipaka kwa kulinganisha na utu, kazi, na huduma ya Kristo Yesu. Ni ukuu wa Bwana wetu Yesu, basi, kwamba unabakia dhamira ya barua hii iliyoandikwa kwa lugha ya kushawishi.

Mashirikisho: Labda hakuna mahali popote katika Agano Jipya ambapo Agano la Kale linaangaziwa zaidi kuliko katika kitabu cha Waebrania, ambacho kina kama msingi wake ukuhani wa kilawi. Mwandishi kwa Waebrania daima analinganisha upungufu wa mfumo wa kutoa dhabihu wa Agano la Kale kwa ukamilifu na kukamilika katika Kristo. Wakati Agano la Kale lilihitaji utoaji wa sadaka mara kwa mara na upatanisho wa dhambi wa kila mwaka uliotolewa na kuhani binadamu, Agano jipya linatoa sadaka moja na ya mwisho kupitia kwa Kristo (Waebrania 10:10) na kufikia kiti cha enzi cha Mungu kwa wote walio ndani ya Kristo.

Vitendo Tekelezi: Kwa wingi wa msingi wa mafundisho ya kikristo, waraka kwa Waebrania pia unatupa mifano ya kututia moyo ya "mashujaa wa imani" wa Mungu ambao walistahimili licha ya matatizo makubwa na hali mbaya (Waebrania 11). Washirika hawa wa nyumba ya imani ya Mungu wanatoa ushahidi wa kutosha kwa uhakika usio na masharti na uwezo wa Mungu wa kutegemewa kabisa. Kadhalika, tunaweza kudumisha imani kamili katika ahadi za Mungu, bila kujali hali zetu, kwa kutafakari uaminifu wa mwamba imara wa utendaji kazi wa Mungu katika maisha ya watu wake katika Agano la Kale.

Mwandishi wa Waebrania anatoa faraja kubwa kwa waumini, lakini kuna onyo tano zito/makini ambazo ni lazima tuzitilie maanani. Kuna hatari ya kupuuza (Waebrania 2: 1-4), hatari ya kutoamini (Waebrania 3: 7-4: 13), hatari ya kutokomaa kiroho (Waebrania 5: 11-6: 20), hatari ya kushindwa kuvumilia (Waebrania 10: 26-39), na asili ya hatari ya kukataa Mungu (Waebrania 12: 25-29). Na hivyo tunapata katika taji la kifungu hiki utajiri mkubwa wa mafundisho, faraja chipukizi ya kuburudisha, na chanzo cha onyo tendaji muhimu dhidi ya uvivu katika mienendo yetu ya Kikristo. Lakini bado kuna zaidi, kwa kuwa katika Waebrania tunapata taswira tukufu iliyotolewa ya Bwana wetu Yesu Kristo-mwanzilishi na mkamilishaji wa wokovu wetu mkuu (Waebrania 12: 2).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Waebrania
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries