settings icon
share icon
Swali

Yuda Iskariote alikuwa nani?

Jibu


Yuda Iskariote kwa kawaida anakumbukwa kwa jambo moja: kumsaliti Yesu. Alikuwa mmoja wa wanafunzi kumi na wawili ambao waliishi na Yesu na kumfuata kwa miaka mitatu. Alishuhudia huduma ya Yesu, mafundisho yake, na miujiza Yake mingi. Alikuwa mweka hazina wa kundi na akatumia nafasi hii ya kuaminika kuiba kutoka kwenye rasilimali yao (Yohana 12: 6).

Yuda lilikuwa jina lililojulikana sana enzi hizo, na kuna Yuda wengine kadhaa waliotajwa katika Agano Jipya. Mmoja wa wanafunzi wengine alikuwa anaitwaye Yuda (Yohana 14:22), na hivyo alikuwa mmoja wa ndugu wa Yesu (Marko 6: 3). Ili kutofautisha, Yohana 6:71 na Yohana 13:26 zinamrejelea msalitiwa wa Kristo kama "Yuda, mwana wa Simoni Isikariote."

Wasomi wana maoni kadhaa jinsi alivyopewa jina hilo. Dhana moja inasema kwamba Iskariote inarejelea Keriothi, eneo au mji huko Yudea. Wazo jingine ni kwamba linamaanisha Sicarii, kikosi cha wauaji waasi wa Kiyahudi.

kulihusisha na Sicarii kunaruhusu dhanio za kuvutia juu ya nia ya Yuda ya kumsaliti Yesu, lakini ukweli kwamba alifanya uamuzi wa kumsaliti Yesu (Luka 22:48) bado unasalia vile vile. Jina la Iskariote ni la muhimu, ikiwa bila sababu yeyote, kwa hiyo inaondoa shaka yoyote kuhusu ni Yuda ambaye anazungumziwa hapa.

Hapa kuna baadhi ya mambo tunapata kutoka kwa mistari muhimu juu ya Yuda na usaliti wake:

Kwa Yuda fedha ilikuwa ya maana. Kama imekwisha elezwa tayari, alikuwa mwizi, kulingana na Mathayo 26: 14-15, makuhani wakuu walilimpa "sarafu za fedha thelathini" ili amsaliti Bwana.

Yesu alijua tangu mwanzo kile ambacho Yuda Iskariote angefanya. Yesu aliwaambia wanafunzi wake, "Je! Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?" (Yohana 6:70). Na katika chakula cha jioni, Yesu alitabiri kusaliti kwake na kumtambua msaliti: "Basi Yesu akajibu, Ndiye mtu yule nitakayemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge, akalitwaa akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote" (Yohana 13:26).

Yesu alisema kwamba Yuda Iskariote hakuwa "mtakatifu"; yaani, hakuwa amejazaliwa tena na hakuwa amesamehewa dhambi zake (Yohana 13: 10-11). Kwa kweli, Yuda alitiwa nguvu kufanya yale aliyotenda na shetani mwenyewe: "Na baada ya hilo tonge Shetani alimwingia. Basi Yesu akamwambia, Uyatendayo yatende upesi" (Yohana 13:27).

Wanafunzi wengine hawakuwa na dokezi lolote kwamba Yuda Iskariote alikuwa na mawazo ya udanganyifu. Wakati Yesu alitaja msaliti katikati yao, wanafunzi wengine walionyesha shaka na kuulizana ni nani miongoni mwao angekuwa si mwaminifu (Yohana 13:22). Hakuna mtu aliyemshuku Yuda. Alikuwa mmoja wa wale kumi na wawili aliyeaminika sana. Hata wakati Yesu alimwambia Yuda, "Uyatendayo yatende upesi" (Yohana 13:27), na Yuda aliondoka kwenye mlo wa Mwisho, wengine waliokuwa wamekaa mezani walidhani Yuda alikuwa ametumwa kununua chakula kingine zaidi au kwenda kutoa msaada (mistari 28-29).

Yuda Iskariote alimsaliti Bwana kwa busu, kikamilifu ujanja wake wa dhati (Luka 22: 47-48). Baada ya kutenda tendo lake la kustahajabisha, Yuda "alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia" (Mathayo 27: 3). Lakini tunajifunza kwamba majuto sio sawa na toba — badala ya kurekebisha au kutafuta msamaha, "akaondoka; akaenda, akajinyonga" (Mathayo 27: 5).

Yuda Iskariote alitimiza unabii wa Zaburi 41: 9, "Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake" (tazama Yohana 13:18). Hata hivyo, Yuda alikuwa bado anajibika kwa matendo yake. Yesu alisema, "Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa" (Mathayo 26:24).

Mathayo 27: 6-8 inasema kuwa makuhani wakuu walichukua ile "pesa ya damu" kutoka kwa Yuda na kununua kiwanja cha mtumbi na kukifanya kuwa mahali pa kuwazika wageni (na hivyo inatimiza unabii wa Zakaria 11: 12-13). Matendo 1: 18-19 inaendeleza hadithi ya kile kilichotokea baada ya kifo cha Yuda na kutupa maelezo ya zaidi ziada. Luka anasema, "Basi mtu huyu alinunua konde kwa ijara ya udhalimu; akaanguka kwa kasi akapasuka matumbo yake yote yakatoka. Ikajulikana na watu wote wakaao Yerusalemu; hata konde lile likaitwa kwa lugha yao Akeldama, maana yake, konde la damu." Maelezo ya ziada tunayojifunza kutoka kwa Luka ni kwamba, baada ya Yuda kujinyonga, mwili wake ulianguka ndani ya shamba ambalo lilinunuliwa kwa fedha alizozipata kwa njia ya uovu.

Kutokana na uhusiano wa karibu wa Yuda na Yesu wakati wa miaka mitatu ya huduma yake, ni vigumu kufikiria jinsi angeweza kufuata njia hiyo ya usaliti. Hadithi ya Yuda inatufunza tujilinde dhidi ya hisia ndogo ndogo zinazojibuka taratibu na ambazo hupata nguvu na uwezo katika maisha yetu na ambazo zinaweza kufungulia njia zingine mbaya za mvuto zaidi. Hadithi yake pia ni kumbukumbu kwamba jinsi mtu anavyoonekana waweza kuwa danganyifu. Yesu alifundisha, " Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu" (Mathayo 7: 22-23).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Yuda Iskariote alikuwa nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries