settings icon
share icon

Kitabu cha Obadia

Mwandishi: Obadia mstari wa 1 unanakili mwandishi wa Kitabu cha Obadia kama Nabii Obadia.

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Obadia huenda kiliandikwa kati ya 848 na 840 kk

Kusudi la Kuandika: Obadia, kitabu kifupi zaidi katika Agano la Kale, kina urefu wa mistari 21 tu. Obadia ni nabii wa Mungu ambaye anatumia fursa hii kulaani Edomu kwa ajili ya dhambi dhidi ya Mungu na Israeli. Waedomi ni wazawa wa Esau na Waisraeli ni watoto wa ndugu yake pacha, Yakobo. Ugomvi baina ya ndugu umeathiri watoto wao kwa zaidi ya miaka 1,000. Mgawanyiko huu ulisababisha Waedomi kuwakataza Waisraeli wasivuke kupitia kwa nchi yao wakati wa Kutoka kwa Waisraeli kutoka Misri. Dhambi za Edomu za kiburi sasa zinahitaji neno la nguvu la hukumu kutoka kwa Bwana.

Mistari muhimu: Obadia mstari wa 4, "Ujapopanda juu kama tai, ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota, nitakushusha kutoka huko; asema Bwana ".

Obadia msitari wa 12, "Lakini usiitazame siku ya ndugu yako, siku ya mashaka yake. Wala usisimange juu ya wana wa Yuda siku ya kuangamizwa kwao, wala usinene maneno ya kiburi katika siku ya shida yao."

Obadia msitari wa 15, "Kwa maana hiyo siku ya Bwana i karibu juu ya mataifa yote; Kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; Malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe"

Muhtasari kwa kifupi: Ujumbe wa Obadia ni wa mwisho na ni wa hakika: Utawala wa Edomu utaharibiwa kabisa. Edomu imekuwa yenye kiburi, wakicheka kwa misiba ya Israeli na wakati majeshi ya adui yanashambulia Israeli na Waisraeli wanaomba msaada, Waedomi wanakataa na kuamua kupigana dhidi yao, si kwa ajili yao. Dhambi hizi za kiburi haziwezi kupuuzwa tena. Kitabu kinaisha kwa ahadi ya kutimiza na ukombozi wa Sayuni katika siku za mwisho wakati nchi itarejeshwa kwa watu wa Mungu Atakapowatawala.

Ishara: Mstari wa 21 wa Kitabu cha Obadia una ishara ya Kristo na Kanisa lake. "Tena waokozi watakwea juu ya mlima Sayuni ili kuuhukumu mlima wa Esau, na huo ufalme utakuwa ni mali ya Bwana" (NKJV). Hawa "waokozi" (pia waitwao "wakombozi" katika matoleo kadhaa) ni mitume wa Kristo, wahudumu wa neno, na hasa wahubiri wa Injili katika siku hizi za mwisho. Wanaitwa "waokozi," si kwa sababu wana wokovu wetu, bali kwa sababu wanahubiri wokovu kupitia kwa Injili ya Kristo na kutuonyesha njia ya kupata wokovu huo. Wao, na Neno ambalo linahubiriwa nao, ni njia ambayo kupitia kwayo habari njema ya wokovu inatolewa kwa watu wote. Wakati Kristo ndiye Mwokozi tu wa pekee ambaye alikuja peke yake kununua wokovu, na ndiye mwandishi wake, waokozi na wakombozi wa Injili watakuwa zaidi na zaidi washahidi mwisho wa kizazi unapokaribia.

Vitendo Tekelezi: Mungu atashinda kwa niaba yetu ikiwa tutabakia kuwa wa kweli kwake. Tofauti na Edomu, ni lazima tuwe tayari kusaidia wengine katika wakati wa mahitaji. Kiburi ni dhambi. Hatuna kitu chochote cha kujivunia isipokuwa Yesu Kristo na kile alichokifanya kwa ajili yetu.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Obadia
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries