settings icon
share icon

Kitabu cha Habakuki

Mwandishi: Habakuki 1: 1 Kinatambua Kitabu cha Habakuki kama ushauri kutoka kwa Nabii Habakuki.

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Habakuki huenda kiliandikwa kati ya 610 na 605 kk

Kusudi la Kuandika: Habakuki alikuwa anashangaa kwa nini Mungu alikuwa anawaruhusu watu wake wateule wapitie kwa mateso ya sasa katika mikono ya maadui zao. Mungu anajibu na imani ya Habakuki inarejeshwa.

Mistari muhimu: Habakuki 1: 2, "Ee Bwana, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa."

Habakuki 1: 5, "Angalieni, enyi mlio kati ya mataifa, katazameni, kastaajabuni sana; kwa maana mimi natenda tendo siku zenu, ambalo hamtaliamini hata mkiambiwa. "

Habakuki 1:12, "Ee Bwana, Mungu wangu, mtakatifu wangu, wewe si wa milele? Hatutakufa. Ee Bwana, umemwandikia hukumu, nawe, Ee jabalĂ­, umemweka imara ili aadhibishwe. "

Habakuki 2: 2-4, "Bwana akanijibu, akasema, iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii vado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia. Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake. " Habakuki 2:20 "Lakini Bwana yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake. "

Habakuki 3: 2, "Ee Bwana, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee Bwana fufuakazi yako katikati ya miaka; katikati ya miaka tangaza habari yake; katika ghadhabu kumbuka rehema.

Habakuki 3:19, "Yehova, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka."

Muhtasari kwa kifupi: Kitabu cha Habakuki kinaanza na Habakuki akilia kwa Mungu kwa jibu ni kwa nini watu wateule wa Mungu wanaruhusiwa kuteseka katika utumwa wao (Habakuki 1: 1-4). Bwana anatoa jibu lake kwa Habakuki akisema kimsingi kwamba, "haungeamini hata nigekuambia" (Habakuki 1: 5-11). Habakuki kisha anafuata kwa kusema, "wewe ni Mungu, lakini bado niambie zaidi kuhusu ni kwa nini haya yanafanyika" (Habakuki 1: 17-2: 1). Kisha Mungu anamjibu tena na kumpa habari zaidi, kisha anaambia dunia kuwa kimya mbele zake (Habakuki 2: 2-20). Kisha Habakuki anaandika maombi akielezea imani yake imara katika Mungu, licha ya majaribu haya (Habakuki 3: 1-19).

Ishara: Mtume Paulo ananukuu Habakuki 2: 4 kwenye hafla mbili tofauti (Warumi 1:17, Wagalatia 3:11) ili kusisitiza mafundisho ya kuhesabiwa haki kwa imani. Imani ambayo ni zawadi ya Mungu na inayopatikana kupitia kwa Kristo ni imani inayookoa mara moja(Waefeso 2: 8-9) na imani inayodumu maishani. Tunapata uzima wa milele kwa imani na kuishi maisha ya Kikristo kwa imani hiyo. Tofauti na "wenye kiburi" katika mwanzo wa mstari, moyo wake hakika hauko ndani yake (NASB) na matakwa yake si imara(NIV). Lakini sisi ambao ni waadilifu kwa imani katika Kristo tumefanywa wenye haki kabisa kwa sababu amebadilishana haki yake kamili kwa ajili ya dhambi zetu (2 Wakorintho 5:21), na ametuwezesha kuishi kwa imani.

Vitendo Tekelezi: Tekelezo kwa msomaji wa Habakuki ni kuwa imeruhusiwa kuuliza kile ambacho Mungu anafanya, ingawa kwa heshima na unyenyekevu. Wakati mwingine haidhihiriki kwetu kinachoendelea, hasa kama tumetupwa katika mateso kwa kipindi cha muda au kama inaonekana adui zetu wanafanikiwa wakati sisi tuko bure. Kitabu cha Habakuki, hata hivyo, kinathibitisha kwamba Mungu ni mkuu, Mungu mwenye nguvu ambaye anadhibiti kila kitu. Tunapaswa tu kutulia na kujua kuwa ako kazini. Yeye ni anayesema kuwa ni Yeye na anatimiza ahadi zake. Atawaadhibu waovu. Hata wakati hatuwezi kuona hivyo, Yeye bado amekalia kiti cha enzi cha ulimwengu. Tunahitaji kukaa makini kwa hili: "Yehova, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka."(Habakuki 3:19). Kutuwezesha kwenda kwa miinuko ni kutupeleka mahali palipoinuka pamoja naye ambapo tunatengwa na dunia. Pengine njia tunayopaswa kwenda ili itufikishe huko ni kupitia kwa mateso na huzuni, lakini kama tutapumzika kwake na kumwamini Yeye, tutatokea anapotutaka.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Habakuki
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries