settings icon
share icon

Kitabu cha 1 Timotheo

Mwandishi: Kitabu cha 1 Timotheo kiliandikwa na Mtume Paulo (1 Timotheo 1: 1).

Tarehe ya kuandikwa: kitabu cha 1 Timotheo kiliandikwa 62-66 BK.

Kusudi la Kuandika: Paulo aliandikia Timotheo kumhimiza katika wajibu wake kwa kuangalia kazi za kanisa la Efeso na pengine makanisa mengine katika jimbo la Asia (1 Timotheo 1: 3). Hii barua inaweka msingi wa utaratibu wa kuamua wazee (1 Timotheo 3: 1-7), na hutoa mwongozo kwa utaratibu wa kuwaweka watu katika maofisi ya kanisa (1 Timotheo 3: 8-13). Kimsingi, 1 Timotheo ni mwongozo wa uongozi kwa mpangilio wa kanisa na usimamiaji.

Mistari muhimu: 1 Timotheo 2: 5, "Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, mwanadamu Kristo Yesu."

1 Timotheo 2:12, "Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu."

1 Timotheo 3: 1-3, "Ni neno la kuaminiwa: mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mtu wa kupenda fedha. "

1 Timotheo 4: 9-10, "Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa; kwa maana twajitaabishana na kujitahidi kwa kusudi hili, kwa sababu tunamtumaini Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa waaminio. "

1 Timotheo 6:12, "Piga vita vile vizuri vya imani. Shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi."

Muhtasari kwa kifupi: Hii ni barua ya kwanza Paulo aliandikia Timotheo, mchungaji kijana ambaye alikuwa msaidizi wa Paulo katika kazi yake. Timotheo alikuwa Mgiriki. Mama yake alikuwa Myahudi na baba yake alikuwa Mgiriki. Paulo alikuwa zaidi ya mshauri na kiongozi kwa Timotheo, alikuwa kama baba kwake na Timotheo alikuwa kama mwana kwa Paulo (1 Timotheo 1: 2). Paulo anaanza barua kwa kumhimiza Timotheo kuwa mwangalifu kwa walimu wa uongo na mafundisho ya uongo. Hata hivyo, sehemu kubwa ya barua inashughulikia mwenendo wa kichungaji. Paulo anamwelekeza Timotheo katika ibada (sura ya 2) na kukuza viongozi komavu kwa kanisa (sura ya 3). Sehemu kubwa ya barua inashughulika na mwenendo wa kichungaji, onyo kuhusu walimu wa uongo, na jukumu la kanisa kwa washiriki watenda dhambi, wajane, wazee na watumwa. Kwa barua nzima, Paulo anamhimiza Timotheo kusimama imara, avumilie, na kubakia kuwa mwaminifu kwa wito wake.

Mashirikisho: Kipatanisho cha kuvutia kwa Agano la Kale katika kitabu cha 1 Timotheo ni dondoo la Paulo la msingi kwa kuzingatia wazee wa kanisa kuwa wanastahili "heshima maradufu," na kustahili heshima wanaposhutumiwa kufanya makosa (1 Timotheo 5 : 17-19). Kumbukumbu 24:15, 25: 4 na Mambo ya Walawi 19:13 vyote vinazungumzia umuhimu wa kumlipa mfanyakazi anachostahili kwa wakati ufaao. Sehemu ya Sheria za Musa zilidai kwamba mashahidi wawili au watatu walikuwa muhimu kuleta mashtaka dhidi ya mtu (Kumbukumbu 19:15). Wakristo Wayahudi katika makanisa ambayo Timotheo alikuwa mchungaji pengine walikuwa na ufahamu mzuri wa mapatanisho haya ya Agano la Kale.

Vitendo Tekelezi: Yesu Kristo anaonyeshwa na Paulo kama mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu (1 Timotheo 2: 5), Mwokozi kwa wale wote ambao wanamwamini. Yeye ni Bwana wa kanisa, na Timotheo anamtumikia kwa kuwa mchungaji wa kanisa lake. Hivyo, tunapata utekelezi wa barua ya kwanza ya Paulo kwa "mwana wake katika imani." Paulo anamwelekeza Timotheo kwa masuala ya mafundisho ya kanisa, Uongozi wa Kanisa, na usimamiaji wa Kanisa. Tunaweza kutumia maelekezo hayo katika uongozi wa madhehebu yetu siku hizi. Kadhalika, kazi na huduma ya mchungaji, sifa za mzee wa kanisa, na sifa za shemasi ni muhimu sana na ya kufaa siku hizi kama yalivyokuwa katika siku za Timotheo. Barua ya Paulo ya kwanza kwa Timotheo inaafikia kitabu cha maelekezo ya kuongoza, usimamiaji, na kuchunga kanisa la mtaa. Maelekezo katika barua hii yanatumika kwa kiongozi yeyote au anayetazamia kuwa kiongozi wa kanisa la Kristo na ni muhimu siku hizi kama yalivyokuwa katika siku za Paulo. Kwa wale wasioitwa katika majukumu ya uongozi katika kanisa lao, kitabu bado ni tekelezi kwao. Kila mfuasi lazima ashikilie imani na kuepuka mafundisho ya uongo. Kila mfuasi lazima asimame imara na kuvumilia.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha 1 Timotheo
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries