settings icon
share icon

Kitabu cha Malaki

Mwandishi: Malaki 1: 1 inatambulisha mwandishi wa Kitabu cha Malaki kama Nabii Malaki.

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Malaki kiliandikwa kati ya 440 na 400 kk

Kusudi la Kuandika: Kitabu cha Malaki ni ushauri: neno la Bwana kwa Israeli kupitia kwa Malaki (1: 1). Hii ilikuwa onyo la Mungu kwa njia ya Malaki kuwaambia watu kumrudia Mungu. Kama kitabu cha mwisho cha Agano la Kale likifunga, tangazo la haki ya Mungu na ahadi ya marejesho yake kupitia kwa Masihi linaimba katika masikio ya waisraeli. Miaka mia nne ya kimya inafuatia, ikiisha na ujumbe unaofanana kutoka kwa nabii wa Mungu aliyefuata, Yohana Mbatizaji, akitangaza, "Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia" (Mathayo 3: 2).

Mistari muhimu: Malaki 1: 6, "Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi umcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? Bwana wa majeshi anawauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, tumelidharau jina lako kwa njia gani?"

Malaki 3: 6-7, "Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo. Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, turudi kwa namna gani?"

Muhtasari kwa kifupi: Malaki aliandika maneno ya Bwana kwa watu wateule wa Mungu ambao walikuwa wamepotea, hasa makuhani waliokuwa wamegeuka kutoka kwa Bwana. Makuhani hawakuwa wanaichukulia maanani sadaka waliopaswa kumtolea Mungu. Wanyama waliokuwa na kasoro walikuwa wakitolewa sadaka ingawa sheria ilidai wanyama bila kasoro (Kumbukumbu 15:21). Wanaume wa Yuda walikuwa wanashughulika na wake za vijana wao bila uaminifu na kushangaa kwa nini Mungu hangekubali dhabihu zao. Pia, watu walikuwa hawatoi fungu la kumi kama wanapaswa kutoa (Mambo ya Walawi 27:30, 32). Lakini licha ya dhambi za watu, na kugeuka kutoka kwa Mungu, Malaki anarudia upendo wa Mungu kwa watu wake (Malaki 1: 1-5) na ahadi zake za Mtume atakayekuja (Malaki 2: 17-3: 5).

Ishara: Malaki 3: 1-6 ni unabii juu ya Yohana mbatizaji. Alikuwa Mtume wa Bwana aliyetumwa kuandaa njia (Mathayo 11:10) kwa ajili ya Masihi, Yesu Kristo. Yohana alihubiri toba na kubatiza katika jina la Bwana, na hivyo kuandaa njia kwa ajili ya ujio wa kwanza wa Yesu. Lakini Mtume ajaye "ghafla kwa Hekalu" ni Kristo mwenyewe katika ujio wake wa pili wakati atakapokuja katika uwezo na nguvu (Mathayo 24). Wakati huo, Yeye "atawatakasa wana wa Lawi" (mst. 3), kumaanisha ya kuwa wale ambao waliachilia Sheria ya Musa wangetaka wenyewe kutakaswa kutoka kwa dhambi kwa damu ya Mwokozi. Hapo ndipo wataweza kutoa "dhabihu katika haki" kwa sababu itakuwa haki ya Kristo iliyohesabiwa kwao kwa njia ya imani (2 Wakorintho 5:21).

Vitendo Tekelezi: Mungu hafurahishwi wakati hatutii amri zake. Atawalipa wale ambao wanamkupuuza. Kwa kuwa Mungu anachukia talaka (2:16), Mungu anachukulia agano la ndoa kwa umakini na Yeye hataki livunjwe. Tunapaswa kubakia kuwa wenye ukweli kwa mke wa ujana wetu maishani. Mungu anaiona mioyo yetu, hivyo Yeye anajua nia zetu ni gani; hakuna kitu kinachoweza kufichwa kutoka kwake. Atarudi na atakuwa Mwamuzi. Lakini ikiwa tutarudi kwake, atarudi kwetu (Malaki 3: 6).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Malaki
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries