settings icon
share icon

Kitabu cha Ezekieli

Mwandishi: Nabii Ezekieli ndiye mwandishi wa Kitabu (Ezekieli 1: 3). Alikuwa Yule Yule katika Yeremia na Danieli.

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Ezekieli huenda kiliandikwa kati ya 593 na 565 kk wakati wa utumwa wa Babeli kwa Wayahudi.

Kusudi la Kuandika: Ezekieli alihudumu kwa kizazi chake ambacho kilikuwa kinazidi kutenda dhambi na kutamaushwa kabisa. Kwa njia ya huduma yake ya kinabii alijaribu kuwaleta katika toba ya haraka na kwa kujiamini katika siku zijazo. Alifundisha kwamba: (1) Mungu hufanya kazi kupitia kwa watumwa wanadamu, (2) Hata katika kushindwa na kukata tamaa watu wa Mungu wana haja ya kuthibitisha ukuu wa Mungu, (3) Neno la Mungu kamwe halishindwi, (4) Mungu yupo na anaweza kuabudiwa mahali popote, (5) Watu lazima wamtii Mungu ikiwa wanatarajia kupokea baraka, na (6) Ufalme wa Mungu utakuja.

Mistari muhimu: Ezekieli 2: 3-6, "Akaniambia, Mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi; wao na baba zao wamekosa juu yangu, naam, hata hivi leo. Na wana hao wana nyuso zisizo na haya, na mioyo yao ni migumu. Mimi nakutuma kwa hao; nawe utawaambia, Bwana Mungu asema hivi. Nao kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia, (maana ndio nyumba ya kuasi hao), hata hivyo watajua ya kwamba nabii amekuwako miongoni mwao. Na wewe, mwanadamu, usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao, ijapokuwa miiba na michongoma I pamoja nawe, nawe unakaa katikati ya nge; usiyaogope maneno yao, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba yenye kuasi.'"

Ezekieli 18: 4, "Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa."

Ezekieli 28: 12-14, "'Mwanadamu, umfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, umwambie, Bwana Mungu asema hivi; wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri. Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari. Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; name nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. "

Ezekieli 33:11, "Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghahiri mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghahirini, ghahirini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli? '"

Ezekieli 48:35, "Na jina la mji huo tangu siku litakuwa hili, Bwana yuko hapo."

Muhtasari kwa kifupi: Ni kwa jinsi gani unaweza kukabiliana na dunia ambayo imepotozwa? Ezekieli, alitazamia kuanza huduma ya maisha yake kama kuhani katika umri wa miaka thelathini, aling'olewa kutoka nchi yake na kupelekwa Babeli katika umri wa miaka ishirini na mitano. Kwa miaka mitano aliteseka katika kukata tamaa. Katika umri wa miaka thelathini maono makuu ya utukufu wa Bwana yalimtawala katika Babeli. kuhani / nabii aligundua Mungu hakukandamizwa kwa shutuma z anchi asili ya Ezekieli. Badala yake, Yeye ni Mungu mwenye haki anayeamuru na kudhibiti watu na mataifa. Katika Babeli, Mungu alimpa Ezekieli Neno lake kwa watu. Uzoefu wa wito wake ulimbadilisha Ezekieli. Yeye akawa mcha wa kujitolea kwa Neno la Mungu. Alitambua kuwa hakuwa na kitu binafsi kwa kusaidia mateka katika hali yao ya uchungu, lakini alishawishika Neno la Mungu lilizungumza na hali zao na litawapa ushindi. Ezekieli alitumika mbinu mbalimbali kufikisha Neno la Mungu kwa watu wake. Yeye alitumia sanaa katika kuchora picha ya Yerusalemu, hatua za mifano na mwenendo usio wa kawaida ili kupata nadhari yao. Yeye alikata nywele zake na ndevu kuonyesha kile Mungu atafanya kwa Yerusalemu na wakazi wake.

Kitabu cha Ezekieli kinaweza kugawanywa katika sehemu nne:
Sura 1-24: unabii juu ya uharibifu wa Yerusalemu
Sura 25-32: unabii wa hukumu ya Mungu juu ya mataifa jirani
Sura ya 33: wito wa mwisho kwa watu wa Israeli watubu
Sura 34-48: unabii kuhusu marejesho ya baadaye ya Israeli

Ishara: Ezekieli 34 ni sura ambayo Mungu anatangaza kwamba viongozi wa Israeli kuwa wachungaji wa uongo kwa ajili ya huduma zao mbovu kwa watu wake. Badala ya kuwatunza kondoo wa Israeli, walijitunza wenyewe. Walikula vizuri, wakavalishwa vizuri na kutunzwa vizuri na wale watu ambao waliwekwa juu yao(Ezekieli 34: 1-3). Kwa upande mwingine, Yesu ni mchungaji mwema ambaye huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo na ambaye huwalinda kutokana na mbwa mwitu ambao huenda wakaharibu kundi la kondoo wake(Yohana 10: 11-12). Mstari wa 4 wa sura ya 34 unaeleza kuhusu watu ambao wachungaji walishindwa kuhudumia kama wanyonge, wagonjwa, wenye majeraha na waliopotea. Yesu ndiye mganga mkuu ambaye huponya majeraha yetu ya kiroho (Isaya 53: 5) kwa kifo chake msalabani. Yeye ndiye anatafuta na kuokoa yule aliyepotea (Luka 19:10).

Vitendo Tekelezi: Kitabu cha Ezekieli kinatuita tujiunge katika kukutana safi na kunakoishi na Mungu wa Ibrahimu, Musa na manabii. Lazima tuwe washindi au sisi tutashindwa. Ezekieli alitupa changamoto ya: kuzoea maono ya kubadilisha maisha ya nguvu za Mungu, maarifa, uwepo wa milele na utakatifu wa Mungu; acha Mungu atuelekeze, tuelewe kina cha na kujitolea kwa uovu ambao unaishi katika kila moyo wa mwanadamu; kutambua kwamba Mungu amewapa watumishi wake jukumu la kuwaonya watu waovu kwa kuangamia kwao, kuzoea uhusiano hai na Yesu Kristo, ambaye alisema kwamba agano jipya ni kupatikana katika damu yake.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Ezekieli
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries