settings icon
share icon
Swali

Je! Ni kwa nini Yesu alimwambia yule kijana tajiri kuwa ataokolewa ikiwa ataitii amri?

Jibu


Ili uelewe jibu la Yesu kwa swali la huyu kijana Tajiri- "Nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?"- lazima tuzingatie mambo matatu: historia ya huyu kijana tajiri tawala, lengo la swali lake, na umuhimu wa injili ya Yesu Kristo. Huyu kijana alikuwa amemuuliza Yesu, "Mwalimu mwema, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?" (Mathayo 19:16). Yesu alijibu, "Lakini ukitaka kuingia uzimani, zitii amri" (aya ya 17). Kwa kuangalia kwa ghafula, inaonekana kuwa Yesu anasema kuwa huyu tajiri mdogo na hususani watu wote lazima waitii amri ili waokoke. Lakini hilo ndilo alikuwa anasema kweli? Tangu umuhimu wa ujumbe wa injili ni kuwa sisi wote tumeokolewa kwa neema kupitia kwa imani (Waefeso 2:8-9), ni kwa nini Yesu ampe tajiri kijana "mpango mbadala"?

Hadithi ya kijana tajiri inapatikana katika vitabu vitatu vya injili, Mathayo 19:16-23; Marko 10:17-22; na Luka 18:18-23. Huyu mtu anaelezewa kama "mtawala," kumaanisha alikuwa mfalme au hakimu wa kiwango fulani. Tangu hakuna mtawala wa Kirumu anaweza mhutubia Yesu kama "mwalimu" au "mkuu" inakusiwa kuwa mtu huyu ilikuwa kiongozi wa Kiyahudi katika hekalu ya Kiyahudi la mtaa. Mtu huyu alikuwa na "utajiri mwingi" (Mathayo 19:22), na Yesu baadaye alitumia mazungumzo Yake na huyu mtu kufindisha juu ya madhara pesa inaweza kuwa nayo katika mataminio ya mtu maishani (aya 23-24). Funzo Yesu anatoa katika tukio hili linahusu pesa, na sio wokovu wa matendo.

Kitu cha kwanza Yesu anasema kwa salambu za huyu tajiri, "Mwalimu mwema," ni kutukumbusha kuwa hakuna aliye mwema ila Mung utu (Mathayo 19:17). Yesu hakuwa anakana Uungu wake. Badala yake, papo hapo Yesu alikuwa anataka huyu tajiri afikirie maana halisi ya "wema)- kwa kuwa ni Mungu tu ndiye mwema, basi kile tunachokiita kizuri kibinadamu kinaweza kuwa kitu kingine tofauti kabisa Ukweli huu unajitokeza katika mazungumzo. Wakati huyo mto alimwuliza Yesu kuelezea hasa ile amri anapaswa kuitunza, Yesu alimsomea amri sita, hii ikiwa ni Pamoja na "umpende jirani yako kama nafsi yako" (Mathayo 19:19). Yule mtu akajibu, "Hizi zote nimezishika… nimepungukiwa na nini?" (aya 20), na hiyo ndiyo kauli mbiu. Yule kijana tajiri kawaida alikuwa wa dini na mnyofu katika kufuata haki. Shida yake ilikuwa alijichukulia kuwa mkamilifu kwa mjibu wa Sheria. Na hii ndio hali Yesu alipatia changamoto.

Yesu akamwambia yule mtu, "Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze vitu vyote ulivyo navyo, na hizo fedha uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate" (Mathayo 19:21). Yule Tajiri kijana aliamua kuwa Yesu alikuwa anaitisha zaidi. "akaenda zake kwa huzuni, kwa sababu alikuwa na mali nyingi" (aya ya 22). Badala ya kumtii maagizo ya Yesu, aligeuka na kumpa Bwana mgongo na kuenda zake. Uamuzi wa yule mtu bila shaka ulimhuzunisha Yesu pia, kwa sababu Yesu alimpenda (Marko 10:21).

Kwa kumwambia yule kijana tajiri azishike amri, Yesu hakuwa anasema kwamba angeokolewa kwa kutii amri hizo, badala yake, Yesu alikuwa anasisitiza Sheria kam kiwango kamili cha Mungu. Ikiwa unaweza kuitunza sheria kikamilifu, basi unaweza kuepuka adhabu ya dhambi- lakini hiyo ni ikiwa kubwa sana. Wakati yule kajana aliitika kuwa alikuwa amefikia kiwango cha Sheria, Yesu aliguzia hoja moja ambayo ilidhihirisha kuwa yule mtu hakuwa amaefikia uadilifu wa Mungu. Yule kijana hakuwa karibu kumfuata Bwana, hata kama hiyo ilimaanisha aachane na utajiri wake. Basi, yule mtu alikuwa anavunja amri mbili kuu; hakumpenda Bwana kwa moyo wake wote, na hakumpenda jirani yake kama nafsi yake. Alijependa sana (na utajiri wake). Mbali na kutunza amri "zote", vile alikuwa anadai, yule mtu alikuwa mwenye dhambi kama mtu yeyote. Sheria ilithibitisha hilo.

Ikiwa yule mtu alikuwa amempenda Mungu na watu wengine zaidi ya vile alivyopenda utajiri wake, angekuwa tayari kuacha mali yake na kumtumikia Mungu na watu wengine. Lakini hali haikuwa hivyo. Alikuwa amefany mali yake mungu, na kuyapenda kuliko Mungu. Kwa upasuaji mahususi, Yesu anafunua uchoyo uliokuwa ndani ya moyo wake-uchoyo ambao yule mtu hangedhania kuwa alikuwa nao. Kauli ya Yesu kuwa ni Mungu pekee aliye mwema (Mathayo 19:18) imetolewa katika jibu la yule kijana kwa mjibu wa amri ya Yesu.

Katika mazungumzo yake na yule kijan tajiri mtawa, Kristo hakufunza kuwa tumeokolewa kwa matendo mema ya Sheria. Ujumbe wa Biblia ni kuwa wokovu ni wa neema kupitia kwa Imani (Warumi 3:20, 28; 4:6); Wagalatia 2:16; Waefeso 2:9; 2 Timotheo 1:9). Badala yake, Yesu alitumia pendo la mali la yule kijana kuonyesha jinsi yule mtu alikuwa amepungikiwa na kiwango cha Mungu- vile sisi wote tumepungukiwa. Kijana tajiri alihitaji mwokozi vile vile sisi tunamwihitaji pia.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni kwa nini Yesu alimwambia yule kijana tajiri kuwa ataokolewa ikiwa ataitii amri?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries