settings icon
share icon

Kitabu cha 1 Yohana

Mwandishi: Yohana ya 1, 2 na 3 zimeshirikishwa tangu mwazo na mtume Yohana, ambaye pia aliandika Injili ya Yohana. Maudhui, mtindo, na msamiati yanaonekana kuipa kibali hitimisho kwamba nyaraka hizi tatu ziliandikiwa wasomaji sawa kama wale wa injili ya Yohana.

Tarehe ya kuandikwa: kitabu cha 1 Yohana huenda kiliandikwa kati ya 85-95 BK.

Kusudi la Kuandika: Kitabu cha 1 Yohana kinaonekana kuwa muhtasari ambao unachukulia maarifa ya wasomaji kuhusu injili kama ilivyoandikwa na Yohana na unatoa hakika kwa imani yao katika Kristo. Waraka wa kwanza unaonyesha kwamba wasomaji walikuwa wanakabiliwa na makosa ya Uaginostiki, ambayo yalikuwa tatizo kubwa zaidi katika karne ya pili. Kama falsafa ya dini ilishikilia kwamba maudhui ni maovu na roho ni nzuri. Suluhisho kwa mvutano kati ya hizi mbili ilikuwa maarifa, au uaginosi, ambayo kwayo mwanadamu alitoka kwa kwa mambo ya kiulimwengu hadi kwa kiroho. Katika ujumbe wa injili, hii ilisababisha nadharia mbili za uongo kuhusu utu wa Kristo, ‘Docetism’-kuhusu Yesu mwanadamu kama pepot-na ‘Cerinthianism’ kumfanya Yesu watu wawili, kwa wakati mwingine binadamu na wakati mwingine Mungu. lengo kuu la 1 Yohana ni kuweka mipaka juu ya maudhui ya imani na kuwapa waumini uhakika wa wokovu wao.

Mistari muhimu: 1 Yohana 1: 9, "Tukiziungama dhambi zetu, Yesu ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote."

1 Yohana 3: 6, "Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.".

1 Yohana 4: 4, "Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia."

1 Yohana 5:13, "Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa Mungu."

Neno muhimu ni maarifa; na maneno yanayolihusiana, yanayoonekana angalau mara 13 katika kitabu cha 1 Yohana.

Muhtasari kwa kifupi: Walimu wa uongo wa kiroho walikuwa tatizo kubwa katika kanisa la kwanza. Kwa sababu hakukuwa na Agano Jipya kamilifu ambalo waumini wangerejelea, makanisa mengi yalikuwa mawindo ya waliojifanya ambao walifundisha mawazo yao wenyewe na kujiweka wenyewe kama viongozi. Yohana aliandika barua hii kwa kuweka rekodi sawa moja kwa moja katika baadhi ya masuala muhimu, hasa kuhusu utambulisho wa Yesu Kristo.

Kwa sababu barua ya Yohana ilikuwa kuhusu misingi ya imani katika Kristo, ilisaidia wasomaji wake kutafakari uaminifu wa imani yao. Iliwasaidia kujibu swali, Je, sisi ni waumini wa kweli? Yohana aliwaambia kwamba wangeweza kutambua kwa kuangalia matendo yao. Ikiwa walipendana, hili ni ushahidi wa uwepo wa Mungu katika maisha yao. Lakini kama waligombanagombana na kupigana wakati wote au walikuwa wenye ubinafsi na hawakuwa wanaangaliana wao kwa wenyewe, walikuwa wanajisaliti kwamba wao, kwa kweli, hawakumjua Mungu.

Hilo halikumaanisha kwamba walipaswa kuwa kamilifu. Kwa kweli, Yohana pia alitambua kuwa kuamini kulishirikisha kukiri dhambi zetu na kutafuta msamaha wa Mungu. Kutegemea Mungu kutakasa kutokana na hatia, pamoja na kukiri makosa yetu dhidi ya wengine na kufanya marekebisho, ilikuwa ni sehemu nyingine muhimu ya kupata kumjua Mungu.

Mashirikisho: Mojawapo ya kifungu ambacho kinanukuliwa mara nyingi kuhusu dhambi hupatikana katika 1 Yohana 2:16. Katika kifungu hiki, Yohana anaeleza mambo matatu ya dhambi ambayo yanakumbusha majaribu ya kwanza na makuu zaidi yanayovunjavunja ulimwengu katika maandiko yote . Dhambi za kwanza- uasi wa Hawa- ulikuwa matokeo yake unaozalisha kwa majaribu yale yale matatu kama tunavyopata katika Mwanzo 3: 6: tamaa ya mwili ("nzuri kwa chakula"); tamaa ya macho ("kupendeza kwa jicho"); na kiburi cha maisha ("kuhitajika kwa kupata hekima").

Vitendo Tekelezi: kitabu cha 1 Yohana ni kitabu cha upendo na furaha. Kinaelezea ushirika tulio nao na watu wengine na Yesu Kristo. Kinatofautisha kati ya furaha, ambayo ni ya muda mfupi unaopita na furaha ya kweli, ambayo 1 Yohana inatuambia jinsi ya kuifikia. Ikiwa tutachukua maneno yaliyoandikwa na Yohana na kuyatekeleza katika maisha yetu ya kila siku, upendo wa kweli, kujitolea, ushirika, na furaha tunayotamani itakuwa yetu.

Mtume Yohana alimjua Kristo vizuri. Anatueleza kwamba tunaweza zote kuwa na uhusiano huo wa karibu na wa ndani na Yesu Kristo. Tuna mashahidi wa watu ambao walikuwa na mgusano wa moja kwa moja na binafsi pamoja naye. Waandishi wa Injili wanawasilisha ushahidi wao ulio na msingi wake katika hali halisi ya kihistoria. Sasa, hilo linatekelezwaje kwa maisha yetu? Kinatueleza kuwa Yesu alikuja hapa kama Mwana wa Mungu kutengeneza uhusiano na sisi ulio na msingi kwa neema yake, huruma, upendo, na kukubalika. Hivyo mara nyingi watu wanadhani Yesu yu katika baadhi ya sehemu za mbali na kwa kweli hajali mapambano yetu ya kila siku, masuala, na maslahi. Lakini Yohana anatueleza kuwa Yesu yu nasi hapa katika maeneo ya kawaida, sehemu za kilimwengu za maisha yetu na katika yaliyo tatanifu, pia sehemu zinazoumiza mwili kwa kusokotoa. Yohana anakiri kama shahidi aliyejionea mwenyewe kwamba Mungu akawa mwili na kuishi miongoni mwa watu. Hiyo ina maana Kristo alikuja hapa kuishi na sisi na Yeye bado anaishi na sisi. Kama alivyotembea duniani pamoja na Yohana, hivyo ndivho anavyotembea siku baada ya siku na sisi. Tunahitaji kutekeleza ukweli huu katika maisha yetu na kuishi kana kwamba Yesu anasimama hakika karibu na sisi kila sekunde ya siku. Ikiwa tutatekeleza ukweli huu, Kristo ataongezea utakatifu kwa maisha yetu, na kutufanya zaidi na zaidi kama yeye.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha 1 Yohana
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries