settings icon
share icon

Kitabu cha Sefania

Mwandishi: Sefania 1: 1 inatambua mwandishi wa Kitabu cha Sefania kama Nabii Sefania. Jina Sefania linamaanisha "aliyetetewa na Mungu."

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Sefania huenda kiliandikwa kati ya 735 na 725 kk

Kusudi la Kuandika: Ujumbe wa Sefania wa hukumu na kutia moyo una mafundisho makubwa matatu: 1) Mungu ni mkuu juu ya mataifa yote. 2) waovu wataadhibiwa na wenye haki watathibitishwa katika siku ya hukumu. 3) Mungu huwabariki wale wanaotubu na kumwamini.

Mistari muhimu: Sefania 1:18, "Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA, bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha. "

Sefania 2: 3, "Mtafuteni Bwana, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu, huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya Bwana.".

Sefania 3:17, "Bwana, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; atakushangilia kwa furaha kuu, atakutuliza katika upendo wake, atakufurahia kwa kuimba."

Muhtasari kwa kifupi: Sefania anatangaza hukumu ya Bwana juu ya dunia nzima, juu ya Yuda, katika mataifa jirani, Yerusalemu, na mataifa yote. Haya yanafuatiwa na matangazo ya baraka za Bwana juu ya mataifa yote na hasa juu ya mabaki waaminifu wa watu wake katika Yuda.

Sefania alikuwa na ujasiri wa kusema waziwazi kwa sababu alijua alikuwa anatangaza Neno la Bwana. Kitabu chake kinaanza na "neno la Bwana" na kuishia na "asema Bwana." Alijua kwamba si miungu mingi ambayo watu waliabudu wala hata nguvu za jeshi la Waashuru zitaweza kuwaokoa. Mungu ni mwenye neema na huruma, lakini wakati maonyo yake yote yanapuuzwa, hukumu lazima itarajiwe. Siku ya Mungu ya hukumu imetajwa mara nyingi katika maandiko. Manabii waliliita kuwa ni "Siku ya Bwana." Walirejelea kwa matukio mbalimbali kama vile kuanguka kwa Yerusalemu kama madhihirisho ya Siku ya Mungu, ambayo kila moja yalilenga siku ya mwisho ya Bwana.

Ishara: Baraka za mwisho juu ya Sayuni zilizotangazwa katika mst. 14-20 hazitimizwi kwa kiasi kikubwa, kutuongoza kuhitimisha kwamba huu ni unabii wa kimasihi ambao unangojea kuja kwa Kristo kwa mara ya pili ili kukamilika. Bwana ameiondoa adhabu yetu tu kupitia kwa Kristo ambaye alikuja kufa kwa ajili ya dhambi za watu wake (Sefania 3:15; Yohana 3:16). Lakini Israeli bado haijamtambua Mwokozi wake wa kweli. Hii bado kutokea (Warumi 11: 25-27).

Ahadi ya amani na usalama kwa Israeli, wakati ambao Mfalme wao ako katikati yao, itatimizwa wakati Kristo atakaporudi kuhukumu ulimwengu na kuukomboa kwa ajili yake. Tu kama alivyopaa mbinguni baada ya kufufuka kwake, ndivyo Yeye atarudi na kuanzisha Yerusalemu mpya hapa duniani (Ufunuo 21). Wakati huo, ahadi zote za Mungu kwa Israeli zitatimizwa.

Vitendo Tekelezi: Kwa marekebisho machache katika majina na hali, nabii huyu wa karne ya saba KK angeweza kusimama katika mimbari yetu siku hizi na kutoa ujumbe huo wa hukumu ya waovu na matumaini kwa waaminifu. Sefania anatukumbusha kwamba Mungu anachukizwa na dhambi za kimaadili na za kidini za watu wake. Watu wa Mungu hawataepuka adhabu wakati wanatenda dhambi makusudi. Adhabu inaweza kuwa chungu, lakini lengo lake linaweza kuwa la ukombozi badala ya kuadhibu. Kutoepukika kwa adhabu ya uovu kunatoa faraja katika wakati inaonekana kwamba maovu hayadhibitiwi na yameshinda. Tuna uhuru wa kutomtii Mungu lakini si uhuru wa kuepuka matokeo ya adhabu ya uasi huo. Wale ambao ni waaminifu kwa Mungu wanaweza kuwa ni wachache sana, lakini yeye hawasahau.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Sefania
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries