settings icon
share icon
Swali

Ni wapi Maandiko ya Kiebrania yanatabiri kifo na ufufuo wa Masihi?

Jibu


Kote katika Maandiko ya Kiebrania, ahadi ya Masihi imepeanwa dhahiri. Huu unabii wa Masihi ulitengenezwa mamia, wakati mwingine maelfu ya miaka kabla ya Yesu Kristo kuzaliwa, na wazi Yesu Kristo ni mtu wa pekee ambaye ametembea dunia hii kuukamilisha. Kwa kweli, Kutoka Mwanzo hadi Malaki, kuna Zaidi ya unabii 300 maalumu unaolezea kuja kwa huyu Aliyepakwa Mafuta. Zaidi ya unabii huo unaolezea kuzaliwa Kwake na bikira, kuzaliwa Kwake Bethlehem, kuzaliwa Kwake kutoka kabila la Yuda, uzao Wake kutoka kwa Mfalme Daudi, Maisha yake yasio na dhambi, na upatanisho Wake kwa dhambi za watu Wake, kifo na ufufuo wa Masihi wa Kiyahudi, kadhalika, uliandikwa vyema katika unabii wa Maandiko ya Kiebrania, mbeleni kabla ya kifo na ufufuo wa Yesu Kristo kutokea katika historia.

Unabii bora unaojulikana katika Maandiko ya Kiebrania kuhusu kifo cha Masihi, Zaburi 22 na Isaya 53 hakika zinasimama. Hasa Zaburi 22 ni ya kushangaza kwa kuwa ilitabiri ishara nyingi tofauti kuhusu kusulubiwa kwa Yesu miaka elfu moja kabla ya Yesu kusulibishwa. Hapa ni baadhi ya mifano. Masihi "atatobolewa" mikono na miguu Yake (Zaburi 22:16; Yohana 20:25). Mifupa ya Masihi haitafujika (miguu ya mtu kwa kawaida ilikuwa inafujwa baada ya kusulubiwa kuharakisha kifo chao) (Zaburi 22:17; Yohana 19:33). Watu watagawanya nguo zote za Masihi (Zaburi 22:18; Mathayo 27:35).

Isaya 53, Maandiko bora ya Wayunani unabii wa Masihi unaojulikana kama unabii wa "Mtumishi wa Kuteseka", pia inaelezea kifo cha Masihi kwa ajili ya dhambi za watu Wake. Zaidi ya miaka 700 kabla ya Yesu kuzaliwa, Isaya anatoa habari za maisha na kifo Chake. Masihi atakataliwa (Isaya 53:3; Luka 13:34). Masihi atauliwa kama dhabihu kwa ajili ya dhambi ya watu Wake (Isaya 53:5-9; 2 Wakorintho 5:21). Masihi atakuwa kimya mbele ya washtaki Wake (Isaya 53:7; 1 Petro 2:23). Masihi atazikwa na matajiri (Isaya 53:9; Mathayo 27:57-60). Masihi atakuwa na wahalifu katika kifo Chake (Isaya 53:12; Marko 15:27).

Zaidi ya kifo cha Masihi wa Kiyahudi, kufufuka Kwake kutoka kwa wafu imetabiriwa pia. Unabii dhahiri Zaidi na unaojulikana bora kwa ufufuo ni ule umeandikwa na Daudi Mfalme wa Israeli katika Zaburi 16:10, ulioandikwa pia milenia kabla ya Yesu kuzaliwa: "Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu."

Katika sikukuu ya Kiyahudi ya Shavuot (Majuma auPentekoste), wakati Petro alihubiri mahubiri ya kwanza ya injili, alitetea kwa ujasiri kwamba Mungu alifufua Yesu Masihi wa Kiyahudi kutoka kwa wafu (Matendo 2:24). Kisha alieleza kwamba Mungu alifanya kitendo hiki cha kimuujiza ili kutimiza unabii wa Daudi katika Zaburi 16. Kwa kweli, Petro alinukuu maneno ya Daudi kwa undani kama yalivyo katika Zaburi 16:8-11. Miaka kadhaa baadaye, Paulo alifanya kitu sawa wakati alizungumza na jumuia ya Kiyahudi katika Antiokia. Kama Petro, Paulo alitangaza kwamba Mungu alifufua Yesu Masihi kutoka kwa wafu ili kutimiza Zaburi 16:10 (Matendo 13:33-35).

Ufufuo wa Masihi umedokezwa vikali katika zaburi nyingine ya Daudi. Tena, hii ni Zaburi 22. Katika mistari ya 19-21, Mwokozi wa kutezeka anaomba kwa ukombozi "kutoka kinywani mwa simba" (sitiari kwa Shetani). Ombi hili lisilo na tumaini kisha linafuatwa mara moja katika mistari ya 22-24 na wimbo wa kusifu ambao Masihi anamshkuru Mungu kwa kusikia maombi Yake na kumkomboa. Ufufuo wa Masihi umedokezwa wazi kati ya mwisho ya maombi katika mstari wa 21 na mwanzo wa wimbo ya kusifu katika mstari wa 22.

Tukirudi tena kwa Isaya 53: baada ya kutabiri kwamba Mtumishi wa Kutezeka wa Mungu atatezeka kwa dhambi ya watu Wake, nabii anasema kisha anaweza "kuondolewa nje ya ardhi ya wanaoishi." Lakini Isaya kisha anasema kwamba Yeye (Masihi) "ataona watoto Wake" na kwamba Mungu Baba "atarefusha siku Zake" (Isaya 53:5, 8, 10). Isaya anaendelea kuhakikisha tena ahadi ya ufufuo katika maneno tofauti: "Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika" (Isaya 53:11).

Kila kipengele cha kuzaliwa, maisha, kifo na ufufuo wa Masihi Yesu yalitabiriwa katika Maandiko ya Waebrania kitambo kabla ya matukio kuonekana katika enzi za historia ya binadamu. Ndio maana Masihi Yesu angeweza kusema kwa viongozi wa kidini wa Kiyahudi wa siku Zake, "Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia" (Yohana 5:39).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni wapi Maandiko ya Kiebrania yanatabiri kifo na ufufuo wa Masihi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries