settings icon
share icon
Swali

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Yoshua?

Jibu


Yoshua anajulikana bora kama wa pili katika mamlaka ya Musa ambaye anachukua hatamu na kuwaongoza Waisraeli katika Nchi ya Ahadi baada ya kifo cha Musa. Yoshua anazingatiwa kuwa mmoja wa viongozi wakuu Zaidi wa kijeshi wa Biblia kwa kuongoza ushindi wa miaka saba ya Nchi ya Ahadi, na mara nyingi huchukuliwa kama kielelezo kwa uongozi na chanzo cha matumizi halisi ya jinsi ya kuwa kiongozi bora. Hebu tuangalie maisha yake kutoka mtazamo wa kibiblia.

Kama kiongozi wa kijeshi, Yoshua anaweza kuchukuliwa kuwa mmoja wa majemadari wakuu katika historia ya binadamu, lakini itakuwa ni kosa kusifu ushindi wa Israeli tu kwa ujuzi wa Yoshua kama jemadari mkuu wa kijeshi. Mara ya kwanza tunamwona Yoshua ni katika Kutoka 17 katika vita dhidi ya Waamaleki. Kutoka 17:13 inatuambia kwamba Yoshua "akawaangamiza Amaleki na watu wake," na hivyo tunajaribiwa kuhitimisha kwamba utaalamu wa kijeshi wa Yoshua uliokoa siku hiyo. Lakini katika kifungu hiki tunaona jambo lisilo la kawaida likijitokeza. Katika mstari wa 11 tunasoma, "Ikawa, Musa alipoinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda." Hatimaye, mikono ya Musa ilikua kuchoka kiasi kwamba jiwe lingeletwa kwake ili kulikalia na Haruni na Huri walishika mikono yake juu. Kwa hiyo, tunaona katika nakshi hii kwamba Yoshua alishinda kwa sababu Mungu alimpa vita.

Hivyo hivyo kunaweza kusemwa juu ya ushindi wa kijeshi katika Nchi ya Ahadi. Bwana alikuwa ameahidi ushindi wa uhakika na kuutoa kwa njia ya kushawishi. Ya pekee ni katika vita vya Ai tu (Yoshua 7). Kuna mambo kadhaa ya kufahamu kuhusu tukio hili. Israeli walivunja imani na Mungu kuhusu "yaliyowekwa wakfu" (Yoshua 7:1). Mungu alikuwa amewaagiza Waisraeli kuweka kila kitu wakfu kwa kuaangamizwa (Yoshua 6:17), na Akani alikuwa amejiwekea baadhi ya mali yaliyoporwa kutoka kwa vita vya Yeriko. Kwa sababu hiyo, Mungu aliwahukumu kwa kutowapa ushindi huko Ai. Kitu kingine cha kufahamu ni kwamba hakuna amri ya wazi ya Mungu kwenda dhidi ya Ai. Kusudi la kuweka hadithi hizi mbili za vita kwa pamoja ni kuonyesha kwamba wakati Mungu anaweka mpango na ajenda, ushindi unafuatia, lakini wakati mtu anaweka mpango na ajenda, kushindwa kunafuatia. Yeriko ilikuwa vita vya Bwana; Ai haikuwa. Mungu alikomboa hali hiyo na hatimaye akawapa ushindi, lakini si hadi lengo la somo kutolewa.

Ushahidi zaidi wa sifa za uongozi wa Yoshua unaweza kuonekana katika imani yake kama mwamba imara katika Mungu. Wakati Waisraeli walipokuwa katika mpaka wa Nchi ya Ahadi katika Hesabu 13, Mungu aliamuru Musa kutuma watu kumi na wawili ili kupeleleza nchi, mmoja kutoka kwa kila kabila la Israeli. Baada ya kurudi, kumi waliripoti kwamba nchi hiyo, ingawa ilikuwa karimu kama vile Bwana ameahidi, ilikuwa imemilikiwa na wapiganaji wenye nguvu na wenye ukali wanaoishi katika miji mikubwa na yenye kuimarika. Zaidi ya hayo, Wanefili (majitu kutoka mtazamo wa Waisraeli) walikuwa katika nchi. Yoshua na Kalebu walikuwa wawili tu waliowahimiza watu kuchukua nchi (Hesabu 14:6-10). Hapa tunaona kitu kimoja kinachowatenga Yoshua (na Kalebu) mbali na Waisraeli wengine — waliamini katika ahadi za Mungu. Hawakutishwa na kimo cha wapiganaji au nguvu ya miji. Badala yake, walimjua Mungu wao na kukumbuka jinsi alivyofanya Misri, taifa lenye nguvu zaidi duniani wakati huo. Ikiwa Mungu angeweza kushughulikia jeshi lenye nguvu la Misri, kwa hakika angeweza kushughulikia makabila mbalimbali ya Wakanaani. Mungu alizawadi imani ya Yoshua na Kalebu kwa kuwasamehe kutoka kizazi kizima cha Waisraeli ambacho kingeangamia jangwani.

Tunaona uaminifu wa Yoshua katika tendo la utii kuwaweka wakfu watu kabla ya uvamizi wa Nchi ya Ahadi na tena baada ya kushindwa huko Ai. Lakini hakuna uaminifu wa wazi wa Yoshua unaonyeshwa kuliko katika mwisho wa kitabu kinachobeba jina lake wakati anawakusanya watu pamoja mara moja ya mwisho na kusimulia matendo ya Mungu kwa niaba yao. Baada ya hotuba hiyo, Yoshua anawahimiza watu kuacha sanamu zao na kubaki waaminifu kwa agano ambalo Mungu alifanya nao huko Sinai, akisema, "Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA"(Yoshua 24:15).

Hivyo tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Yoshua? Je! Tunaweza kutoa kanuni kwa uongozi kutoka kwa maisha yake? Hakika. Kwamba Mungu alimpa ushindi katika kuchukua Nchi ya Ahadi hachukui kutoka kwa uongozi wake wa kijeshi. Zaidi ya hayo, alikuwa kiongozi mwenye uwezo zaidi wa Waisraeli, lakini ujuzi wake katika uongozi si somo la msingi tunapaswa kutoa kutoka maisha ya Yoshua. Somo bora zaidi ni uaminifu wa Yoshua, msimamo wake dhidi ya wapelelezi kumi ambao walileta ripoti kuumbua kuhusu vikwazo katika kuchukua Nchi ya Ahadi, na ari yake katika kuhakikisha uaminifu wa agano la watu. Lakini hata imani yake haikuwa kamilifu. Kuna ukweli kwamba Yoshua alituma wapelelezi Yeriko hata ingawa Mungu alikuwa amehakikisha ushindi, na kisha kuna kujiamini zaidi alioonyesha katika vita vya Ai.

Somo la msingi la kutuo kutoka maisha ya Yoshua ni kwamba Mungu ni mwaminifu kwa ahadi Zake. Mungu aliahidi Ibrahimu kuwa wazao wake watakaa katika nchi, na, chini ya Yoshua, Mungu aliwaleta watu katika nchi aliyoahidi kuwapa. Tendo hili lilikamilisha kazi ya ukombozi ambayo Mungu alianza na Musa katika kuwaleta Israeli nje ya Misri. Pia ni aina ambayo inayoonyesha ukombozi wa mwisho ambao Yesu analeta kwenye jumuiya ya imani. Kama Musa, Yesu alituokoa kutoka minyororo na utumwa wa dhambi, na, kama Yoshua, Yesu atatuleta katika Nchi ya Ahadi ya Milele na mapumziko ya Sabato ya milele (Waebrania 4:8-10).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Yoshua?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries