settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nini kipawa cha kiroho cha uponyaji?

Jibu


Kipawa cha kiroho cha uponyaji ni udhihirisho usio wa kawaida wa Roho wa Mungu ambao kimuujiza huleta uponyaji na uokoaji kutokana na magonjwa na/au udhaifu. Ni nguvu ya Mungu inayoharibu kazi ya dhambi na/au shetani katika mwili wa binadamu, kama vile uponyaji ambao Yesu na wanafunzi walifanya (Mathayo 4:24, 15:30; Matendo 5:15-16; 28:8-9). Kipawa cha uponyaji kilichotolewa kwa kanisa kinatajwa hasa katika 1 Wakorintho 12, ambapo vipawa vya kiroho vimeorodheshwa.

Vipawa vya kiroho ni nguvu, ujuzi, uwezo, au hekima iliyotolewa na Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu kwa Wakristo. Paulo anaiambia kanisa kwamba madhumuni ya vipawa vya kiroho ni kuadilisha waumini wengine na, hatimaye, kumtukuza Mungu. Mungu hutoa vipawa hivi kwa ajili ya matumizi Yake, lakini katika kanisa la Korintho, vilikuwa dhahiri aina ya ishara ya hali au kutumiwa kuonyesha ukuu. Kwa kupendeza, 1 Wakorintho 12:9 inataja "vipawa" vya uponyaji kwa wingi, ambayo inaweza kuonyesha kwamba kuna vipawa tofauti vya uponyaji. Vipawa vya uponyaji vinaweza kumaanisha ujuzi au uwezo mkubwa sana. Hii inaweza kuwa kutoka kwa nguvu ya kufanya uponyaji wa muujiza au ya ajabu, kama kufanya viwete kutembea, au matumizi au ufahamu wa dawa. Hata inaweza kuwa na uwezo wa kuhisi na kuonyesha upendo kwa wengine hadi kiwango cha kuponya jeraha la kihisia.

Kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu matumizi ya kipawa cha kiroho cha uponyaji kati ya Wakristo. Wengine wanaamini kipawa cha uponyaji na baadhi ya ishara ya vipawa vingine havitumiki tena leo, wakati wengine wanaamini vipawa vya kimuujiza bado vinatumika leo. Bila shaka, nguvu ya kuponya haikuwa kamwe katika mtu mwenye kujitunuku mwenyewe. Nguvu ya kuponya ni kutoka kwa Mungu na Mungu pekee. Ingawa Mungu bado anaponya leo, tunaamini uponyaji Wake kwa njia ya kipawa cha uponyaji kilichokuwa hasa kwa mitume wa kanisa la karne ya kwanza kuthibitisha kwamba ujumbe wao ulikuwa kutoka kwa Mungu (Matendo 2:22; 14:3).

Mungu bado anafanya miujiza. Mungu bado anawaponya watu. Hakuna kitu kinachozuia Mungu kumponya mtu mmoja kupitia huduma ya mtu mwingine. Hata hivyo, kipawa cha ajabu cha uponyaji, kama kipawa cha kiroho, hakionekani kufanya kazi leo. Mungu kwa hakika anaweza kuingilia kati kwa namna yoyote Yeye anayoona inafaa, iwe katika mtindo wa "kawaida" au kupitia muujiza. Wokovu wetu wenyewe ni muujiza. Tulikufa katika dhambi, lakini Mungu aliingia katika maisha yetu na kutufanya viumbe vipya (2 Wakorintho 5:17). Huo ndio uponyaji mkubwa wa wote.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nini kipawa cha kiroho cha uponyaji?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries