settings icon
share icon

Kitabu cha Kumbukumbu La Torati

Mwandishi: Musa aliandika kitabu cha Kumbukumbu La Torati, ambacho kwa kweli ni mkusanyiko wa mahubiri yake kwa Israeli tu kabla ya wao kuvuka Yordani. "Haya ndiyo maneno aliyowaambia Musa " (1: 1). Mtu mwingine (Yoshua, labda) uenda ndiye aliandika sura ya mwisho.

Tarehe ya Kuandia: Mahubiri haya yalipeanwa wakati siku 40 kipindi kabla ya Israeli kuingia nchi ya ahadi. Mahubiri ya kwanza yalitolewa siku ya 1 ya mwezi 11 (1: 3), na Israeli walivuka Yordani siku 70 baadaye, tarehe 10 ya mwezi 1 (Yoshua 4:19). Ondoa siku 30 za maombolezo baada ya kifo cha Musa (Kumbukumbu La Torati 34: 8), na Tumebakisha siku 40. Mwaka ulikuwa 1410 KK

Kusudi la Kuandika: Kizazi kipya cha Israeli kilikuwa karibu kuingia Nchi ya Ahadi. Umati huu haukuwa umepitia muujiza katika bahari ya Shamu au kusikia sheria zilizotolewa katika Sinai, na wao walikuwa karibu kuingia katika nchi mpya na hatari nyingi na majaribu. Kitabu cha Kumbukumbu La Torati kilitolewa kwa kuwakumbusha sheria za Mungu na nguvu za Mungu.

Mistari muhimu: "Msiliongeze neon niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za BWANA, Mungu wenu, niwaamuruzo." (Kumbukumbu La Torati 4: 2)

"Sikiza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja. Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya ninayokuamuruleo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. "(Kumbukumbu La Torati 6: 4-7)

"Akawaambia, Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo nashuhudia kwenu hivi leo; nayo waamuruni watoto wenu, wayatunze na kuyafanya maneno yote ya torati hii. Kwa maana si jambo lisilofaa kwenu; maana, ni maisha yenu, na jambo hili mtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki. "(Kumbukumbu la Torati 32: 46-47)

Muhtasari kwa kifupi: Wanaisraeli wameamriwa kukumbuka mambo manne: uaminifu wa Mungu, utakatifu wa Mungu, baraka za Mungu, na maonyo ya Mungu. Sura tatu za mwanzo zinarejea safari kutoka Misri na eneo lao la sasa, Moabu. Sura ya 4 ni mwito wa utii, kwa kuwa waaminifu kwa Mungu ambaye alikuwa mwaminifu kwao.

Sura ya 5 hadi 26 ni marudio ya sheria. Amri Kumi, sheria juu ya dhabihu na siku maalum, na sheria zingine kutolewa kwa kizazi kipya. Baraka inahaidiwa kwa wale wanaotii (5:29; 6: 17-19; 11: 13-15), na njaa inahaidiwa kwa wale wanaovunja sheria (11: 16-17).

Dhamira ya baraka na laana inaendeleshwa katika sura 27-30. Sehemu hii ya kitabu inaishia kwa kuweka wazi uamuzi mbele ya Israeli: "nimeweka mbele yanu uzima na mauti, baraka na laana." Mapenzi ya Mungu kwa watu wake hupatikana katika kile inapendekeza: "chagua uzima" (30:19) .

Katika sura ya mwisho, Musa anawatia moyo watu, anamteua mwenye anachukua mahali pake , Yoshua, anaandika wimbo; na anatoa baraka za mwisho kwa kila kabila la Israeli. Sura ya 34 inahusiana na mazingira ya kifo cha Musa. Yeye alipanda Mlima Pisga, ambapo Bwana alimwonyesha Nchi ya Ahadi ambayo angeweza kuingia. Katika umri wa miaka 120, lakini bado na macho mazuri na nguvu za ujana, Musa alikufa katika uwepo wa Bwana. Kitabu cha Kumbukumbu La Torati kinaishia na tanzia fupi juu ya nabii huyu mkubwa.

Ishara: Dhamira mingi za agano Jipya yapo katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati. Ya maana miongoni mwao ni umuhimu wa kutunza kikamilifu Sheria za Musa na ugumu wa kufanya hivyo. Dhabihu zisizo na mwisho ni muhimu kwa upatanisho wa dhambi za watu- ambao waliendelea kuvunja Sheria-ambapo wangepata timisho lao katika mwisho "mara moja ya mwisho" dhabihu la Kristo (Waebrania 10:10). Kwa sababu ya kazi ya upatanisho wake juu ya msalaba,hatutaitaji dhabihu zingine kwa ajili ya dhambi.

Mungu kuchagua Wanaisraeli kama watu Wake maalum ni ishara Yeye kuchagua wale ambao watamwamini Kristo (1 Petro 2: 9). Katika Kumbukumbu La Torati 18: 15-19, Musa anatabiri juu ya nabii mwangine- hatimaye atakuja Nabii ambaye ni Mesia. Kama Musa, atapokea na kuhubiri ufunuo wa Mungu na ataongoza watu wake (Yohana 6:14; 7:40).

Vitendo tekelezi: kitabu cha Kumbukumbu La Torati inasisitiza umuhimu wa Neno la Mungu. Ni sehemu muhimu ya maisha yetu. Ingawa sisi hatuko tena chini ya sheria ya Agano la Kale, sisi bado tungali na wajibu wa kuwasilisha mapenzi ya Mungu katika maisha yetu. Utii wa rahisi huleta baraka, na dhambi ina madhara yake.

Hakuna hata mmoja wetu aliye "juu ya sheria." Hata Musa, kiongozi na nabii aliyechaguliwa na Mungu, alitakiwa kutii. Sababu ya kutoruhusiwa kuingia Nchi ya Ahadi ilikuwa kwamba yeye aliasi amri wazi za Bwana (Hesabu 20:13).

Wakati wa kujaribiwa kwake jangwani, Yesu alinukuu kutoka katika kitabu cha Kumbukumbu La Torati mara tatu (Mathayo 4). Kwa kufanya hivyo, Yesu anatuelezea umuhimu wa kuficha Neno la Mungu katika mioyo yetu ili tusiweze fanya dhambi dhidi yake (Zaburi 119: 11).

Vile Israeli ilikumbuka uaminifu wa Mungu, hata sisi pia. Kuvuka bahari ya Shamu, uwepo takatifu katika Sinai, na baraka za mana kule jangwani ni kitu cha kututia moyo sisi pia. Njia kubwa ya kuhifadhi kwenda mbele ni kuchukua muda wa kuangalia nyuma na kuona kile Mungu amefanya.

Pia tuna picha nzuri katika Kumbukumbu La Torati ya Mungu mwenye upendo ambaye anatamani uhusiano na watoto wake. Bwana anataja upendo kama sababu ya kutoa Israeli kutoka Misri "kwa mkono wenye nguvu" na kuwakomboa (Kumbukumbu La Torati 7: 7-9). Jambo gani la ajabu kama kuwa huru kutoka katika utumwa wa dhambi na kupendwa na Mungu mwenye nguvu zote!

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Kumbukumbu La Torati
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries