settings icon
share icon
Swali

Kifo cha kiroho ni nini?

Jibu


Kifo ni kujitenga. Kifo cha kimwili ni kutenga nafsi kutoka kwa mwili. Kifo cha kiroho, ambacho ni muhimu zaidi, ni kutenganisha nafsi kutoka kwa Mungu. Katika Mwanzo 2:17, Mungu anamwambia Adamu kwamba siku ambayo atakula tunda alilokatazwa hakika "atafa." Adamu alianguka, lakini kifo chake cha kimwili hakikutoke mara hiyo; Mungu lazima awe na aina nyingine ya kifo kwa akili-kifo cha kiroho. Utengano huu kutoka kwa Mungu ndio ule hasa tunauona katika Mwanzo 3: 8. Wakati Adamu na Hawa waliposikia sauti ya Bwana, "walijificha kutoka mbele ya Bwana Mungu." Ushirika ulivunjika. Walikuwa wamekufa kiroho.

Mtu asiye na Kristo amekufa kiroho. Paulo anaelezea kuwa "kuwa mbali na maisha ya Mungu" katika Waefeso 4:18. (Kutengwa na uzima ni sawa na kuwa mfu.) Mtu wa kawaida, kama Adamu kujificha katika bustani, na kutengwa kutoka kwa Mungu. Tunapozaliwa tena, kifo cha kiroho kinaingiliwa. Kabla ya wokovu, tumekufa (kiroho), lakini Yesu anatupa uzima. "Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu," (Waefeso 2: 1). " Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote" (Wakolosai 2:13).

Kwa kuiweka katika mfano, fikiria juu ya kufufuka kwa Lazaro katika Yohana 11. Lazaro aliyekufa kimwili hakuweza kufanya kitu kwa nafsi yake mwenyewe. Yeye hakuwa na hisia sozote kwa yale yalikuwa yanaendelea, bila kujali maisha yote yaliyo karibu naye, zaidi ya msaada wowote au tumaini-ila kwa msaada wa Kristo ambaye ni "Ufufuo na Uzima" (Yohana 11:25). Kwa wito wa Kristo, Lazaro alikuwa amejazwa na uzima, naye akaitikia kwa kadri. Kwa njia ile ile, tulikuwa tumekufa kiroho, hatukuweza kujiokoa wenyewe, hatukuwa na uwezo wa kutambua maisha ya Mungu-mpaka Yesu akatuita kwake. Yeye "alitufufua" sisi; "si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake" (Tito 3: 5).

Kitabu cha Ufunuo kinasema "kifo cha pili," ambacho ni cha mwisho (na cha milele) kutenganishwa na Mungu. Wale ambao hawajawahi kuishi maisha mapya katika Kristo ndio watashiriki katika kifo cha pili (Ufunuo 2:11, 20: 6, 14; 21: 8).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kifo cha kiroho ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries