settings icon
share icon

Kitabu cha Danieli

Mwandishi: Kitabu cha Danieli kinamtambua nabii Danieli kama mwandishi wake (Danieli 9: 2, 10: 2). Yesu pia alimtaja Danieli kama mwandishi(Mathayo 24:15).

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Danieli huenda kiliandikwa kati ya 540 na 530 kk

Kusudi la Kuandika: Katika 605 kk, Nebukadreza, mfalme wa Babeli alikuwa ameshinda Yuda na kufukuza wakazi wake wengi hadi Babeli – ikiwa ni pamoja na Danieli. Danieli alitumikia katika mahakama ya kifalme ya Nebukadreza na watawala kadhaa ambao walimfuata Nebukadreza. Kitabu cha Danieli kinanakili vitendo, unabii, na maono ya nabii Danieli.

Mistari muhimu: Danieli 1: 19-20, "Naye mfalme akazungumza nao, na miongoni mwao wote hawakuonekana waliokuwa kama Danieli, na Hanania, na Mishaeli na Azaria; kwa hiyo wakasimama mbele ya mfalme. Na katika kila jambo la hekima na ufahamu alilowauliza mfalme, akawaona kuwa walifaa mara kumi zaidi ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake. "

Danieli 2:31, "Wewe, Ee mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha."

Danieli 3: 17-18, "Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha. "

Danieli 4: 34-35, "Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukakadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi, na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, unafanya nini wewe?"

Danieli 9: 25-27, "Basi ujua na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu. Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakataliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kusudiwa. Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu."

Muhtasari kwa kifupi: Danieli inaweza kugawanywa katika sehemu tatu. Sura ya 1 inaeleza kushindwa kwa Yerusalemu na Wababiloni. Pamoja na wengine wengi, Danieli na marafiki zake watatu walifungwa Babeli na kwa sababu ya ujasiri wao na baraka za wazi za Mungu juu yao, walipandishwa cheo katika huduma ya mfalme (Danieli 1: 17-20).

Sura 2-7 zinarekodi Nebukadreza kuwa na ndoto ambayo tu Danieli ndiye anaweza kuitafsiri vizuri. Ndoto ya Nebukadneza ya sanamu kubwa iliwakilisha falme ambazo zingetokea katika siku zijazo. Nebukadreza alitengeneza sanamu kubwa yake mwenyewe na kulazimisha kila mtu aiabudu. Shadraka, Meshaki, na Abednego walikataa na waliokolewa kimiujiza na Mungu licha ya kutupwa katika tanuru ya moto. Nebukadreza anahukumiwa na Mungu kwa kiburi chake, lakini baadaye anarejeshwa punde tu alipotambua na kukiri mamlaka ya Mungu.

Danieli sura ya 5 inarekodi kuhusu Belshaza mwana wa Nebukadneza akifuja vitu vilivyochukuliwa kutoka kwa hekalu la Yerusalemu na kupokea ujumbe kutoka kwa Mungu, ulioandikwa katika ukuta. Tu Danieli ndiye angeweza kutafsiri maandishi, ujumbe wa hukumu ijayo kutoka kwa Mungu. Danieli anatupwa katika tundu la simba kwa kukataa kuomba kwa Kaisari, lakini aliokolewa kimiujiza. Mungu alimpa Danieli maono ya wanyama wanne. Hawa wanyama wanne wawakilisha falme za Babeli, Umedi na Uajemi, Ugiriki, na Roma.

Sura 8-12 zina maono yanayoshirikisha kondoo, mbuzi, na pembe kadhaa - pia zikirejelea falme zijazo na watawala wake. Danieli sura ya 9 inarekodi unabii wa Danieli wa "majuma sabini". Mungu alimpa Danieli ratiba sahihi ya wakati Masihi atakuja na kuuawa. Unabii huo pia unataja mtawala atakayekuja baadaye ambaye atafanya agano la miaka saba na Israeli na kulivunja baada ya miaka mitatu na nusu, ikifuatiwa muda mfupi baadaye na hukumu kuu na kuangamizwa kwa vitu vyote. Danieli anatembelewa na kutiwa nguvu na malaika baada ya maono haya makubwa, na malaika anamwelezea Danieli kuhusu maono kwa kina kirefu.

Ishara: Tunaona katika hadithi za tanuru ya moto na Danieli katika tundu la simba ishara ya wokovu unaotolewa na Kristo. Wale wanaume watatu wanatangaza kwamba Mungu ni Mungu wa kuokoa ambaye anaweza kutoa njia ya kuepuka (Danieli 3:17). Kwa njia hiyo hiyo, kwa kumtuma Yesu kufa kwa ajili ya dhambi zetu, Mungu ametoa njia ya kuepuka kutoka kwa moto wa Jehanamu (1 Petro 3:18). Katika suala la Danieli, Mungu alimtuma malaika kufunga vinywa vya simba na kuokoa Danieli kutoka kwa mauti. Yesu Kristo ni mwokozi wetu kutokana na hatari ya dhambi ambayo inatishia kutuangamiza.

Maono ya Danieli ya nyakati za mwisho yanaonyesha Masihi wa Israeli na ambaye kupitia kwake wengi watafanywa safi na takatifu (Danieli 12:10). Yeye ni haki yetu (1 Petro 5:21) na ambaye dhambi zetu, ingawa ni nyekundu kama damu, zitafutiliwa mbali na tutakuwa weupe kama theluji (Isaya 1:18).

Vitendo Tekelezi: Kama Shadraka, Meshaki na Abednego, tunapaswa daima kusimama kwa kile tunajua ni kweli. Mungu ni mkuu kuliko adhabu yoyote ambayo inaweza kuja juu yetu. Kama Mungu ataamua kutuokoa au la, Yeye daima anastahili tumwamini. Mungu anajua kilicho bora, na Yeye anaheshimu wale wanaomtumainia na kumtii.

Mungu ana mpango, na mpango wake ni wa kina kirefu. Mungu anajua na ako katika udhibiti wa baadaye. Kila kitu ambacho Mungu alitabiri kimekuwa kweli sawa kabisa na jinsi alivyotabiri. Kwa hivyo, tunapaswa kuamini na kujua kwamba mambo ambayo ametabiri kwa siku zijazo siku moja yatatokea kama vile Mungu ametangaza.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Danieli
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries