settings icon
share icon

Kitabu cha 1 Wathesalonike

Mwandishi: 1 Wathesalonike 1: 1 inaonyesha kuwa kitabu cha 1 Wathesalonike kiliandikwa na Mtume Paulo, pengine pamoja na Sila na Timotheo.

Tarehe ya kuandikwa: kitabu cha 1 Wathesalonike kiliandikwa katika takriban 50 BK.

Kusudi la Kuandika: Katika kanisa la Thesalonike kulikuwa na baadhi ya kutoelewana juu ya kurudi kwa Kristo. Paulo alitaka kutoa utata huo katika barua yake. Pia anauandika kama mafundisho ya kuishi maisha matakatifu.

Mistari muhimu: 1 Wathesalonike 3: 5, "Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalimtuma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida. "

1 Wathesalonike 3: 7, "Kwa sababu hiyo, ndugu, tulifarijiwa kwa habari zenu, katika msiba na dhiki yetu yote, kwa imani yenu."

1 Wathesalonike 4: 14-17. "Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu na parapanda ya Mungu , nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. "

1 Wathesalonike 5:16-18, "Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambbo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. "

Muhtasari kwa kifupi: Sura tatu za kwanza ni kuhusu hamu ya Paulo kutembelea kanisa la Thesalonike lakini hakuweza kuenda kwa sababu Shetani aliwazuhia(1 Wathesalonike 2:18), na jinsi Paulo alivyowajali na alitiwa moyo kusikia jinsi walivyoendelea. Paulo kisha anawaombea (1 Wathesalonike 3: 11-13). Katika sura ya 4, Paulo anawafundisha waumini wa Thesalonike jinsi ya kuishi katika Kristo Yesu, maisha matakatifu (1 Wathesalonike 4: 1-12). Paulo anaendelea kuwafundisha kuhusu kuelewa vibaya waliokuwa nao. Anawaambia kuwa watu waliokufa katika Kristo Yesu pia wataenda mbinguni wakati atarejea (1 Wathesalonike 4: 13-18, 5: 1-11). Kitabu kinaishia na maelekezo ya mwisho ya kuishi maisha ya Kikristo.

Mashirikisho: Paulo anawakumbusha Wathesalonike kwamba mateso waliokuwa wakipokea kutoka kwa "wananchi wenzao"(mst. 2:15), Wayahudi waliokataa Masihi wao, ni sawa na mateso ambayo manabii wa Agano la Kale walipata (Yeremia 2:30, Mathayo 23 : 31). Yesu alionya kwamba manabii wa kweli wa Mungu wangepingwa daima na wasio wenye haki (Luka 11:49). Katika Wakolosai, Paulo anawakumbusha kuhusu ukweli huo.

Vitendo Tekelezi: Kitabu hiki kinaweza kutumika kwa hali nyingi za maisha. Kinatupa ujasiri kama Wakristo kwamba iwe tumekufa au tuko hai wakati Kristo atarudi tutakuwa pamoja naye (1 Wathesalonike 4: 13-18). Kinatuhakikishia sisi kama Wakristo kwamba hatutapokea ghadhabu ya Mungu (1 Wathesalonike 5: 8-9). Kinatufundisha jinsi ya kutembea maisha ya kikristo kila siku (1 Wathesalonike 4-5).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha 1 Wathesalonike
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries