settings icon
share icon
Swali

Kila mtume alikufa namna gani? Je! Bibilia imerekodi kifo cha mitume?

Jibu


Mtume peke ambaye kifo chake kimeandikwa katika Bibilia ni Yakobo (Matendo Ya Mitume 12:2). Mfalme Herode alimweka Yakobo “afe kwa kisu,” kuna uwezekano kuwa alikatwa kichwa. Hali ya kifo cha mitume wengine zimehusiana kutakona na tamaduni ya Kanisa, kwa hivyo tusiweke uzito mwingi kwa tukio lo lote. Tamaduni ya Kanisa ya pamoja umekubalika kuhusiana na kifo cha mitume ni kuwa Mtume Petero alisulubiwa kichwa chake kikiangalia chini kwa msalaba wa umbo la X huko Rumi kwa kutimiza unabii wa Yesu (Yohana 21:18). Yafuatayo ni “tamaduni” zinazojulikana sana kuhusu kifo cha Mitume wengine:

Mathayo aliteseka kwa ajili ya injili huko Uhabeshi, aliuwawa na donda la kisu. Yohana alikumbana na mateso juu ya injili wakati alichomwa katika bakuli kubwa la mfuta yachomayo wakati wa uvumi wa mateso huko Rumi. Ingawa aliokolewa kimuujiza kutoka kwa kifo. Yohana alihukumiwa vidimbwi vya kisinga cha Patmosi. Alikiandika kitubu chake cha unabii cha Ufunuo huko Patmosi. Mtume Yohana baadaye alifunguliwa na akarudishwa nchi hii leo yaitwa Uturuki. Alikufa akiwa mzee, Mtume pekee aliyekufa kifo cha kawaida.

Yakobo, nduguye Yesu (si mtume halisi), alikuwa kiongozi wa Kanisa huko Yerusalemu. Alitubwa kutoka mnara wa juu sana wa Kusini-Mashariki wa Hekalu (takribani futi mia moja kwenda chini) wakati alikataa kumkana Babaye katika Kristo. Wakati waligundua kwamba ameponea mwanguko huo, maadui wake walimpiga Yakobo kwa rungu hadi akafa. Hii imetuhumiwa kuwa mnara ambao Shetani alikuwa amempeleka Yesu wakati wa majaribu.

Bartholomayo, ambaye anaitwa Nathanaeli, alikuwa mmisionari huko Asia. Alishuhudia ambayo sasa yaitwa Uturuki na akauwawa ka sababu ya kuhubiri injili huko Armenia, kwa kupigwa hadi kifo na kijiti. Andrea alisulubiwa kwa msalaba wa umbo la X huko Ugiriki. Baada ya kuchapwa kwa kijiti mara nyingi na walinzi saba, waliufunga mwili wake kwa msalaba kurefusha machungu yake. Wafuasi wake wakaripoti kuwa wakati aliongozwa kuelekea kwa msalaba, Andrea akawapungukia mkono kwa maneno yafuatayo, “kwa muda mrefu nimengoja na kutamani saa kama hii ya furaha. Mslaba umekwisha takaswa kwa mwili wa Kristo ulioangikikwa juu yake.” Aliendelea kuwahubiria watesi wake kwa siku mbili hadi wakati alikufa. Mtume Tomaso alichomelewa mkuki huko India wakati wa mojawapo ya safari zake kama mmisionari lilianzisha Kanisa huko. Thadayo, mtume aliyechaguliwa kuchukua nafasi ya Yuda Iskariote, alipigwa mawe na kichwa chake kutaktwa. Mtume Pauo alitezwa na baadaye kichwa chake kikakatwa na mfalme mwovu Niro huko Rumi katika mwaka wa A.D 67. Kuna tamaduni kuhusu mitume wengine vilevile, lakini hakuna hata mmoja inaweza kuaminika au kuwa na uungaji wa kitamaduni.

Si muimu ni namna gani mitume walikufa. Cha maana ni kuwa walikuwa tayari kukufa kwa sababu ya Imani yao. Ikiwa Yesu hakuwa amefufuka, mitume wangejua hivyo. Watu hawatakufa kwa kitu wanakijua kuwa uongo. Hoja kwamba mitume wote walikuwa tayari kufa kifo kibaya, walikataa kuikana Imani katika Kriso ni uthibitisho mkubwa kuwa kwa kweli walishuhudia ufufuo wa Yesu Kristo.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kila mtume alikufa namna gani? Je! Bibilia imerekodi kifo cha mitume?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries