settings icon
share icon
Swali

Je! Misheni ya Kikristo ni gani?

Jibu


Misheni ya Kikristo ni kufutuata wito wa Kristo: kushiriki injili na ulimwengu unaopotea kupitia kwa hekima na nguvu za Mungu.

Umisheni wa Kikristo ni kumtii Kristo
Baada ya kifo na kufufka kwa Kristo, Bwana aliwaamuru wanafunzi wake kushiriki injili, ujumbe wa ukombozi wake: "Kwa sababu hii, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, 20nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati (Mathayo 28:19-20).

Utume mkuu vile vile upo kwa Wakristo hii leo. Badala ya kutuchosha na mizigo, kutii wito wa Mungu kunaleta furaha na tuzo mbinguni. Tunapaswa kutimiza utume wetu na sio kwa kulazimishwa bali kwa upendo: "Kwa kuwa upendo wa Kristo unatutia nguvu, kwa sababu tunasadiki kuwa mmoja alikufa kwa ajili ya wote, kwa hiyo wote walikufa. Naye alikufa kwa ajili ya watu wote, ili kwamba wote wanaoishi wasiishi tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa na kufufuliwa tena kwa ajili yao. … Haya yote yanatokana na Mungu, ambaye ametupatanisha sisi na nafsi yake kwa njia ya Yesu Kristo na kutupata sisi huduma ya upatanisho: Kwamba Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake mwenyewe, akiwa hawahesabii watu dhambi zao. Naye ametukabidhi sisi ujumbe huu wa upatanisho. Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Kristo, kana kwamba Mungu anawasihi kupitia kwa vinywa vyetu. Nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu. Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kwake yeye" (2 Wakorintho 5:14-21).

Mungu atabadilisha kila mmoja kwa kutumia mwanga wa kupofusha na kwa sauti ya Kristo jinsi alivyofanya kwa mtume Paulo. Badala yake, anawapa Wakristo utume wa kupatanisha (Matendo 1:8-9). Anafanya kazi kupitia kwetu, akiita wenye dhambi kumgeukia Kristo katika toba na imani.

Utume wa Kikristo ni kushiriki Kristo
Utume wetu ni kumtangaza Kristo kama Mwokozi pekee kutoka dhambini na njia pekee ya utele, uzima wa milele. Ni nani tunaambia? Yesu aliwaambia Wakristo kufikia "matiafa yote" (Mathayo 28:19). Yesu ametutuma kwa makundi yote ya watu, kwa kila kabila tamaduni ambao hawana wa kuwaambia injili.

Walakini, utume wa Kikristo hauishii huduma ya kimatiafa pekee. Huku waumini wakipaswa kuwaunga mkono kwa uaminifu wale ambao wanawafikia wale wa nchi za kigeni ambao hawajafikiwa Wakristo wote wana utume wa kushiriki Kristo na wenzao pale nyumbani na familia, marafiki, wafanyikazi wenza, na jamii.

Utume wa Kikristo wa kushiriki Kristo hauishii na wokovu wa mwenye dhambi. Agizo hilo lilikuwa la kuwafanya wanafunzi — sio waumini wenye hawajakomaa. Kwa hivyo, umisionari wa Kikristo hauhusishi uinjilisti tu pekee, bali na uanafunzi pia.

Utume wa Kikristo unamtegemea Kristo
Kushiriki injili kwa unyenyekevu, kwa ujasiri, na kwa furaha ni utume wetu wa Kikristo. Lakini hatuwezi kufanya hiyo peke yetu. Nguvu na matokeo ya utume wa Kikristo hutoka kwa Bwana. Yeye anatupa hekima, nguvu, na hamu ya kushuhudia! Kupitia ushuhuda wetu, Yeye hufanya kazi ya toba na imani moyoni mwa mwenye dhambi (2 Wakorintho 5: 20-21).

Ingawa utume ni kazi ya Mungu, Wakristo wanawajukumu la kuielewa na kuishiriki injili na kuwa na uhusiano thabiti na Kristo. Uhusiano kama huo hulinda dhidi ya unafiki. "Bali mtakaseni Kristo kuwa Bwana mioyoni mwenu. Siku zote mwe tayari kumjibu mtu yeyote atakayewauliza kuhusu sababu ya tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa heshima, 16mkizitunza dhamiri zenu ziwe safi, ili wale wasemao mabaya dhidi ya mwenendo wenu mzuri katika Kristo waaibike kwa ajili ya masingizio yao" (1 Petro 3: 15-16). Yesu alituhakikishia kuwa mateso yataambatana na utume, lakini Mungu hutumia hata mateso kwa wema (Warumi 8:28).

Kwa jumla, utume wa Kikristo ni kumtii Kristo, kushiriki Kristo, na kumtegemea Kristo. Hasa, wamishonari waliotumwa na Mungu kupitia msaada wa kanisa kwa wale ambao hawajafikiwa. Wakristo wote, hata hivyo, wana utume wa upatanisho. Bwana hufanya kazi kupitia wao kuwaokoa waliopotea. Je! Ni utume gani mkubwa zaidi ambao mtu anaweza kutimiza?

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Misheni ya Kikristo ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries