settings icon
share icon

Kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati

Mwandishi: Kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati hakimtaji wazi mtunzi wake. Utamaduni ni kwamba Mambo ya Nyakati ya 1 na 2 ziliandikwa na Ezra.

Tarehe ya Kuandikwa: Kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati kina uwezekano kiliandikwa kati ya 450 na 425 BC

Kusudi la Kuandika: Vitabu vya Mambo ya Nyakati ya 1 & 2 vinashughulikia zaidi ujumbe sawa na Samweli 1 & 2 pia Wafalme 1 & 2. Mambo ya Nyakati ya 1 & 2 ulenga zaidi suala la kikuhani wa kipindi cha muda. Kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati kiliandikwa baada ya uhamisho kuwasaidia wale waliorudi Israeli ili waelewa jinsi ya kumwabudu Mungu. Historia ililenga ufalme wa kusini, makabila ya Yuda, Benjamini na Lawi. Makabila haya yalijifanya kuwa yaaminifu zaidi kwa Mungu.

Mistari muhimu: 1 Mambo ya Nyakati 11: 1-2, "Ndipo Israeli wote wakamkusanyikia Daudi huko Hebroni, wakisema, Tazama, sisi tu mfupa wako na nyama yako. Katika zamani za kale, hata hapo Sauli alipokuwa mfalme,wewe ndiwe uliyewatoa na kuwaingiza Israeli. Naye Bwana, Mungu wako, akakuambia, ndiwe, utakayewalisha watu wangu Israeli, ndiwe utakayekuwa mkuu juu ya watu wangu Israeli. "

1 Mambo ya Nyakati 21:13, "Naye Daudi akamwambia Gadi, nimeingia katika mashaka sana;basi sasa na nianguke katika mkono wa Bwana, kwa kuwa rehema zake ni nyingi sana; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu. "

1 Mambo ya Nyakati 29:11, "Ee Bwana, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu,na kushinda, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee Bwana, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote. "

Muhtasari kwa kifupi: Sura 9 za kwanza za 1 Mambo ya Nyakati zimeweka wakfu kwa orodha na nasaba. Orodha na nasaba zaidi zimetambaa katika sura zilizobaki za 1 Mambo ya Nyakati. Katikati, Kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati kinanakili jinsi Daudi alivyo fanywa mfalme na matendo yake baada ya hapo. kitabu kinamalizia kwa Solomoni mwana wa Daudi kuwa mfalme wa Israeli. Kwa kifupi, kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati ni kama ifuatavyo: sura ya 1: 1-9: 23 - Ukoo Teule, Sura 9: 24-12: 40 – kuinuliwa kwa Daudi; Sura ya 13: 1-20: 30 utawala wa David .

Ishara: Katika wimbo wa Daudi wa shukrani kwa Mungu katika 1 Nyakati 16:33, yeye anarejelea wakati Mungu atakuja kuhukumu dunia.Hii inaashiria Mathayo 25, ambayo Yesu anaeleza wakati atakuja kuhukumu dunia. Kupitia kwa mifano ya wasichana kumi mabikra na vipaji, anaonya kwamba wale ambao watapatikana bila damu ya Kristo imefunika dhambi zao watatupwa katika giza nje. Yeye anatia watu wake moyo ili wawe tayari kwa sababu wakati atakuja, atawatenga kondoo na mbuzi katika hukumu.

Sehemu ya Agano na Daudi ambalo Mungu anarudia katika sura ya 17 inarejelea Masihi ajaye baadaye ambaye atakuwa mjukuu wa Daudi. Misitari 13-14 inaelezea Mwana ambaye ataimarishwa katika nyumba ya Mungu na ambaye kiti chake cha enzi kitakuwa imara milele. Hii inaweza tu kurejelea Yesu Kristo.

Vitendo Tekelezi: Vizazi kama vile katika 1 Mambo ya Nyakati vinaweza kuonekana kavu kwetu, lakini vinatukumbusha kwamba Mungu anajua kila mmoja wa mtoto wake binafsi, hata chini ya idadi ya nywele juu ya vichwa vyetu (Mathayo 10:30). Tunaweza kuchukua faraja katika ukweli kwamba sisi ni nani na kile tufanyayo kimeandikwa milele katika mawazo ya Mungu. Kama sisi ni wa Kristo, majina yetu yameandikwa milele katika kitabu cha Mwanakondoo cha uzima (Ufunuo 13: 8).

Mungu ni mwaminifu kwa watu wake na anahifadhi ahadi zake. Katika kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati, tunaona timizo la ahadi ya Mungu kwa Daudi wakati yeye anafanywa mfalme juu ya Israeli yote (1 Mambo ya Nyakati 11: 1-3). Tunaweza kuwa na hakika kwamba ahadi zake kwetu zitatimizwa pia. Ameahidi baraka kwa wale ambao watamfuata, na ambao watatii Neno lake.

Kutii kunaleta baraka, uasi huleta hukumu. Kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati, vile vile Samweli ya 1 na 2 na Wafalme ya 1 na 2, ni rekodi ya mitindo ya dhambi, toba, msamaha, na marejesho ya taifa la Israeli. Kwa njia hiyo hiyo, Mungu anatuvumilia na anatusamea dhambi zetu wakati tunakuja kwake kwa toba ya kweli (1 Yohana 1: 9). Tunaweza kuchukua faraja katika ukweli kwamba Yeye anasikia maombi yetu ya huzuni, husamehe dhambi zetu, anatutayarisha kwa kufanya ushirika naye, na anatuweka katika njia ya furaha.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries