settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nani ambaye ni kichwa cha kanisa tunapoongea kibiblia?

Jibu


Vifungu viwili katika Agano Jipya vinaiweka wazi kuwa kichwa cha kanisa ni Yesu Kristo. Wakolosai 1: 17-18 inafundisha, "Yeye alikuwepo kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja. Yeye ndiye kichwa cha mwili, yaani kanisa, naye ndiye mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, ili yeye awe mkuu katika vitu vyote." Kifungu hiki kinafanya ulinganisho mfupi kati ya mwili wa mwanadamu na kanisa. Kanisa ni mwili, na Yesu ndiye kichwa. Yesu alikuwepo kabla ya vitu vyote na anashikilia vitu vyote pamoja. Hii ni pamoja na kanisa.

Waefeso 5: 22-25 inazungumzia uhusiano kati ya mume na mke na inajumuisha mafundisho ya Yesu kama kichwa cha kanisa:

"Ninyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama vile Kristo alivyo kichwa cha Kanisa, ambalo ni mwili wake, naye Kristo ni Mwokozi wake. Basi, kama vile Kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo na wake nao imewapasa kuwatii waume zao kwa kila jambo. Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake."

Katika kifungu hiki, wake wanapaswa kuwatii waume zao jinsi kanisa linavyomnyenyekea kwa Kristo, na waume wanapaswa kuwapenda wake zao kwa kujitolea kwa njia ambayo Kristo alikuwa tayari kulikufia kanisa. Katika muktadha huu, Yesu anaitwa "kichwa cha kanisa, ambao ni mwili wake." Pia Anaitwa Mwokozi wa kanisa lake.

Je! Inamaanisha nini kuwa kichwa cha kanisa? Wakolosai 1 na Waefeso 5 zinasisitiza uongozi wa Kristo na nguvu zake. Katika Wakolosai, Kristo ni kichwa kwa sababu Anashikilia vitu vyote pamoja. Katika Waefeso, Kristo ni kichwa kwa sababu Yeye ni Mwokozi.

Matokeo ya mafundisho haya ni makubwa mno. Kwanza, viongozi wa kanisa wanapaswa kusalimisha uongozi wao kwa Bwana Yesu Kristo. Yeye ndiye anayeongoza na kuamua mafundisho na utamaduni wa kanisa. Washiriki wa kanisa wanapaswa kumfuata Kristo kwanza na viongozi wa kidunia wawe wa pili, viongozi hao wanapomuiga Kristo (ona 1 Wakorintho 11: 1 na 1 Petro 5: 3-4)

Pili, upendo Yesu alio nao kwa kanisa unadhihirishwa katika nia Yake kwamba sisi pia tulipende kanisa. Kanisa sio jengo au shirika bali ni kikundi cha watu wanaomjua na kumwabudu Yesu. Wakristo wanafundishwa, "Tuangaliane na kuhimizana sisi kwa sisi katika upendo na katika kutenda mema. Wala tusiache kukutana pamoja, kama wengine walivyo na desturi, bali tuhimizane sisi kwa sisi kadiri tuonavyo Siku ile inakaribia" (Waebrania 10: 24-25). Kujiunga mara kwa mara na waumini wengine humheshimu Bwana, kunatutia moyo kibinafsi sisi kama waumini, na kutuwezesha kuwatia moyo na kuwahudumia wengine.

Huku kila kanisa litakuwa na viongozi wake wa mtaa, kiongozi mkuu wa kanisa lolote ni Bwana Yesu. Alisema, "Nitajenga kanisa langu" (Mathayo 16:18, kutilia mkazo umeongezwa); ni mali Yake. Yeye ndiye kichwa cha mwili na Ndiye pekee aliye na nguvu ya kuliongoza na kulipenda kanisa vya kutosha.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nani ambaye ni kichwa cha kanisa tunapoongea kibiblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries