settings icon
share icon

Kitabu cha Ruthu

Mwandishi: Kitabu cha Ruthu hakimtaji kwa wazi mtunzi wake. Utamaduni ni kwamba Kitabu cha Ruthu kiliandikwa na nabii Samweli.

Tarehe ya Kuandikwa: Tarehe halisi ya kuandikwa kwa Kitabu cha Ruthu haijulikani. Hata hivyo, mtazamo wa kawaida ni kati ya tarehe 1011 na 931 BC.

Kusudi la Kuandika: Kitabu cha Ruthu kiliandikwa kwa Wana wa Israeli. Kinafundisha kwamba upendo wa kweli wakati mwingine kunahitaji dhabihu thabiti. Bila kujali mengi katika maisha yetu, tunaweza kuishi kulingana na maagizo ya Mungu. Upendo wa kweli na ukarimu utatuzwa. Mungu huwabariki kwa wingi wale ambao wanatafuta kuishi maisha ya kutii. Kuishi kwa kutii hakuruhusu "ajali" katika mpango wa Mungu. Mungu anaonyesha huruma kwa wenye huruma.

Mistari muhimu: Ruthu 1:16, "Naye Ruthu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu.”

Ruthu 3: 9, "'Akasema, Ama! Ni nani wewe? Akamjibu Ni mimi Ruthu, mjakazi wako; uitande nguo yako juu ya mjakazi wako; kwa kuwa ndiwe wa jamaa aliye karibu.”

Ruthu 4:17, "Nao wale wanawake waliokuwa jirani wake wakampa jina, wakisema, Naomi amazaliwa mwana; wakamwita jina lake Obedi; yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.”

Muhtasari kwa Kifupi: Utunzi wa Kitabu cha Ruthu ulianza katika nchi ya makafiri wa Moabu, sehemu ya kaskazini mashariki mwa Bahari ya Chumvi, lakini kisha unaenda hadi Bethlehemu. Nakili hii ya kweli inafanyika wakati wa siku za kuhuzunisha kwa kuanguka na uasi wa Waisraeli, unaoitwa kipindi cha Waamuzi. Njaa inamlazimisha Elimeleki na mkewe Naomi, kutoka nyumbani kwao Israeli hadi nchi ya Moabu. Elimeleki anakufa na Naomi anaachwa na wanawe wawili, ambao wanaoa kwa haraka wasichana wawili wa Wamoabi, Orpa na Ruthu. Baadaye wanawe Naomi wote wanakufa, na Naomi anaachwa pekee na Orpa na Ruthu katika nchi wasioijua. Orpa anarudi kwa wazazi wake, lakini Ruthu anaamua kukaa na Naomi vile wanaposafiri kwenda Bethlehemu. Hii hadithi ya upendo na kujitolea kunatwaambia kuhusu ndoa ya Ruthu baadaye kwa mtu tajiri aitwaye Boazi, ambaye anamzalia mwana, Obedi, ambaye anakuwa babu wa Daudi na babu wa Yesu. Utiifu unamleta Ruthu katika ukoo wa Kristo.

Ishara: Mada kuu ya kitabu cha Ruthu ni ile ya jamaa-mkombozi. Boazi, jamaa wa Ruthu upande wa mumewe, alifanya kwa wajibu wake kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Musa kuwakomboa jamaa maskini na hali yake (Law. 25: 47-49). Hali hii inarudiwa na Kristo, ambaye alitukomboa sisi, umaskini wa kiroho, kutoka utumwa wa dhambi. Baba yetu wa mbinguni alimtuma mwanaye msalabani ili tuweze kuwa watoto wa Mungu na ndugu na dada wa Kristo. Kwa kuwa mkombozi wetu, sisi tukawa jamaa zake.

Vitendo tekelezi: Uhuru wa Mungu wetu mkuu unaonekana wazi katika hadithi ya Ruthu. Yeye alimwoongoza yeye kwa kila hatua na njia ya kuwa mtoto wake na kutimiza mpango wake wa kuwa babu wa Yesu Kristo (Mathayo 1: 5). Kwa njia hiyo hiyo, tuna uhakika kwamba Mungu ana mpango kwa kila mmoja wetu. Vile Naomi na Ruthu walimwamini Yeye kuwatolea wao, ndivyo itupasavyo nasi kumwamini.

Tunaona katika Ruthu mfano wa mwanamke mwaadilifu wa Mithali 31. Licha ya kujitolea kwa familia yake (Ruthu 1: 15-18; Mithali 31: 10-12) na kwa uaminifu kutegemea Mungu (Ruthu 2:12; Mithali 31:30), tunaona katika Ruthu mwanamke wa usemi wa kimungu. Maneno yake ni ya kupendeza, karimu na yenye heshima, kwa Naomi na Boazi wote. Mwanamke mwadilifu wa Mithali 31 "kufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake" (v. 26). Tunaweza kutafuta mbali na pana kupata mwanamke siku hizi wa dhamana kuwa mfano wetu bora kama Ruthu.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Ruthu
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries