settings icon
share icon
Swali

Kuna aina zipi tofauti za fasihi za kibiblia?

Jibu


Mojawapo ya ukweli unaovutia sana kuhusu Biblia ni kwamba, ingali ni mawasiliano ya Mungu (Mathayo 5:17, Marko 13:31; Luka 1:37; Ufunuo 22: 18-19), wanadamu walikuwa nguzo ya mchakato wa kuandika. Kama Waebrania 1: 1 isemavyo, "Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi," "Njia nyingi" zinajumuisha sajala tofauti za fasihi. Waandishi wa Biblia wa kibinadamu walitumia aina tofauti za fasihi ili kuwasilisha jumbe tofauti kwa nyakati tofauti.

Biblia ina fasihi ya kihistoria (Wafalme1 na 2 ), fasihi ya kidrama (Ayubu), stakabathi za kisheria (nyingi za kitabu cha Kutoka na Kumbukumbu la Torati), mistari ya nyimbo (Wimbo ulio bora na Zaburi), mashairi (mengi ya Isaya), fasihi za hekima (Mithali na Mhubiri), fasihi ya kiinjilisti (Ufunuo na sehemu za Danieli), hadithi fupi (Ruthu), mahubiri (kama ilivyoandikwa katika Matendo), hotuba na matangazo (kama yale ya Nebukadreza katika Danieli), sala (Zaburi nyingi), mafumbo (kama yale Yesu aliyowaambia), hadithi (kama zile Yothamu alizowaambia), na barua (Waefeso na Warumi).

Sajala tofauti zinaweza kukinzana. Zaburi nyingi, kwa mfano, pia ni sala. Baadhi ya mabarua yana mashairi. Kila aina ya fasihi ina sifa za pekee na inapaswa kufikiwa kwa kuzingatia. Kwa mfano, hadithi ya Jotamu (Waamuzi 9: 7-15) haiwezi kutafsiriwa sawa na Amri Kumi (Kutoka 20: 1-17). Kufafanua mashairi, kwa kutegemea mitindo na vifaa vingine vya mashairi, ni tofauti na kutafsiri maelezo ya kihistoria.

2 Petro 1:21 inasema kwamba "bali wanadamu walinena yalitoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu." Kwa kutumia neno la kisasa, mhariri mkuu wa Biblia alikuwa Roho Mtakatifu wa Mungu. Mungu aliweka alama ya uandishi wake kwenye kila kitabu kati ya vitabu 66 vya Biblia, bila kujali sajala ya fasihi. Mungu "alipumua" maneno yaliyoandikwa (2 Timotheo 3: 16-17). Kwa kuwa wanadamu wana uwezo wa kuelewa na kufahamu aina mbalimbali za fasihi, Mungu alitumia sajala nyingi za kuwasiliana Neno Lake. Msomaji wa Biblia atagundua madhumuni moja ambayo huunganisha sehemu za ukusanyaji. Atatambua malengo, maono, maudhui yaliyorudiwa, na wahusika wanaojirudia. Kupitia yote, atapata kwamba Biblia ni kitovu cha uandishi wa dunia-na Neno la Mungu mwenyewe.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kuna aina zipi tofauti za fasihi za kibiblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries