settings icon
share icon
Swali

Tunafaa kujipatia nini kutoka kwa uhai wa mtume Yohana?

Jibu


Mtume Yohana ndiye aliyenakiri vitabu vitano vya Agano Jipya: Injili ya Yohana, barua fupi tatu zinazotambulika kwa anwani yake (1, 2, na 3 Yohana) na nakala la Ufunuo. Yohana alikuwa miongoni mwa "jamii ya karibu" ya Yesu na, kujumuishwa Petro na Yakobo, Yohana alipata naasi ya kipekee kuona majadiliano kati ya Yesu, Musa na Eliya mlimani alipobadilishwa (Matayo 17: 1-9). Umuhimu wake miongoni mwa thenashara ulikomaa alivyoendelea kukua na baada ya kusulubiwa, alikuwa "kizingiti" kwenye hekalu la Yerusalemu (Wagalatia 2: 9), akatoa huduma pamoja na Petro (Matendo 3: 1, 4:13, 8:14), na mwishowe akachukuliwa kizingani Patmos na Warumi, na hapo akapata maono kutoka kwa Bwana na akayanakiri katika Ufunuo.

Bila kutaabishwa na Yohana Mbatizaji, Mtume Yohana ni kakaye Yakobo, aliye mmoja wa wafuasi thenashara wa Kristu. Wote walichaguliwa na Kristu, "Boanerges," kumaanisha "watoto wa radi," na mumo tunajipatia mwanya kwa ubinadmu wa Yohana. Wote ndugu hao walijulikana kwa kumiliki kujitolea, moyo na shauku. Nyakati zake za kwanza na Kristu, Yohana alikuwa na mbio, bila kumakinika, maamuzi bila kujali na mkali. Tunampata kwenye Marko 9 kumkataza mtu kutoa mapepo kutumia anwani ya Kristu kwa maana hakuwa miongoni mwa wale thenashara. (Marko 9: 38-41). Yesu kwa upendo akamkanya, akinena hamna atakaye fukuza mapepo kwa anwani ya Kristu na baadaye kuongea maovu dhidi Yake. Luka 9: 51-55, tunapata mandugu wanaowania kuita moto kutoka juu kuwateketeza Wasamaria waliokaidi kumlaki Kristu. Pia, Kristu akawakanya kwa kutvumilia kwao na kupungukiwa na upendo thabiti kwa wasioamini. Juhudi za Yohana kwa sababu ya Kristu ziliathirika na matamanio ya kiasili, ilivyodhihirika katika kuomba {kupitia mamake} kuwa yeye na kakaye waketi kwa kushoto na kulia kwa Kristu katika utukufu wake, jambo ambalo lilishua rabsha miongoni mwa makaka na wafuasi wengine (Mathayo 20: 20-24; Marko 10: 35-41).

Hata kama matamshi haya ya ujana yaliyokosa mwelekeo mwafaka, Yohana akaongezeka miaka vizuri. Alingamua sababu ya kuwa na stahimili miongoni mwa waliotamani kuwa wakuu. Injili ya Yohana ndiyo tu inanakili Yesu akiosha wafuasi miguu. (Yohana 13: 1-16). Kitendo cha unyenyekevu cha Kristu kweli lilimgusa Yohana pakubwa. Hadi pale pa kusulubiwa, Yesu aliamini sana kijana huyo kuwa na ujasiri kubadilisha kumtunza mamake kwenda kwake, jukumu Yohana alilitenda bila msaha. Kutoka siku ile, Yohana alimtunza kama nina yake (Yohana 19: 25-27). Tamanio la Yohana la kupatiwa mtazamo wa kipekee kwenye utukufu lilitengeneza upenyo kwa kuhurumia na kujishusha iliyodhihirisha namna ya huduma yake kwenye uhai wa keshoye. Hata kama alisalia kuwa na nguvu na busara, kusudio lake lilikuwa na kunyenyekea aliyosoma miguuni pa Kristo.

Tumaini la Yohana kuwatendea wengine na kuumia kwa sababu ya Injili bila shaka ilimsaidia kuvumilia maisha yake ya hatimaye akiwa Patmos ambapo, kama ilivyo nakala za kihistoria, alikaa kizingani, akajitenga na wale aliowapenda, na akatendewa kinyama na ghadhabu. Kwenye kipengele cha kwanza kwenye Ufunuo, alichopata kutoka kwa Roho Mtakatifu kwa muda ule, Yohana alijitambulisha kuwa"ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu " (Ufunuo 1: 9). Alijifahamisha kuangalia zaidi ya kuteseka kwake dunia kwa malengo ya utukufu wa mbinguni unaongoja wanaovumilia kwa ukweli.

Yohana alijitolea kwa hakika kutangaza ukweli. Hamna mwingine Zaidi ya Kristu,alimiliki mengi ya kunena kuhusu ukweli. Furaha yake ilijionyesha kwa kutangaza ukweli kwa watu na kuwaangalia walivyoenenda kwa hiyo (3 Yohana 1: 4). Pingamizi lake kuu ni kwa wale walioasi ukweli na kuwapotosha wengine vile vile, na kama walikuwa wanaamini. (1 Yohana 2: 4). Azimio lake la upendo liliongoza mtazamo wake kwa kondoo walioathirika kulaghaiwa na walimu wa uongo, na kemeo lake kwao linasungumziwa kwa kina katika 1 Yohana. Hakuhitaji ufafanuzi kufahamu "makuani wasio wa kweli" na "wapinga-Kristo" wale waliokusudia kuzuia ukweli, na hata kueneza uongo. (1 Yohana 2:18, 26, 3: 7, 4: 1-7).

Mara hiyo, Yohana pia anatambulika "mfuasi wa upendo." Kwenye Injili yake yeye, anajitambua kuwa "aliyependwa na Kristu" (Yohana 13:23, 20: 2, 21: 7, 21:20). Anadhihirishwa kama anayeegemea kwenye kifua cha Yesu kwenye chajio cha hatima, na hata kuthibitisha kuwa alikuwa mdogo kwa wale thenashara. Kwenye waraka wake wa kwanza, Yohana ananakiri Mungu kuwa upendo na kupenda kwa wenzetu ni onyesho la upendo wa Mungu kwetu (1 Yohana 3; 4: 7-21). Waraka wake mfupi wa pili umejaa maonyesho yake ya upendo wa kweli kwa kutunza kwake. Anaandikia kundi la walioamini "ninaowapenda katika kweli" na kuwahimiza "kupendana" kwa kuishi kwa kutii torati za Kristu (2 Yohana 1: 1, 5-6). Yohana anawatambua wanaosoma kama "wapendwa" kwenye 1 Yohana na 3 Yohana.

Uhai wa Yohana hutumika kutujuza mambo mingi tunayoweza kuhusisha kwenye uhai wetu. Mwanzo, suluhu la ukweli inalazimu kusawasishwa na mapendo kwa waja. Kukosa haya, inaeza badilika kuwa makali na kuhukumu. Mbadala yake, mapenzi ya kweli yanayokosa uwezo kungamua kweli dhidi ya makosa inaweza kuwa legevu. Vile Yohana alivyosoma komaa,kama tutasema ukweli kwa mapendo, sisi, na tunaotangamana nao, "katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo"" (Waefeso 4:15).

Pili, nguvu na kutoogopa, usio sambaratishwa na neema na upendo, unaweza kubadilishwa kwa haraka na kiburi. Kuwa na ujasiri ni kitu mwafaka, ila kutokuwa na kunyenyekea, huenda ikawa ubinafsi, unaoweza kuleta kiburi na roho ya kutohusisha wengine. Hayo yatakapotokea, shuhudia kwetu rehema ya Bwana kutakuwa haifu, na wengi htazama ndani yetu kile wasichotaka kushuhudia. Jinsi ilivyo kwa Yohana, kama tutakuwa wakamilivu kwa ajili ya Yesu, mienendo yetu ndiyo itadhihirisha nia yetu ya ukweli, imani kwa wngine,na hamaki ya kutumikia na kuwakilisha Mungu wetu kwa kuonyesha uzuri wake na rehema.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tunafaa kujipatia nini kutoka kwa uhai wa mtume Yohana?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries