settings icon
share icon

Kitabu cha Mambo ya Walawi

Mwandishi: Musa alikuwa mwandishi wa Kitabu cha Mambo ya Walawi.

Tarehe ya Kuandikwa: Kitabu cha Mambo ya Walawi kiliandikwa kati ya 1440 na 1400 KK.

Kusudi la Kuandika: Kwa sababu Waisraeli walifungwa katika Misri kwa miaka 400, dhana ya Mungu ilikuwa imebadilishwa na washirikina, Wamisri makafiri. Madhumuni ya Mambo ya Walawi ni kutoa taratibu na sheriaza kuongoza mwenye dhambi, watu ambao bado hawajakombolewa katika uhusiano wao na Mungu mtakatifu. Kuna msisitizo katika Mambo ya Walawi juu ya haja ya utakatifu binafsi katika kukubali Mungu Mtakatifu. Dhambi lazima zisafishwe kwa njia ya sadaka ya dhabihu sahihi (sura 8-10). Mada zingine zilizoshughulikiwa katika kitabu ni mlo (safi na vyakula chafu), kujifungua, na magonjwa ambayo yamedhibitiwa kwa makini (sura 11-15). Sura ya 16 inaeleza Siku ya Upatanisho wakati wa dhabihu la kila mwaka kwa ajili ya dhambi za watu zilizojumulishwa . Aidha, watu wa Mungu wanasitaili kujihadhari katika maisha yao binafsi, maadili, na kuishi kijamii, katika tofauti ya mazoea ya wakati huo ya makafiri yaliwazungusha (sura ya 17-22).

Mistari muhimu: Mambo ya Walawi 1: 4, "Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake."

Mambo ya Walawi 17:11, "Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi."

Mambo ya Walawi 19:18, "'Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama yako; Mimi ndimi BWANA."

Muhtasari kwa Kifupi: Sura 1-7 inaorodhesha sadaka zinazoitajika na walei na ukuhani wote. Sura 8-10 inaelezea wakfu wa Haruni na wanawe kwa ukuhani. Sura 11-16 ni maagizo ya aina mbalimbali ya uchafu. Sura 10 za mwisho ni miongozo ya Mungu kwa watu wake kwa vitendo vya utakatifu. Karamu mbalimbali zilianzishwa na watu katika kuabudu Yehovah Mungu, zilizoitishwa na kufanywa kwa mujibu wa sheria za Mungu. Baraka au laana ingeandamana kutunza au kupuuza amri za Mungu (sura ya 26). Viapo kwa Bwana zimeshughulikiwa katika Sura ya 27.

Dhamira ya kimsingi ya Mambo ya Walawi ni utakatifu. Mahitaji ya Mungu kwa utakatifu katika watu wake una asili kimsingi kwa utakatifu wake mwenyewe. Dhamira sambamba ni ile ya upatanisho. Utakatifu lazima uimarishwe mbele za Mungu, na utakatifu unaweza tu kufikiwa kwa njia ya upatanisho sahihi.

Ishara: Mengi ya mazoea ya matambiko ya kuabudu inajionyesha kwa njia nyingi utu na kazi ya Mkombozi wetu, Bwana Yesu Kristo. Waebrania 10 inatuambia kwamba Sheria ya Musa ni “ kivuli tu cha mambo mema ambayo yanakuja" na ambayo yalimaanisha kwamba dhabihu za kila siku zilizotolewa na makuhani kwa ajili ya dhambi za watu zilikuwa zinawakilisha dhabihu la mwisho-Yesu Kristo, ambaye dhabihu lake lingekuwa la mwisho kwa wakati wote kwa wale ambao wanatamwamini Yeye. Utakatifua uliotawanyika kwa muda tu kwa Sheria siku moja utabadilishwa kwa kufikia utakatifu kamilivu wakati Wakristo walibadilishana dhambi zao kwa utakatifu wa Kristo (2 Wakorintho 5:21).

Vitendo tekekelezi: Mungu anachukulia utakatifu wake kwa umakini sana na hivyo ndivyo tupasavyo pia. Mwenendo katika kanisa ya kisasa ni kuumba Mungu kwa mfano wetu wenyewe, tukimpa yeye sifa ambazo tungependa awe nazo badala ya zile Neno lake limeeleza. Utakatifu wa Mungu ni kamili, fahari yake ya uwezo mkumbwa, na yake "nuru isiyoweza kukaribiwa" (1 Timotheo 6:16) ni dhana geni kwa Wakristo wengi. Tumeitwa kutembea katika Nuru na kuweka mbali njia za giza katika maisha yetu ili tuweze kupendeza machoni pake. Mungu Mtakatifu hawezi kuvumilia wazi, dhambi zisizo na haya katika watu wake na utakatifu wake unamhitaji Yeye aziadhibu. Hatupaswi kuthubutu kuwa na mzaha katika mtazamo wetu kwa dhambi au chuki ya Mungu kwazo, wala kuifanya rahisi kwa njia yoyote.

Bwana asifiwe kwamba kwa sababu ya kifo cha Yesu kwa ajili yetu, hatutatoa tena dhabihu za wanyama. Mambo ya Walawi nzima inahusu kibadala. Kifo cha wanyama kilikuwa ni adhabu mbadala kwa wale ambao walifanya dhambi. Katika njia sawa hiyo, lakini bora zaidi, dhabihu la Yesu juu ya msalaba ilikuwa mbadala kwa ajili ya dhambi zetu. Sasa tunaweza kusimama mbele ya Mungu mwenye utakatifu bila hofu kwa sababu yeye anaona ndani yetu utukufu wa Kristo.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Mambo ya Walawi
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries