settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inamaanisha nini inaposema katika hasira yako usitende dhambi?

Jibu


Waefeso 4:26 inasema, “Mkikasirika, msitende dhambi, wala jua lisichwe mkiwa bado mmekasirika.” Katika kuelewa amri hii, ni vizuri kutofautisha hisia kutoka kwa vitendo. Sisi sote tunahisi hisia. Nyakati zingine tunahisi huzuni, majonzi, fadhaiko, msisimko, furaha, na hasira. Hisia kama hizo huja kwa kawaida na sio dhambi zenyewe. Ni jinsi tuvanavyotenda kuhusu hisia hizo ambayo inaweza kuwa dhambi. Hisia ni za ndani na hazielekezwi dhdi ya watu. Kitendo ni cha nje na kinaweza kuelekezwa vyema au ubaya kwa wengine.

Huu ndio muktadha wa aya: “Kwa hiyo kila mmoja wenu avue uongo na kuambiana kweli mtu na jirani yake, kwa maana sisi sote tu viungo vya mwili mmoja. Mkikasirika, msitende dhambi, wala jua lisichwe mkiwa bado mmekasirika, wala msimpe ibilisi nafasi. Yeye ambaye amekuwa akiiba, asiibe tena, lakini lazima ajishughulishe, afanye kitu kifaacho kwa mikono yake mwenyewe, ili awe na kitu cha kuwagawia wahitaji. Maneno mabaya yasitoke vinywani mwenu, bali yale yafaayo kwa ajili ya kuwajenga wengine kulingana na mahitaji yao, ili yawafae wale wasikiao. Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwake mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi. Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na masingizio pamoja na kila aina ya uovu. Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi” (Waefeso 4:25-32).

Kifungu hiki kinafuata mafundisho ya Paulo kuhusu asili mpya tunayokumbatia kupitia Roho Mtakatifu kwa imani katika Yesu Kristo (Waefeso 4:17-24). Ikiwa tunakasirika kwa sababu fulani-tunapatwa na hisia zisizo za hiari au shauku ya hasira-hatupaswi kuiruhusu ichochee matendo ya dhambi. Hatukai kwa hasira. Na hatudumu katika hisia hizo. Tunaishughulikia kwa haraka, kwa njia mwafaka na za kumtukuza Mungu, kwa hivyo haikui na kukuza hasira maishani mwetu. Ushauri wa kibiblia ni kukabiliana na hasira siku ile ile ya kukasirishwa. Kabla hatujaenda kulala usiku huo, lazima tungechukua hatua bora za kutafuta suluhu kwa tatizo na kupunguza hasira.

Ikiwa tunashindwa kukabiliana na hasira vilivyo na kujihusisha dhahiri katika dhambi, tunampa shetani nafasi fulani dhidi yetu (Waefeso 4:27). Kifungu hicho hicho kinaendelea kusema kwamba tunapaswa kujitahidi kuondoa hasira zote na dhambi zote sinazoandamana nayo: “Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na masingizio pamoja na kila aina ya uovu” (aya ya 31).

Badala ya kuruhusu hisia za hasira kugeuka na kuwa matendo ya dhambi, tanapaswa “Kuwa wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi” (Waefeso 4:32). Yote ni sehemu ya “utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu” (aya ya 24). Mojawapo ya nguvu ambazo Roho Mtakatifu amewapa waumini baada ya mabadiliko yao ya kiroho kupitia imani katika Yesu Kristo ni kiasi (soma Wagalatia 5:22-23). Tunahitaji kumwomba Mungu atujaze na Roho wake tunapokasirika; kujidhibiti itakuwa ni matokeo ya kiajabu.

Sisi sote huruhusu hasira zetu zitutawale wakati mwingine. Wakati tumekosewa au kuhisi kuwa tumekandamizwa, kwa kawaida tunataka kulipiza kisasi au “kusuluhisha tatizo” kwa njia ya haraka zaidi. Lakini wakati mwitikio wetu unahusisha “ghadhabu, hasira, makelele na masingizio” (Waefeso 4:31), tumevuka mpaka. Tumetenda dhambi katika hasira zetu na kumpa shetani nafasi. Wakati mwingine, muda mrefu kabla ya tungekuwa tumesonga mbele, tunakuwa na hamu ya kurejerelea jeraha na kushikilia hasira. Hii inasababisha uchungu tu. Ni lazima tujisalimishe kwa Roho Mtakatifu na kutumainia nguvu zake kuishinda dhambi hiyo.

Sulemani katika hekima yake alikuwa na baadhi ya mambo ya vitendo ya kusema kuhusu jinsi ya kukabiliana na hasira:

“Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi, bali anayekasirika haraka huonyesha upumbavu” (Mithali 14:29).
“Jawabu la upole hugeuza ghadhabu, bali neno liumizalo huchochea hasira” (Mithali 15:1).

“Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi, bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi” (Mithali 15:18).
“Ni afadhali mtu mstahimilivu kuliko shujaa, mtu anayeitawala hasira yake kuliko yule autekaye mji” (Mithali 16:32).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inamaanisha nini inaposema katika hasira yako usitende dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries