settings icon
share icon

Kitabu cha Esta

Mwandishi: Kitabu cha Esta hakimtaji wazi mtunzi wake. Tamaduni maarufu zaidi ni Mordekai (muhusika mkuu katika kitabu cha Esta), Ezra na Nehemia (ambao huenda walikuwa maarufu na desturi za Kiajemi).

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Esta huenda kiliandikwa kati ya 460 na 350 kk

Kusudi la Kuandika: lengo la Kitabu cha Esta ni kuonyesha utoaji wa Mungu, hasa kwa kuzingatia watu wake wateule, Israeli. Kitabu cha Esta kinarekodi taasisi ya Sikukuu ya Purimu na wajibu wa uchunguzi wa kudumu. Kitabu cha Esta kilisomwa katika Sikukuu ya Purimu ya kuadhimisha ukombozi mkubwa wa taifa la Wayahudi ulioletwa na Mungu kupitia kwa Esta. Bado Wayahudi siku hizi wanasoma kitabu cha Esta wakati wa Purimu.

Mistari muhimu: Esta 2:15 – Hata ilipowadia zamu yake Esta, binti Abihaili, mjomba wake Mordekai, ambaye alimtwaa kuwa binti yake, yeye hakutaka kitu, ila vile vilivyoagizwa na Hegai, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda wanawake. Naye huyu Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona.

Esta 4:14 - Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine, ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?

Esta 6:12 – Kisha Mordekai akarudi kwenye mlango wa mfalme. Bali Hamani akaenda mbio nyumbani kwake, mwenye msiba, na kichwa chake kimefunikwa.

Esta 7: 3 – Ndipo malkia Esta alipojibu, akasema, mfalme, ikiwa nimepata kibali machoni pako, na mfalme akiona vema, nipewe maisha yangu kuwa dua yangu, na watu wangu kuwa haja yangu.

Muhtasari kwa kifupi: Kitabu cha Esta kinaweza kugawanywa katika sehemu kuu tatu. Sura za 1: 1-2: 18 - Esta anachukua nafasi ya Vashiti, 2: 19-7: 10 - Mordekai anamshinda Hamani, 8: 1-10: 3 – Waisraeli wanaepuka jaribio la Hamani la kuwaangamiza. Esta mwenye cheo kikubwa alijihatarisha kwa kifo chake mwenyewe alipotambua hatari iliokuwepo. Yeye alifanya kwa hiari yake chenye kingekuwa shawishi la mauti na akachukua amri ya pili ya ufalme wa mumewe, Hamani. Yeye Alithibitisha busara na dhamana kubwa, ambaye wakati wote alibakia kuwa mnyenyekevu na mwenye heshima kwa mamlaka ya mume wake-mfalme. Mengi kama hadithi ya Yusufu katika Mwanzo 41: 34-37, hadithi zote zinahusisha watawala/wafalme wa kigeni ambao wanadhibiti hatima ya Wayahudi. Nakala zote zinaonyesha ushujaa wa watu wa Israeli ambao wanatoa njia za wokovu wa watu na taifa lao. Mkono wa Mungu ni dhahiri, katika kile kinachoonekana kuwa hali mbaya hakika kiko chini ya udhibiti wa Mwenyezi Mungu ambaye hatimaye ana wema wa watu katika moyo. Katikati mwa hadithi hii kuna tofauti inayoendelea kati ya Wayahudi na Waamalakite, ambayo ilinakiliwa kuanza katika kitabu cha Kutoka. Lengo la Hamani ndilo juhudi ya mwisho iliyorekodiwa katika kipindi cha Agano la kale ya kuwaangamiza kabisa Wayahudi. Mipango yake hatimaye inaishia na mauti yake mwenyewe, na kupandishwa cheo kwa adui yake Mordekai kuchukua nafasi yake, sambamba na ukombozi wa Wayahudi.

Karamu ni mada kuu ya kitabu hiki, kuna karamu kumi ambazo zimerekodiwa, na matukio mengi yalipangwa, msuko wake kuundwa, au kuwekwa wazi katika karamu hizo. Ingawa jina la Mungu halitajwi katika kitabu hiki, ni dhahiri kwamba Wayahudi wa Shushani walimtafuta aingilie kati wakati walifunga na kuomba kwa siku tatu (Esta 4:16). Licha ya ukweli kwamba sheria ya kuruhusu kuharibiwa kwao iliandikwa kwa mujibu wa sheria za Wamedi na Waajemi, kuihakikishia kutobadilika, njia ya maombi yao kujibiwa ilitengenezwa. Esta alihatarisha maisha yake kwa kwenda bila kualikwa kwa mfalme si mara moja bali mara mbili, (Esta 4: 1-2; 8: 3). Yeye hakuridhika na uharibifu wa Hamani, yeye alikuwa na nia ya kuokoa watu wake. Taasisi ya Sikukuu ya Purimu imeandikwa na kuhifadhiwa kwa wote kuona na bado inatambuliwa siku hizi. Wateule wa Mungu, bila kutaja jina lake moja kwa moja, walikubaliwa kukaa kwa utekelezaji kupitia kwa hekima na unyenyekevu wa Esta.

Ishara: Katika Esta, tumepewa mtazamo fiche wa mapambano yanayoendelea ya Shetani dhidi ya makusudio ya Mungu na hasa dhidi ya Masihi wake anayetarajiwa. Kristo kuingia katika jamii ya binadamu ilitabiriwa kwa kuwepo kwa ukoo wa Wayahudi. Tu kama Hamani alipopanga dhidi ya Wayahudi ili kuwaangamiza, hivyo ndivyo Shetani amejiweka mwenyewe dhidi Kristo na watu wa Mungu. Tu kama Hamani alishindwa na kuwekwa juu ya mti aliojengea Mordekai, vivyo hivyo Kristo anatumia silaha ambayo adui yake ametengeneza kumwangamizia na mbegu yake ya kiroho. Kwa msalaba, ambao juu yake Shetani alipanga kumwangamiza Masihi, ulikuwa njia ambayo kupitia kwake Kristo "akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani. Akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo"(Wakolosai 2: 14-15). Tu kama Hamani alitundikwa juu ya mti wenye alijengea Mordekai, ndivyo hivyo shetani alivyoangamizwa kwa msalaba aliouweka kumwangamiza Kristo. Vitendo Tekelezii: Kitabu cha Esta kinaonyesha uamuzi tunaofanya kati ya kuushudia mkono wa Mungu katika hali zetu katika maisha na kuona mambo tu kama ni matukizi kwa bahati mbaya. Mungu ni Mtawala wa haki wa ulimwengu na tunaweza kuwa na uhakika kwamba mipango yake haitabadilishwa kwa matendo ya watu waovu. Ingawa jina lake halitajwi katika kitabu, utunzaji wake kwa watu wake, watu binafsi na taifa, ni dhahiri daima. Kwa mfano, hatuwezi kushindwa kuona Mwenyezi akiweka ushawishi juu ya Mfalme Ahasuero wa kukosa usingizi kwa muda. Kupitia kwa mfano wa Mordekai na Esta, lugha kimya ya upendo Baba yetu anayotumia kuongea moja kwa moja na roho zetu imeonyeshwa katika kitabu hiki. Esta alidhibitisha kuwa na roho ya kimungu na ya kufundishika ambayo pia ilionyesha nguvu kubwa na utiifu wa hiari. Unyenyekevu wa Esta ulikuwa tofauti kabisa na wale walio karibu naye, na hili lilimsababishia kuinuliwa kuwa Malkia. Anatuonyesha kwamba kubaki kuwa mwenye heshima na unyenyekevu, hata katika hali ngumu ila si hali isiyowezekana kwa binadamu, mara nyingi anatuweka katika baraka zizizoonekana kwetu wenyewe na wengine. Tunaweza kufanya vizuri kuiga tabia yake ya ucha Mungu katika hali zote za maisha, lakini hasa katika majaribu. Hakuna hata kidogo malalamiko au tabia mbaya inaonyeshwa katika maandishi. Mara nyingi tunasoma yeye alishinda "neema" ya wale walio karibu naye. Neema kama hiyo ndiyo hatimaye iliokoa watu wake. Tunaweza kupewa neema kama hiyo tunapokubali hata mateso yasiyo ya haki na kufuata mfano wa Esta wa kudumisha mtazamo chanya, ikiwa ni pamoja na unyenyekevu na kujitolea kumtegemea Mungu. Nani anajua lakini kwamba Mungu ndiye anatuweka katika mamlaka kama hiyo, kwa ajili tu ya wakati kama huo?

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Esta
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries