settings icon
share icon

Kitabu cha Hosea

Mwandishi: Hosea 1: 1 inatambua mwandishi wa kitabu kama nabii Hosea. Ni rekodi binafsi ya Hosea ya ujumbe wake wa kinabii kwa watoto wa Mungu na ulimwengu. Hosea ndiye tu nabii wa Israeli ambaye aliacha unabii andishi ambao ulinakiliwa wakati wa miaka ya baadaye ya maisha yake.

Tarehe ya kuandikwa: Hosea, mwana wa Beeri, alitabiri kwa muda kabisa, tangia 785-725 kk. Kitabu cha Hosea huenda kiliandikwa kati ya 755 na 725 kk

Kusudi la Kuandika: Hosea aliandika kitabu hiki kuwakumbusha waisraeli-na sisi-kwamba Mungu wetu ni mwenye upendo ambaye uaminifu kwa watu wake kwa ahadi hautingiziki. Licha ya waisraeli kuendelea kuabudu miungu ya uongo, upendo wa Mungu imara unaonekana katika mateso ya muda mrefu ya mume wa mke asiyekuwa mwaminifu. Ujumbe wa Hosea pia ni moja ya onyo kwa wale ambao wataasi dhidi ya upendo wa Mungu. Kupitia kwa ishara ya ndoa ya Hosea na Gomeri, upendo wa Mungu kwa taifa la waabudu sanamu la Israeli unaonyeshwa katika sitiari murwa katika mada za dhambi, hukumu, na upendo wenye kusamehe.

Mistari muhimu: Hosea 1: 2, "Hapo kwanza Bwana aliponena kwa kinywa cha Hosea, Bwana alimwambia Hosea, enenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana.

Hosea 2:23, "Nami nitapanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe; Nami nitamrehemu yeye asiyepewa rehema; name nitawaambia wale wasiokuwa watu wangu, ninyi ndinyi watu wangu; nao watasema, Wewe ndiwe Mungu wangu. "

Hosea 6: 6, "Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa."

Hosea 14: 2-4, "Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie Bwana; mkamwambie, ondoa maovu yetu, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo mtakavyotoa sadaka za midomo yetukana kwamba ng’ombe. Ashuru hatatuokoa; hatutapanda farasi; wala hatutaiambia tena kazi ya mikono yetu, ninyi ndinyi miungu yetu; maana kwako wewe wasio na baba hupata rehema. Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha."

Muhtasari kwa kifupi: Kitabu cha Hosea kinaweza kugawanywa katika sehemu mbili: (1) Hosea 1: 1-3: 5 ni maelezo ya mke asiyekuwa mwaminfu na mume mwaminifu, ambayo ni ishara ya kukosa uaminifu kwa Israeli kwa Mungu kupitia kuabadu sanamu, na ( 2) Hosea 3: 6-14: 9 ina kulaaniwa kwa Israeli, hasa Samaria, kwa ajili ya kuabudu sanamu na marejesho yake ya baadaye.

Sehemu ya kwanza ya kitabu ina mashairi matatu bainifu yanayoelezea jinsi watoto wa Mungu walikurudi mara kwa mara kuabadu sanamu. Mungu anaamuru Hosea kuoa Gomeri, lakini baada ya kuzaa naye watoto watatu, yeye anamtoroka Hosea na kwenda kwa wapenzi wake. Ishara ya mkazo inaweza kuonekana wazi katika sura ya kwanza kama Hosea anapolinganisha vitendo vya Israel kama kugeuka kutoka kwa ndoa na kuishi kama malaya. Sehemu ya pili ina shutuma ya Hosea kwa waisraeli lakini ikifuatiwa na ahadi na huruma za Mungu.

Kitabu cha Hosea ni nakili ya kiunabii ya upendo wa Mungu usiopunguza kwa watoto wake. Tangu mwanzo viumbe vya Mungu visivyo na shukrani na visivyostahili vimekuwa vikikubali upendo wa Mungu, neema na huruma wakati bado haviwezi kujiepusha na uovu wao.

Sehemu ya mwisho ya Hosea inaonyesha jinsi upendo wa Mungu kwa mara nyingine tena unawarudisha watoto wake kama vile anasahau matendo yao maovu wakati wakimrudia kwa moyo wa kutubu. Ujumbe wa kinabii wa Hosea unatabiri kuja kwa M asihi wa Israeli miaka 700 katika siku zijazo. Hosea ananukuliwa mara nyingi katika Agano Jipya.

Ishara: Hosea 2:23 ni ujumbe wa ajabu wa kinabii kutoka kwa Mungu kuwashirikisha watu wa mataifa mengine [wasio Wayahudi] kama watoto wake kama ilivyorekodiwa pia katika Warumi 9:25 na 1 Petro 2:10. Watu wa mataifa mengine kiasili si watu wa Mungu, lakini kwa huruma na neema yake, yeye amemtoa Yesu Kristo, na kwa imani kwake tumepandikwa kwa mti wa watu wake (Warumi 11: 11-18). Huu ni ukweli wa ajabu juu ya Kanisa, ambayo inaitwa fumbo/siri kwa sababu kabla ya Kristo, watu wa Mungu walichukuliwa kuwa tu Wayahudi pekee. Kristo alipokuja, Wayahudi walipofishwa kwa muda mpaka "idadi kamili ya watu wa mataifa mengine waliingizwa ndani" (Warumi 11:25).

Vitendo Tekelezi: Kitabu cha Hosea kinatuhakikishia upendo wa Mungu usio na masharti kwa watu wake. Lakini pia ni mfano wa jinsi Mungu anafedheheshwa na kukasirishwa na matendo ya watoto wake. Jinsi gani mtoto ambaye anapewa upendo mwingi, huruma na neema anamkosea heshima Baba yake? Bado, tumefanya tu hivyo kwa karne nyingi. Tunapochunguza jinsi Waisraeli walivyomuasi Mungu, tunahitaji tusiangalie zaidi ya kioo kilicho mbele yetu ili kuona uakisi wa waisraeli wale wale.

Tu kwa kukumbuka ni kiasi gani Mungu amefanya kwa kila mmoja wetu ndio tutakuwa na uwezo kuepuka kumkataa mmoja ambaye anaweza kutupa uzima wa milele katika utukufu badala ya jehanamu tunayostahili. Ni muhimu kwamba tujifunze kuheshimu Muumba wetu. Hosea ametuonyesha kwamba wakati tunafanya makosa, kama tuna moyo unayohuzunika na ahadi ya kutubu basi Mungu tena ataonyesha upendo wake usioisha kamwe kwetu (1 Yohana 1: 9).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Hosea
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries