settings icon
share icon

Kitabu cha 2 Timotheo

Mwandishi: 2 Timotheo 1: 1 kinamtambua mwandishi wa kitabu cha 2 Timotheo kama mtume Paulo.

Tarehe ya kuandikwa: kitabu cha 2 Timotheo huenda kiliandikwa mnamo 67 BK, muda mfupi kabla ya Mtume Paulo kuuawa.

Kusudi la Kuandika: Kwa kufungwa tena katika Roma, Mtume Paulo alihisi upweke na aliyeachwa. Paulo alitambua kwamba maisha yake hapa duniani yalikuwa na uwezekano wa kufika mwisho hivi karibuni. kitabu cha 2 Timotheo kimsingi ni "maneno ya mwisho" ya Paulo. Paulo alitazamia zaidi ya hali zake mwenyewe ili kuonyesha kujali kwake kwa makanisa na hasa kwa Timotheo. Paulo alitaka kutumia maneno yake ya mwisho kumtia moyo Timotheo, na waumini wengine wote, kuvumilia katika imani (2 Timotheo 3:14) na kutangaza Injili ya Yesu Kristo (2 Timotheo 4: 2).

Mistari muhimu: 2 Timotheo 1: 7, "Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi"

2 Timotheo 3: 16-17, "Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema."

2 Timotheo 4: 2, "Lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. "

2 Timotheo 4: 7-8, "Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda. Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake. "

Muhtasari kwa kifupi: Paulo anamtia moyo Timotheo kubakia kuonyesha hisia kali kwa ajili ya Kristo na kubaki imara katika mafundisho ya kweli (2 Timotheo 1: 1-2, 13-14). Paulo anamkumbusha Timotheo kuepuka na imani potofu na matendo maovu na kujitenga na chochote kiovu (2 Timotheo 2: 14-26). Katika nyakati za mwisho kutakuwa na mateso makali na uasi kutoka kwa imani ya Kikristo (2 Timotheo 3: 1-17). Paulo anamaliza kwa ombi kali kwa waumini kusimama imara katika imani na kumaliza mbio kwa nguvu (2 Timotheo 4: 1-8).

Mashirikisho: Hivyo alivyojali Paulo kumwonya Timotheo na wale aliokuwa mchungaji wao kuhusu hatari za walimu wa uongo ambao aliomba kwa Mungu hadithi ya waganga wa Misri ambao walimpinga Musa (Kutoka 7:11, 22; 8: 7, 18, 19; 9:11 ). Ingawa majina yao hayakutajwa katika Agano la Kale, utamaduni ni kwamba watu hawa walichochea kujengwa kwa ndama ya dhahabu na waliuawa na wengine waabudu sanamu (Kutoka 32). Paulo anatabiri maangamizi sawa kwa wale ambao wanapinga ukweli wa Kristo, upumbavu wao hatimaye kufanywa "wazi kwa kila mtu" (2 Timotheo 3: 9).

Vitendo Tekelezi: Ni rahisi kupata umeteleza katika maisha ya Kikristo. Tunapaswa kuweka macho yetu kwa zawadi – ambayo inatuzwa mbinguni na Yesu Kristo (2 Timotheo 4: 8). Lazima tujitahidi kuepuka mafundisho ya uongo na matendo maovu. Hili linaweza tu kutimizwa kwa kuwekwa kwa msingi katika ufahamu wetu wa Neno la Mungu na msimamo wetu imara katika kukataa kwetu kukubali chochote kisicho cha kibiblia.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha 2 Timotheo
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries