settings icon
share icon
Swali

Muumini anaweza kupata faraja baada ya kifo cha mzazi?

Jibu


Kifo cha mzazi (au mwanachama yeyote wa familia) kinaweza kuwa cha uchungu kwa Mkristo. Hata wakati mmoja tuliopoteza ni muumini, si rahisi kusema kwaheri, hasa ikiwa kifo kilikuwa cha ghafla. Kuomboleza kwa wapendwa wetu ni sahihi na unatarajiwa; Kristo mwenyewe alilia kwenye kaburi la rafiki yake Lazaro (Yohana 11:35). Biblia hutoa faraja, na sisi kama Wakristo tunaweza kupata faraja hata katika kumpoteza mtu aliye mpendwa sana kwetu.

Katika kumpoteza mzazi wa Kikristo, faraja kubwa zaidi ya muumini ana matumaini na imani kwamba uhusiano wetu na wazazi wetu hauwezi kufa. Mkristo aliyempoteza mzazi Mkristo anaweza kupumzika katika ahadi ya kuwa kutakuwa na ushirika nao tena mbinguni. Mzazi wetu sasa yu pamoja na Kristo, akifurahia furaha yake (2 Wakorintho 5: 8). Wakati wa ufufuo, wote ambao walimkubali Kristo watatukuzwa na kupewa miili isiyoharibika (1 Wakorintho 15: 42-44; Yohana 11:25). Kwa Mkristo, Kristo ameshinda kifo! Kama Paulo anavyoandika kwa furaha katika 1 Wakorintho 15: 54-57, "Mauti imemezwa kwa kushinda. Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo."

Kumpoteza mzazi kunaweza kuwa vigumu zaidi ikiwa hatuna uhakika wa wokovu wa mzazi wetu. Lakini tunaweza bado kushikamana na ahadi za Mungu na kumtafuta faraja. Tunatarajia wakati ambapo vitu vyote vitatengenezwa upya, na kuamini kwamba Yeye ni wa haki na mzuri.

Mungu wa Biblia hufurahia kuwatia moyo walio adhirika na kuwaponya moyo uliovunjika (Yeremia 17:14; 2 Wakorintho 1: 3-4; 7: 6). Yeye ni "baba ya watoto wasio na baba" (Zaburi 68: 5). Tunapofadhaika kwa kuwapoteza wapendwa wetu, Mungu yuko tayari kutupa amani Yake. Katikati ya maombolezo yetu, tunaweza kujua uwepo wa Mungu yu pamoja nasi; hata katika huzuni yetu, tunaweza kumkaribia Yeye kwa maombi na ibada. Kama waumini, hatuna haja ya kusikitika peke yetu. Tuna wengine katika Mwili wa Kristo ambao watatusaidia kubeba mzigo, kushiriki maumivu, na "kulia na wale wanaomboleza" (Warumi 12:15).

Kufa kwa wazazi wetu kunaweza kuwa kwa chungu sana, hasa kwa kuwa wanacheza jukumu muhimu katika kuunda maisha yetu. Kwa kweli, mara nyingi wazazi wetu ndio ambao hutufariji tunapoumia, na kuwapoteza tunaweza kujihisi kama tumpoteza msaada wetu wa kihisia. Lakini Wakristo wanaweza kuwa na moyo kwa kuwa tunapata faraja zaidi kuliko kutoka kwa familia zetu; Mungu wa Uumbaji, ambaye anatujua bora zaidi kuliko tunavyojijua wenyewe, anaelewa maumivu yetu na anatamani kutukuza na kutuponya na kutupa amani yake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Muumini anaweza kupata faraja baada ya kifo cha mzazi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries