settings icon
share icon
Swali

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Yusufu?

Jibu


Yusufu alikuwa mwana wa kumi na moja wa Yakobo, mwanawe wa kwanza kupitia mke wake aliyempenda, Raheli. Hadithi ya Yusufu inapatikana katika Mwanzo 37-50. Baada ya kutangaza kuzaliwa kwake, tunamwona Yusufu baadaye akiwa na umri wa miaka kumi na saba akirudi kutoka kuchunga kundi la kondoo pamoja na ndugu zake wa kambo kumpa Yakobo ripoti mbaya juu yao. Pia tunaambiwa kwamba Yakobo "alimpenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa uzee wake, akamfanyia kanzu ndefu" (Mwanzo 37:3). Ndugu zake Yusufu walijua baba yao alimpenda Yusufu kuliko wao, ambayo iliwasababisha wamchukie (Mwanzo 37:4). Kufanya mambo mabaya zaidi, Yusufu alianza kuhusisha ndoto zake kwa familia-maono ya kinabii yaliyoonyesha Yusufu siku moja angetawala juu ya familia yake (Mwanzo 37:5-11).

Chuki kuelekea Yusufu ilifikia kilele wakati ndugu zake walipanga kumuua jangwani. Reubeni, kifungua mimba, alikataa papo hapo kuua na akapendekeza wamtupe Yusufu ndani ya kisima, kwa vile alipanga kurudi na kumwokoa kijana. Lakini, katika ukosefu wa Reubeni, wafanyabiashara wengine walipita, na Yuda alipendekeza kumwuza Yusufu kwa utumwa; ndugu walikamilisha kazi kabla ya Reubeni kumwokoa. Wavulana walichukua kanzu ya Yusufu na, baada ya kuzamisha kanzu katika damu ya mbuzi, walidanganya baba yao katika kufikiria mwanawe aliyempenda ameuawa na wanyama wa mwitu (Mwanzo 37:18-35).

Yusufu aliuzwa na wafanyabiashara kwa Mmisri wa cheo cha juu aliyeitwa Potifa na hatimaye akawa msimamizi wa nyumba ya Potifa. Katika Mwanzo 39 tunasoma juu ya jinsi Yusufu alivyotia fora katika majukumu yake, akawa mmoja wa watumishi wa kuaminiwa zaidi wa Potifa, na akawekwa msimamizi wa nyumba yake. Potifa aliweza kuona kwamba, chochote Yusufu alifanya, Mungu alionekana kupendezwa juu yake na alifanikiwa katika yote aliyoyafanya. Kwa bahati mbaya, mke wa Potifa alijaribu kumtongoza Yusufu. Yusufu mara kwa mara alikataa kutongozwa naye, akionyesha heshima kwa bwana ambaye alimkabidhi mengi na kusema kwamba itakuwa "jambo baya na dhambi dhidi ya Mungu" kwa yeye kulala na mke wa Potifa (Mwanzo 39:9). Siku moja mke wa Potifa alimpata Yusufu kwa joho na tena akafanya maendeleo ya kingono. Yusufu akatoroka, akachaa joho lake mkononi mwake. Kwa hasira, akamshtaki Yusufu kwa uongo wa kujaribu kumbaka, na Potifa akamtia gerezani (Mwanzo 39:7-20).

Jelani, Yusufu alibarikiwa tena na Mungu (Mwanzo 39:21-23). Yusufu alifafanua ndoto za wafungwa wenzake wawili. Ufafanuzi wote ulithibitisha kuwa wa kweli, na mmoja wa wanaume baadaye aliachiliwa kutoka jela na kurejeshwa kwa cheo chake kama mwandazi divai wa mfalme (Mwanzo 40:1-23). Lakini mwandazi divai alisahau kuhusu Yusufu na akashindwa kuzungumza kwa Farao juu yake. Miaka miwili baadaye, mfalme mwenyewe alikuwa na ndoto za kusumbua, na mwandazi divai alikumbuka kipawa cha Yusufu cha kutafsiri. Mfalme alimwita Yusufu na kumwambia ndoto zake. Kulingana na ndoto za Farao, Yusufu alitabiri miaka saba ya mavuno makubwa na ikifuatiwa na miaka saba ya njaa kali katika Misri na kumshauri mfalme kuanza kuhifadhi nafaka katika matayarisho ya upungufu ujao (Mwanzo 41:1-37). Kwa hekima yake, Yusufu alifanywa mtawala katika Misri, wa pili tu kwa mfalme. Yusufu alikuwa na wajibu wa kuhifadhi chakula wakati wa miaka wa mavuno mengi na kuiuza kwa Wamisri na wageni wakati wa miaka ya njaa (Mwanzo 41:38-57). Katika miaka hii ya mavuno mengi Yusufu alikuwa na wana wawili-Manase na Efraimu (Mwanzo 41:50-52).

Wakati njaa ilipiga, hata Kanaani iliathirika. Yakobo akatuma wanawe kumi kwenda Misri kununua nafaka (Mwanzo 42:1-3). Aliweka Benyamini, kitinda mimba wake na mwana wa pekee mwingine wa Raheli, nyuma (Mwanzo 42:4). Wangali Misri, wanaume walikutana na ndugu yao aliyepotea kwa muda mrefu, ambaye hawakumtambua. Yusufu, hata hivyo, aliwatambua ndugu zake. Aliwajaribu kwa kuwashtaki kuwa wapelelezi. Aliwafunga kwa muda wa siku tatu kisha akawaachilia wote ijapokuwa mmoja, akituma pamoja nao nafaka kwa kaya zao na kuwataka kurudi na ndugu yao mdogo zaidi (Mwanzo 42:6-20). Bado bila kujua utambulisho wa Yusufu, ndugu waliumizwa na hatia kwa kumwuza ndugu yao miaka kadhaa iliyopita (Mwanzo 42:21-22). Yusufu alisikia majadiliano yao na akageuka upande na kulia (Mwanzo 42:23-24). Alimwaacha Simeoni na akawatuma wengine, akarudisha kwa siri fedha zao kwenye magunia yao ya nafaka (Mwanzo 42:25). Wakati ndugu waligundua baadaye kuwa fedha zilirejeshwa, waliogopa hata zaidi (Mwanzo 42:26-28, 35). Walipofika nyumbani, walimwambia Yakobo yote yaliyotokea. Yakobo aliomboleza tena kupotea kwa Yusufu na kuongezeka kwa kupotea kwa Simeoni. Alikataa kumtuma Benyamini, licha ya ahadi ya Reubeni kwamba, ikiwa hangerudi na Benyamini, Yakobo angeweza kuua wana wawili wa Reubeni (Mwanzo 42:35-38).

Njaa ikawa kali sana kiasi kwamba Yakobo alikubali. Yuda alimshawishi Yakobo kutuma Benyamini pamoja naye, akitoa maisha yake kama dhamana (Mwanzo 43:1-10). Yakobo alikubali, kutuma pia matunda mazuri na pesa mara mbili kwa nafaka (Mwanzo 43:11-14). Wakati Yusufu aliwaona wanaume, aliwaagiza watumishi wake kuchinja mnyama na kuandaa chakula kwa ajili ya ndugu kula pamoja naye (Mwanzo 43:15-17). Wakiogopa kwa mwaliko kwa nyumba ya Yusufu, ndugu waliomba msamaha kwa mtumishi wa Yusufu kwa fedha ambazo zilibadilishwa mara ya kwanza. Mtumishi wa Yusufu aliwahakikishia na kumtoa nje Simeoni (Mwanzo 43:18-25). Wakati Yusufu alirejea, ndugu zake wakamsujudia, akitimiza unabii wake wa awali (Mwanzo 43:26). Aliuliza juu ya ustawi wa familia zao na tena akalia, wakati huu akijiondoa kuenda chumba chake (Mwanzo 43:27-30). Wakati wanaume walipokuwa wameketi kula chakula, kwenye meza tofauti kutoka kwa Yusufu, walishangaa kupangwa kwa mpangilio wa umri wa kuzaliwa. Benyamini alipewa sehemu mara tano zaidi ya ndugu wengine walivyopokea (Mwanzo 43:31-34). Kabla ya kuwatuma kwa baba yao, Yusufu alijaribu tena ndugu zake kwa kurudisha fedha zao kwenye magunia yao ya nafaka na kuweka kikombe chake cha fedha katika gunia la Benyamini. Aliwaacha ndugu zake kuanza safari yao na kisha kutuma mtumishi wake nyuma yao ili kujifanya hasira na kutishia kumwua Benyamini. Kurudi mbele ya Yusufu, Yuda aliomba kwa ajili ya maisha ya Benyamini, akisema kwamba, ikiwa Benyamini angekufa, vivyo hivyo Yakobo angekufa. Yuda alielezea huzuni wa Yakobo juu ya kupotea kwa Yusufu na imani yake kwamba hangeweza kuvumilia kupotea kwa kaka yake Yusufu. Yuda pia alizungumza juu ya ahadi yake kwa Yakobo na akatoa maisha yake kwa ajili ya maisha ya Benyamini (Mwanzo 44).

Alipoona ushahidi huu wa mabadiliko ya mioyo wa ndugu zake, Yusufu aliwafukuza watumishi wake wote na kulia kwa wazi na kwa sauti ya kutosha kusikika na nyumba ya Farao. Kisha akajidhihirisha kwa ndugu zake (Mwanzo 45:1-3). Yusufu mara moja akawahakikishia, akiwaambia wasijikasirikie wenyewe kwa kile walimtendea na kusema kwamba Mungu alimtuma Misri ili awahifadhi (Mwanzo 45:4-8). Yusufu alithibitisha msamaha wake miaka kadhaa baadaye, baada ya kifo cha baba yake, akisema kwamba, ingawa ndugu zake walikusudia maovu kwake, Mungu alikuwa amekusudia mema (Mwanzo 50:15-21). Yusufu aliwatuma ndugu zake kwa Yakobo ili kuokoa wa nyumba zao waliobaki ili kuja kuishi Gosheni, ambapo wangekuwa karibu na Yusufu na angeweza kuwakimu (Mwanzo 45:9--47:12).

Yakobo alikuja kuishi Misri na familia yake yote. Kabla ya kifo chake, Yakobo alibariki wana wawili wa Yusufu na kumshukuru Mungu kwa wema Wake: "Sikudhani ya kwamba nitakuona uso wako, na Mungu amenionyesha na uzao wako pia" (Mwanzo 48:11). Yakobo alitoa baraka kubwa kwa mdogo wa wana wawili (mistari 12-20). Baadaye katika historia ya Israeli, Efraimu na Manase, kabila za Yusufu, mara nyingi walichukuliwa kuwa kabila mbili tofauti. Ukoo wa Yakobo uliishi Misri kwa miaka 400, hadi wakati wa Musa. Wakati Musa aliwaongoza Waebrania kutoka Misri, alichukua mabaki ya Yusufu pamoja naye, kama Yusufu alivyoomba (Mwanzo 50:24-25; tazama Kutoka 13:19).

Kuna mengi ya kujifunza kutoka hadithi ya Yusufu. Kama wazazi, tuna maonyo juu ya upendeleo wa Yakobo na athari ambayo inaweza kuwa kwa watoto wengine kama inavyoonekana katika kipenzi kijana wa Yusufu na wivu na chuki ya ndugu zake. Tuna mfano mzuri wa jinsi ya kushughulikia majaribu ya kingono-kimbia (Mwanzo 39:12, tazama 2 Timotheo 2:22), na tuna picha wazi ya uaminifu wa Mungu. Hawaachi watoto Wake, hata katika kati ya mateso: "Bwana alikuwa pamoja na Yusufu" (Mwanzo 39:3, 5, 21, 23).

Kunaweza kuwa na hali nyingi za kuhuzunisha tunayojipata ndani wenyewe, na baadhi yao huenda zikawa hata si za haki, kama zilivyokuwa katika maisha ya Yusufu. Hata hivyo, kama tunavyojifunza kutokana na akaunti ya maisha ya Yusufu, kwa kuendelea kuwa waaminifu na kukubali kwamba Mungu ndiye ana udhibiti wa mwisho, tunaweza kuwa na hakika kwamba Mungu atazawadi uaminifu wetu katika ukamilifu wa wakati. Nani angeweza kumlaumu Yusufu ikiwa angewarudisha ndugu zake katika mahitaji yao? Bado Yusufu aliwaonyesha huruma, na Mungu anataka tuwe na rehema juu ya dhabihu nyingine zote (Hosea 6 6; Mathayo 9:13).

Hadithi ya Yusufu pia inaonyesha utambuzi wa ajabu kwa jinsi Mungu anavyofanya kazi kwa mamlaka ili kushinda uovu na kuleta mpango Wake. Baada ya mateso yake yote, Yusufu aliweza kuona mkono wa Mungu ukifanya kazi. Alipokuwa akidhihirisha utambulisho wake kwa ndugu zake, Yusufu alizungumza juu ya dhambi zao kwa njia hii: "Msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu. . . . Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu"(Mwanzo 45:5, 8). Baadaye, Yusufu aliwahakikishia ndugu zake, akitoa msamaha na kusema, "Nanyi kweli mlikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema" (Mwanzo 50:20). Makusudio mabaya zaidi ya mwanadamu hayawezi kamwe kuzuia mpango kamili wa Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Yusufu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries