settings icon
share icon

Kitabu cha 2 Petro

Mwandishi: 2 Petro 1: 1 hasa kinataja kwamba Mtume Petro alikuwa mwandishi wa 2 Petro. Uandishi wa wa Petro wa kitabu cha 2 Petro umekuwa ukitiwa changamoto zaidi kuliko ile ya kitabu kingine chochote katika Agano Jipya. Hata hivyo, wazee wa kwanza wa kanisa hawakupata sababu nzuri ya kukataa. Hatuoni sababu nzuri ya kukataa uandishi wa Petro wa kitabu cha 2 Petro.

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha 2 Petro kiliandikwa mwishoni mwa maisha ya Petro. Kwa kuwa Petro aliuawa katika Roma wakati wa utawala wa Nero, kifo chake lazima kilitokea kabla ya 68 BK. Yeye huenda aliandika 2 Petro kati ya 65 na 68 BK.

Kusudi la Kuandika: Petro alijulishwa kwamba walimu wa uongo walikuwa wameanza kujipenyeza makanisani. Aliwataka Wakristo kukua na kuwa na nguvu katika imani yao ili waweze kutambua na kupambana na uasi unaoenea. Yeye alisisitiza kwa nguvu uhalisi wa Neno la Mungu na uhakika wa kurudi kwa Bwana Yesu.

Mistari muhimu: 2 Petro 1: 3-4, "Kwa kuwa uwezo wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua Yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. "

2 Petro 3: 9: "Bwana hakawii kutimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba. "

2 Petro 3:18: Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele. "

Neno muhimu ni maarifa; pamoja na maneno yanayopatana nalo, yanayoonekana angalau mara 13 katika kitabu cha 2 Petro.

Muhtasari kwa kifupi: Akijua kwamba wakati wake ni mfupi (2 Petro 1: 13-15), na makanisa haya yalikabiliwa na hatari ya ghafla (2 Petro 2: 1-3), alitoa wito kwa wasomaji waziimarishe kumbukumbu zao (2 Petro 1:13 ) na kuchochea mawazo yao (2 Petro 3: 1-2) ili kwamba wangeweza kukumbuka mafundisho yake (2 Petro 1:15). Yeye alitoa changamoto kwa waumini wawe wakomavu zaidi katika imani yao kwa kuiongezea wema/maadili maalum ya kikristo, na hivyo kuwa wenye nguvu/wanaofaa na zalishi katika ufahamu wao wa Yesu Kristo (2 Petro 1: 5-9). Waandishi wa Agano la Kale na Agano Jipya waliwekwa mbele kama mamlaka yao kwa imani yao (2 Petro 1: 12-21, 3: 2, 3: 15-16). Petro alitamani wawe na nguvu katika imani yao kuhimili walimu wa uongo ambao walikuwa wamejipenyesha na kuathiri makanisa vibaya. Katika kuwashutumu, alifafanua mwenendo wao, kulaaniwa kwao, na sifa zao (2 Petro sura ya 2), na pia kwamba walidhihaki kuja kwa Bwana mara ya pili (2 Petro 3: 3-7). Kwa Wakristo, Petro alifundisha kwamba kuja kwa mara ya pili ni motisha kwa kuishi maisha matakatifu (2 Petro 3:14). Baada ya onyo la mwisho, Petro tena aliwatia moyo kukua katika neema na katika kumjua Bwana wao na Mwokozi Yesu Kristo. Alihitimisha na neno la sifa kwa Bwana na Mwokozi wake(2 Petro 3:18).

Mashirikisho: Katika kuwashutumu kwake kwa manabii wa uongo, Petro anarudia dhamira maarufu katika Agano la kale ambayo ingeweza kufahamika kwa na wasomaji wake. Wengi wa Wakristo wa awali walikuwa Wayahudi waliokuwa wamemeokoka ambao walikuwa wamefunzwa vizuri katika sheria na manabii. Wakati Petro alirejelea kwa "neno la manabii" la Agano la Kale katika 2 Petro 1: 19-21, yeye kwa wakati mmoja aliwashutumu manabii wa uongo na akahakikisha kwamba manabii wa kweli walikuwa wakiongozwa na Roho Mtakatifu ambaye alizungumza kupitia kwao (2 Samweli 23 : 2). Yeremia alikuwa sawa kinguvu katika mashutu yake ya manabii wa uongo, akiuliza "Ni kwa muda gani haya yataendelea katika mioyo ya manabii hawa wa uongo, watabirio udanganyifu wa akili zao wenyewe?" (Yeremia 23:26). Dhahiri, walimu hao hao wa uongo ambao walitaabisha watu wa Mungu katika Agano la Kale na Jipya bado wako na sisi, na kuifanya barua ya pili ya Petro kuwa muhimu siku hizi kama ilivyokuwa miaka 2000 iliyopita.

Vitendo Tekelezi: Hakika, kama Wakristo katika karne ya 21, tuko karibu sana na kurudi kwa Bwana wetu kuliko Wakristo wa karne ya kwanza ambao waraka huu uliandikwa kwao. Kupitia kwa televisheni na njia zingine za vyombo vya habari, Wakristo wakomavu wanatambua kuwa walaghai wengi wamejikusanya kama viongozi wa kikristo wa kweli, na kwamba Wakristo wachanga "wamechukuliwa" na utapeli wao wa kitaalamu na tafsiri zao za uongo za maandiko. Yawapasa wakristo wote waliookoka kuwekwa katika msingi wa Neno kwamba tuweze kutambua ukweli kutoka katika makosa.

Maagizo sawa kwa ukuaji katika imani ambayo Petro alitoa (2 Petro 1: 5-11), wakati yanatekelezwa kwa maisha yetu, yatatuhakikishia pia tuzo kubwa "katika Utawala wa milele wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo" (2 Petro 1 : 10-11). Msingi kwa imani yetu ni na daima utakuwa Neno lile lile la Mungu ambalo Petro alihubiri.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha 2 Petro
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries