settings icon
share icon
Swali

Je! Kuna umuhimu gani wa kujifunza Biblia katika kikundi?

Jibu


Kwa sababu Ukristo haukukusudiwa kuwa juhudi ya mtu binafsi, mafunzo ya Biblia katika kikundi sio ya thamani tu, ni ya thamani isiyokadrika. Kujifunza katika makundi ya watu wachache ni mzuri sana ambayo kwamba Yesu aliutumia kuwafundisha wanaume ambao wangetambulika kuwa mitume (Luka 6: 12-16; Marko 4:34).

Ukristo umekusudiwa kuwa wa uhusiano-kwanza, kati yetu na Mungu na, pili, kati yetu na wale wanaotuzunguka. Mafunzo ya kikundi cha watu wachache cha Biblia hutuhamisha toka kuwa watazamaji katika ibada ya kanisa ya kila wiki hadi kuwa washiriki wenye bidii katika jamii yenye nia moja iliyojitolea kwa ukuaji wa kiroho.

Tunapolichambua Neno la Mungu pamoja, tuna nafasi ya kushiriki mitazamo na ufahamu wetu tofauti na tunapanuliwa kwa sababu ya kuamshana. Habari zaidi huhifadhiwa wakati kuna ushirikiano tendaji, kwa hivyo ufahamu wetu wa Biblia huimarishwa. Matumizi na uwajibikaji huleta uelewo ambao huhamisha Neno la Mungu kutoka kwa akili hadi moyoni. Mabadiliko yanahimizwa (Warumi 12: 2), na maisha yetu yanabadilishwa. Wakati maisha yetu yamebadilishwa, maisha ya wale wanaotuzunguka yanabadilishwa pia.

Mahusiano hayatokei tu, na sisi sote tunahitaji kikundi cha marafiki kusaidia wakati wa dhoruba za maisha. Marafiki wanahitaji tuchukue wakati wetu mwingi na kiwango cha hatari na uaminifu. Waebrania 10: 24-25 inasema kuwa tunapaswa "Tujitahidi kushughulikiana kwa ajili ya kuongezeana bidii ya kupendana na kutenda mema. Tusiache ile desturi ya kukutana pamoja, kama vile wengine wanavyofanya. Bali tunapaswa kusaidiana." Ni wapi mahali bora pa kufanikisha hili kuliko katika kikundi cha mafunzo ya Biblia?

Mafunzo ya kikundi cha Biblia yanaweza kuwa mahali pa kusherehekea ushindi wa maisha, kupata msaada wa maombi, kuhimizwa wakati wa hali ngumu, na sisi wenyewe kujiweka kuwajibika katika ukuaji wetu wa kibinafsi. Mafunzo ya Biblia ya kikundi hutoa wakati uliopangwa wa kuzingatia mada ambazo zinaangazia mahitaji yetu au masilahi yetu. Yanatoa mahali pa kutia moyo na kujenga yanayotusaidia kusonga toka Jumapili hadi Jumapili na mahali salama pa kushughulikia changamoto tunazokabiliana nazo.

Waumini ni Mwili wa Kristo (Warumi 12: 5); kwa sababu hiyo, sisi ni mikono na miguu Yake duniani, wale ambao wataendeleza kazi Yake. Wakorintho wa Kwanza 12: 4-12, Warumi 12: 4-8, na Waefeso 4: 11-13 zinaorodhesha karama zilizopewa Mwili wa Kristo. Mafunzo ya Biblia ya vikundi vidogo ndio mahali ambapo watu wengi wanaanza kutambua na kuonyesha karama hizo. Tunapokua katika ufahamu wetu wa Biblia na kudumisha uhusiano wetu na Mungu na waumini wengine (Wakolosai 2: 7), tunajiami na silaa za kutosha kuishi na kushiriki injili na wale walio tunaosoma noa pamoja, maskani yeto na maeneo yake, na mahali pa kazi.

Kujitolea kwetu kwa kikundi cha mafunzo ya Biblia ni mfano kwa wale walio karibu nasi. Ni Dhahiri kwamba tunathamini ukuaji wetu wa kiroho vya kutosha kiwango cha kutumia muda wetu kwalo. Watoto wetu wanayatizama matendo yetu, na wanapata ujuzi wa kibinafsi juu ya kile inamaanisha kuwa mfuasi wa Kristo na kuheshimu Neno Lake. Wananufaika na kujitolea kwetu kwa sababu wanatuona tunaishi maisha yanayolingana na imani tunayoihimiza, tukikaza kwa wokovu wetu (Wafilipi 2:12).

Wengine wanaweza kuwa na hofu juu ya kuingia katika mazingira ya kikundi kidogo. Hofu ya kukataliwa na hofu ya kuathiriwa ni aina mbili ambazo zinaweza kuonekana kama majitu yanayozuia kile kinachoweza kuwa kitu bora kwetu. Lakini kuhusika katika kundi dogo kunaweza kuwa suluhu ya Mungu ya kukomesha upweke ambao unatushika katika ulimwengu huu ulio mbioni na, usio na utu.

Mungu alituumba sisi njia ambayo tunamhitaji Yeye na kuhitaji kila mmoja wetu. Neno lake kwetu ni kufikia wengine na kupendana. Wakolosai 3:16 inasema tunapaswa kuruhusu "Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu." Je! Ni mahali gani bora kwa hilo kuliko katika kikundi kidogo cha kujifunza Biblia?

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kuna umuhimu gani wa kujifunza Biblia katika kikundi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries