settings icon
share icon

Kitabu cha Tito

Mwandishi: Tito 1: 1 inatambua mtume Paulo kama mwandishi wa kitabu cha Tito.

Tarehe ya kuandikwa: Barua kwa Tito ilikuwa imeandikwa mnamo 66 BK.Safari nyingi za Paulo zimenakiliwa vizuri na zinaonyesha kwamba yeye aliandika kwa Tito kutoka Nikopoli katika Epirusi. Katika baadhi ya Biblia mchango kwa barua unaweza kuonyesha kwamba Paulo aliandika kutoka Nikopoli katika Makedonia. Hata hivyo, hakuna mahali panapojulikana hivyo na michango haina mamlaka kwa kuwa si halisi.

Kusudi la Kuandika: Barua kwa Tito inajulikana kama moja ya Nyaraka za Kichungaji kama zilivyo barua mbili kwa Timotheo. Waraka huu uliandikwa na mtume Paulo kumtia moyo ndugu yake katika imani, Tito, ambaye alikuwa amemwacha Krete kuongoza kanisa ambalo Paulo alikuwa ameanzisha katika mojawapo ya safari zake za kimishenari (Tito 1: 5). Hii barua inamshauri Tito kuhusu ni sifa gani anafaa kuangalia katika viongozi kwa kanisa. Yeye pia anamwonya Tito kuhusu sifa za wale wanaoishi katika kisiwa cha Krete (Tito 1:12).

Kuongezea kwa maelekezo kwa Tito kuhusu anayopaswa kuangalia katika kiongozi wa kanisa, Paulo pia alimtia moyo Tito kurudi Nikopoli kwa ajili ya kumtembelea. Ina maana kuwa, Paulo aliendelea kumchunga Tito kama mtume na wengine walivyoendelea kukua katika neema ya Bwana (Tito 3:13).

Mistari muhimu: Tito 1: 5, "Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru."

Tito 1:16, "Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai. "

Tito 2:15, "Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote. "

Tito 3: 3-6, "Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu. "

Muhtasari kwa kifupi: Ni ajabu kiasi gani ilikuwa wakati Tito alipokea barua kutoka kwa mshauri wake, mtume Paulo. Paulo alikuwa mtu aliyeheshimiwa sana, na hivyo kweli, baada ya kuanzisha makanisa kadhaa mashariki ya dunia yote. Huu utangulizi maarufu kutoka kwa mtume huenda ulisomwa na Tito, "Kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tuishirikiyo. Neema na iwe kwako na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu" (Tito 1: 4).

kisiwa cha Krete ambapo Tito aliachwa na Paulo kuongoza kanisa kilikaliwa na wenyeji wa kisiwa na Wayahudi ambao hawakujua ukweli wa Yesu Kristo (Tito 1: 12-14). Paulo alihisi kuwa ni wajibu wake kufuatilia kupitia kwa Tito kumwelekeza na kumtia moyo katika kuendeleza viongozi ndani ya kanisa la Krete. Kama mtume Paulo alivyoelekeza Tito katika kutafuta viongozi, Paulo pia alipendekeza jinsi Tito angewaelekeza viongozi ili waweze kukua katika imani yao kwa Kristo. Maelekezo yake ni pamoja na yale ya wanaume na wanawake wa umri wote (Tito 2: 1-8).

Ili kusaidia Tito kuendelea katika imani yake katika Kristo, Paulo alipendekeza Tito kuja Nikopoli na kuleta pamoja naye washirika wengine wawili wa kanisa (Tito 3: 12-13).

Mashirikisho: Kwa mara nyingine tena, Paulo anaona ni muhimu kuwafundisha viongozi wa kanisa kuwa waangalifu dhidi ya Wayahudi, wale ambao walitafuta kuongeza kazi kwa zawadi ya neema ambayo inazalisha wokovu. Anaonya dhidi ya wale ambao ni waasi waongo, hasa wale ambao waliendelea kudai tohara na kutii kanuni na sherehe za Sheria za Musa bado walikuwa muhimu (Tito 1: 10-11). Hii ni dhamira inayorudiwarudiwa kwa nyaraka za Paulo na katika kitabu cha Tito, anazidi hata kusema kwamba vinywa vyao lazima vinyamazizwe.

Vitendo Tekelezi: Mtume Paulo anastahili makini yetu tunapotazamia kwa Biblia kwa maelekezo ya jinsi ya kuishi maisha yanayompendeza Bwana wetu. Tunaweza kujifunza nini tunapaswa kuepuka vilevile kile tunachostahili kujitahidi kuiga. Paulo anapendekeza kwamba tutafute kuwa safi tunapoepuka mambo ambayo yatachafua akili zetu na fahamu. Na kisha Paulo anatoa kauli ambayo haitasahaulika kamwe: "Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai "(Tito 1:16). Kama Wakristo, ni lazima tujichunguze wenyewe kuwa na uhakika maisha yetu yanawiana na taaluma yetu ya imani katika Kristo (2 Wakorintho 13: 5).

Pamoja na onyo hili, Paulo pia anatuambia jinsi ya kuepuka kumkana Mungu: "Alituokoa kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu" (Tito 3: 5b- 6). Kwa kutafuta kufanywa upya kila siku kwa akili zetu na Roho Mtakatifu tunaweza kukua hadi tukawe Wakristo wanaomheshimu Mungu kwa njia tunavyoishi.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Tito
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries