settings icon
share icon

Kitabu cha Kutoka

Mwandishi: Musa alikuwa mwandishi wa kitabu cha Kutoka (Kutoka 17:14; 24: 4-7; 34:27).

Tarahe Ya Kuandikwa: Kitabu cha Kutoka kiliandikwa kati ya 1440 na 1400 KK

Kusudi la Kuandika: Neno "kutoka 'linamaanisha kuondoka. Katika majira ya Mungu, kuhama kwa Wanaisraeli kutoka Misri kuliashiria mwisho wa kipindi cha dhiki kwa kizazi cha Ibrahimu (Mwanzo 15:13), na mwanzo wa kutimiza ahadi ya agano kwa Ibrahimu kwamba kizazi chake kingekuwa si tu kuishi katika Nchi ya Ahadi, lakini pia kuzidisha na kuwa taifa kubwa (Mwanzo 12: 1-3, 7). Madhumuni ya kitabu yanaweza kuwa kudhihirisha asili ya ukuaji wa haraka wa kizazi cha Yakobo kutoka Misri kwenye uanzishwaji wa taifa la kitheokrasi katika Nchi yao ya Ahadi.

Mistari muhimu: Kutoka 1: 8, "Basi akaniuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu."

Kutoka 2: 24-25, "Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo. Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia."

Kutoka 12:27, "'Ndipo mtamwaambia, Ni dhabihu ya pasaka ya BWANA, kwa kuwa alipita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu. Hao watu wakainama vichwa na kusujudia. "

Kutoka 20: 2-3, "Mimi BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na Miungu mingine ila mimi."

Muhtasari kwa kifupi: Kutoka huanzia mahali ambapo Mwanzo huachia vile Mungu anashughulika na watu wake wateule, Wayahudi. Inaasilia matukio tangu wakati Israeli waliingia Misri kama wageni wa Yusufu, ambaye alikuwa na nguvu katika Misri, hadi walipokombolewa hatimaye kutoka utumwa wa kikatili ambapo walikuwa wameletwa na "... mfalme mpya ... ambaye hakumjua Yusufu "(Kutoka 1: 8).

Sura 1-14 inaelezea hali ya ukandamizaji wa Wayahudi chini ya Farao, kuteuliwa kwa Musa kama mkombozi wao, mapigo ya Mungu yaliyoletwa juu ya Misri kwa kiongozi wao kukataa kujiwasilisha kwake, na kuondoka kutoka Misri. Huru na nguvu za mkono wa Mungu zinaonekana katika miujiza ya mapigo-kumalizia na pigo la vifo vya vifungua mimba na taasisi ya kwanza ya Pasaka-ukombozi waWaisraeli, kutawanyika kwa bahari ya Shamu na uharibifu wa jeshi la Misri.

Sehemu ya kati ya Kutoka imetolewa kwa kuzurura katika jangwa na utoaji wa kimiujiza wa Mungu kwa watu wake. Lakini, hata kama aliwapa mkate kutoka mbinguni, maji matamu kutoka kwa yale machungu, maji kutoka kwa mwamba, ushindi juu ya wale ambao wangewaangamiza, sheria zake zilizoandikwa kwenye ubao wa mawe kwa mkono wake mwenyewe, na uwepo wake katika mfumo wa nguzo za moto na wingu, watu waliendelea kunung'unika na kuasi dhidi yake.

Sehemu ya tatu ya mwisho ya kitabu inaeleza ujenzi wa sanduku la Agano na mpango kwa ajili ya hema na yenye dhabihu mbalimbali, madhabahu, samani, sherehe, na mifumo ya kuabudu.

Ishara: Dhabihu mingi zilizoitajika na Wanaisraeli ni ishara ya sadaka ya mwisho, Pasaka ya Mwanakondoo wa Mungu, Yesu Kristo. Usiku wa pigo la mwisho juu ya Misri, mwanakondoo asiyekuwa na dosari aliuliwa na damu yake kupakwa kwa milango ya nyumba ya watu wa Mungu, ili kuwalinda dhidi ya malaika wa kifo. Hii ni ishara ya Yesu, Mwanakondoo wa Mungu bila doa au kilema (1 Petro 1:19), ambaye damu yake ilipakwa kwetu na kutuhakikishia uzima wa milele . Miongoni mwa ishara ya Kristo katika kitabu cha Kutoka ni hadithi ya maji kutoka kwenye mwamba katika Kutoka 17: 6. Kama Musa alivyoupiga mwamba na kutoa maji ya kupeana uhai watu wakakunywa, ndivyo Mungu alipiga Mwamba wa wokovu wetu, kumsulubisha Yeye kwa ajili ya dhambi zetu, na kutoka kwa mwamba ikakucha zawadi ya maji ya uhai (Yohana 4:10) . Utoaji wa mana kule jangwani ni ishara kamilifu ya Kristo, mkate wa uzima (Yohana 6:48), uliotolewa na Mungu ili kutupa uzima.

Vitendo tekelezi: Sheria ya Musa ilitolewa katika sehemu ili kuonyesha wanadamu kwamba walikuwa hawana uwezo wa kuiweka. Tunashindwa kumpendeza Mungu kwa kutunza sheria; Kwa hivyo, Paulo hatusihi "Hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki." (Wagalatia 2:16).

Utoaji wa Mungu kwa ajili ya Wana Wa Israeli, tangu ukombozi kutoka utumwa hadi mana na tombo katika jangwa, ni dalili za wazi za utoaji wa neema kwa watu wake. Mungu ameahidi atatupatia mahitaji yetu yote,”Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingine katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.” (1 Wakorintho 1: 9)

Twasitahili kumtegemea Bwana, kwa kuwaYeye anaweza kutuokoa kutoka kwa lolote. Lakini Mungu hairuhusu dhambi kwenda bila kuadhibiwa milele. Matokeo yake, tunaweza kumtumaini katika kulipiza kisasi chake na haki. Wakati Mungu anatutoa kutoka hali mbaya, hatupaswi kutafuta kurudi nyuma. Wakati Mungu anatuitaji, Anatarajia tukubali, lakini wakati huo huo Yeye hutoa neema na huruma kwa sababu anajua kwamba, juu yetu wenyewe, sisi hatutaweza kutii vikamilifu.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Kutoka
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries