settings icon
share icon

Kitabu cha Hesabu

Mtunzi/Mwandishi: Musa alikuwa mwandishi wa Kitabu cha Hesabu.

Tarehe ya Kuandikwa: Kitabu cha Hesabu kiliandikwa kati ya 1440 na 1400 KK

Kusudi la Kuandika: Ujumbe wa Kitabu cha Hesabu, umeenea kote na hujalenga kipindi Fulani cha wakati.Kinawakumbusha waumini vita vya kiroho ambavyo wao wanashiriki, kwani Hesabu ni kitabu cha huduma na kutembea kwa watu wa Mungu. Kitabu cha Hesabu kimsingi kiliuanganisha pengo kati ya Wana Wa Israeli kupokea sheria (Kutoka na Mambo Ya Walawi) na kuwaandaa wao kuingia katika Nchi ya Ahadi (Kumbukumbu La Torati na Yoshua).

Mistari muhimu: Hesabu 6: 24-26, "BWANA akubarikie, na kukulinda; BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; BAWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani."

Hesabu 12: 6-8, "Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi BWANA, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote, Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu huyo Musa?”

Hesabu 14: 30-34, "Hakika yangu hamtaingia ninyi katika nchi, ambayo niliinua mkono wangu ya kwamba nitawaketisha humo, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni. Lakini Watoto wenu, ambao mlisema watakuwa mateka, ndio nitakaowaleta na kuwatia ndani, nao wataijua nchi ninyi mliyoikataa. Lakini katiak habari zenu, mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili. Kisha Watoto wenu watakuwa wachungaji jangwani muda wa miaka arobaini nao watachukua mzigo wa uasherati wenu, ata mizoga yenu itakapoangamia jangwani. Kwa hesabu ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi,yaani, siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arobaini, nanyi mtakujua kufarikana kwangu ".

Muhtasari kwa Kifupi: Matukio mengi ya kitabu cha Hesabu hufanyika katika jangwa, hasa kati ya mwaka wa pili na miaka arobaini ya kuzurura kwa Waisraeli. Sura za kwanza 25 za kitabu zinatarihi uzoefu wa kizazi cha kwanza cha Israeli katika jangwa, huku sehemu iliyobaki ya kitabu inaelezea uzoefu wa kizazi cha pili. Dhamira ya utiifu na uasi ikifuatiwa na toba na baraka zimekita mizizi kitabu chote, vile vile Agano lote la kale.

Dhamira ya utakatifu wa Mungu unaendeleshwa kutoka kitabu cha Mambo ya Walawi hadi katika kitabu cha Hesabu, ambayo inaonyesha maelezo ya Mungu na maandalizi ya watu wake kuingia Nchi ya Ahadi ya Kanaani. Umuhimu wa kitabu cha Hesabu umeonyeshwa kwa kurejelewa kwake katika Agano Jipya mara nyingi. Roho Mtakatifu unazingatia umakini maalum kwa kitabu cha Hesabu katika 1 Wakorintho 10: 1-12. Maneno "mambo hayo yote yaliwafanyikia wao kwa mifano" hurejelea dhambi za Waisraeli na hasira ya Mungu kwao nao.

Katika Warumi 11:22, Paulo anaongea kuhusu "wema na ukali wa Mungu." Kwamba, kwa kifupi, ni ujumbe wa Hesabu. Ukali wa Mungu unaonekana katika kifo cha kizazi kilicho asi katika jangwa, wale ambao kamwe hawakuingia Nchi ya Ahadi. Wema wa Mungu unatambulika katika kizazi kipya. Mungu alilinda, akahifadhi, na kuwatolea hawa watu mpaka wakaimiliki nchi. Hii inatukumbusha juu ya haki na upendo wa Mungu, ambao daima ni huru mwafaka.

Ishara: Mahitaji ya Mungu kwa utakatifu katika watu wake kabisa na hatimaye umeridhishwa katika Yesu Kristo, ambaye alikuja kutimiza sheria kwa niaba yetu (Mathayo 5:17). Dhana ya Masihi aliyeahidiwa inaenea kitabuni. Hadithi katika sura ya 19 ya dhabihu la mtamba mwekundu "bila kasoro ya dosari" inabainisha Kristo, Mwana-kondoo wa Mungu bila doa au dosari ambaye alitolewa kafara kwa ajili ya dhambi zetu. Picha ya nyoka wa shaba iliyoinuliwa juu ya mti kutoa uponyaji wa kimwili (sura 21) pia inabainisha kuinuliwa kwa Kristo, pengine juu ya msalaba, au katika huduma ya neno, ili yeyote atamtazamia Yeye kwa imani ataezapata uponyaji wa kiroho.

Katika sura ya 24, mizimuni ya nne ya Balaamu inazungumzia nyota na fimbo ambaye itainuka kutoka kwa Yakobo. Hapa ni unabii wa Kristo ambaye anaitwa "nyota ya asubuhi" katika Ufunuo 22: 16 kwa utukufu wake, mwangaza, na kushinda, na kwa ajili ya mwangaza unaokuja kutoka kwake. Yeye pia anaweza kuitwa fimbo, yaani, mbeba fimbo, kwa sababu ya mamlaka yake. Yeye si tu ana jina la mfalme, bali ana ufalme, na anatawala kwa fimbo ya neema, huruma na haki.

Vitendo tekelezi: Mada kuu ya kiteolojia inayoendeleshwa katika Agano Jipya kutoka kitabu cha Hesabu ni kwamba dhambi na kutoamini, hasa uasi, huvuna hukumu ya Mungu. Wakorintho wa Kwanza inasema bayana-na Waebrania 3: 7-4: 13 inadokeza kwa nguvu -kwamba matukio haya yaliandikwa kama mifano kwa waumini kuchunguza na kuepuka. Hatupaswi "kuweka mioyo yetu juu ya mambo mabaya" (mstari 6.), Au kuwa wazinzi (v. 8), au kumjaribu Mungu (v. 9) au kunung’unika na kulalamika (v 10).

Kama vile Waisraeli walizurura jangwani miaka 40 kwa sababu ya uasi wao, hivyo pia wakati mwingine Mungu anaturuhusu sisi kuzunguka mbali naye na kuteseka upwekeni na ukosefu wa baraka wakati sisi tunaasi dhidi yake. Lakini Mungu ni mwaminifu na wa haki, na kama vile yeye aliwarejesha Waisraeli kwa nafasi yao katika moyo wake, Yeye daima atarejesha Wakristo kwa nafasi ya baraka na ushirika wa karibu pamoja naye kama sisi tutatubu na kurudi kwake (1 Yohana 1: 9 ).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Hesabu
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries