settings icon
share icon
Swali

Tunajifunza yapi kutoka kwa uhai wa Yohana Mbatizaji?

Jibu


Hata kama anwani yake inaashiria aliwabatiza waja (alichotenda), uhai wa Yohana ulimwenguni ulizidi kubatiza tu. Maisha ya uzimani wa Yohana ulijazwa na kujitolea na kujipeana kwa Yesu Kristo na ufalme Wake. Sauti ya Yohana ikawa "sauti ya mtu aliaye nyikani" (Yohana 1:23) jinsi alivyoelezea kurejea kwa Masihi kwa waja waliomwazia Mwokozi. Ndiye alikuwa mwanzilishi wa uinjilisti wa kisasa alioutangaza bila aibu habari njema ya Yesu Kristo. Alikuwa mja aliyekuwa na imani thabiti na kielelezo kwetu sisi tunaoweza kuambiana imani tuliyonayo na wenzetu.

Karibu kila mja, aliyeamini na asiyeamini kwa pamoja walipata kusikia habari za Yohana Mbatizaji. Ni mmoja wa walio wa maana na wa kutambulika kwenye maandiko. Pale Yohana alitambulika kuwa "Mbatizaji," kwa kweli ndiye nabii wa kwanza kuitwa na Mungu tangia Malaki karibia miaka 400 iliyotangulia. Kukuja kwa Yohana kulitabiriwa zaidi ya miaka 700 hapo mwanzo na nabii mwingine: "Sauti ya mtu aliaye:" itengenezeni nyikani njia ya Bwana, nyoosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu. Kila bonde litainuliwa na kila mlima na kilima kitashushwa, palipopotoka patakuwa pamenyoka na palipoparuza patasawasishwa; na utukufu wa Bwana utaunuliwa na wote wenye mwili watauona pamoja kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena haya "(Isaya 40: 3-5). Kipengele hiki kinatuonyesha mipango ya Mungu vile Bwana alimpendelea kuwa balozi kueneza kurejea kwake.

Kuzaliwa kwa Yohana kulikuwa kwa miujiza. Alipatikana na wazazi wakongwe waliokuwa hawajapata uwezo wa kupata watoto (Luka 1: 7). Ndipo Malaika Gabrieli alimjuza Zekaria, kuhani wa Kialawi, kuwa angepata mtoto –jambo Zakaria alilopata kwa kutoamini (mistari 8-18). Gabrieli akanena haya kuhusu Yohana: "Yeye atakuwa mkuu mbele za Bwana. Yeye. . . atajazwa na Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye. Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao. Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya,. . . kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa"(mistari 15-17). Kama lilivyokweli neno la Bwana, bibi ya Zekaria, Elizabeth, akamzaa Yohana. Kwenye sherehe ya kutahiriwa, Zakaria akaongea kuhusu mtoto wake, "Nawe mtoto utaitwa nabii wake Aliye Juu; kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia "(mstari wa 76).

Yohana alifananishwa na Yesu, sababu nina zao walikuwa wanahusiana kijamii (Luka 1:36). Aidha, malaika Gabrieli alipomwarifu Maria kuwa angepata Yesu, alifanya ivyo hata kuhusu Yohana. Maria wakati alikuwa amembeba Kristu tumboni mwake, alimtembelea Elizabeti, na Yohana akageuka tumboni mwa mama yake kwa furaha ya kusikia sauti ya Maria (Luka 1: 39-45).

Ilivyo kwa mja mkomavu Yohana aliishi uhai wa taabu milimani mwa Yudea, katikati mwa mji wa Yerusalemu na Bahari ya Mauti. Mavazi yake yalitokana na singa za ngamia na mshipi wa ngozi kiunoni sawia tu na nabii wa kawaida. Lishe lake lilikuwa si ngumu nzige na asali ya mwitu (Mathayo 3: 4). Yohana aliishi uhai wa kirahisi maana alizingatia tu kazi ya ufalme uliokuwa umemtangulia.

Huduma ya Yohana Mbatizaji ilienea kwa kujulikana sana, inavyonakiliwa kwa Mathayo 3: 5-6: "Ndipo walipomwendea Yerusalemu na Uyahudi wote na nchi zote za kando kando ya Yordani. naye akawabatiza katika mto wa Yordani . "Kubatizwa na Yohana ni kukiri makosa na kutubu-iliyokuwa, hata ivyo, namna mwafaka ya kujitayarisha kwa Mkombozi anayekuja. Kuungama kunakohusishwa na ulihifadhi walio haki dhidi ya maji, maana hawakuona wakiwa wadhambi. Kwa walio bila dhambi, Yohana alikuwa na kemeo kali akiwatambua, "wazao wa nyoka" na kuwajuza wasitegemee kizazi chao cha Kiyahudi ndipo wapate kuokoka,ila kwa kukiri,"kuzaa matunda kutokana na kufanya kuungama" (Mathayo 3: 7- 10). Waja wa enzi hizo hawakutambua wakuu, wa dini, ama wengine, kwa ajili ile kwa kuogopa kuadhibiwa. Ila imani ya Yohana ikamfanya kutokuwa na woga mbele ya wapinzani.

Watu wengi huenda walichukulia kuwa ndiye Masihi, kwa maana ya mtazamo wa jumla wa Yohana Mbatizaji ukawa kuwa alikuwa nabii wa Mungu (Mathayo 14: 5). Hii hikuwa azimio lake kwa sababu alikuwa ameona fika aliloitiwa kutenda. Kwenye Yohana 3:28 Yohana ananena, "Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, 'Mimi siye Kristo bali nimetumwa mbele yake.'" Yohana aliwapa onyo wafuasi wake kuwa chenye waliona na kusikia kutoka kwake ni mwanzo tu miujiza ambayo ingekuja kwa mfano wa Yesu Kristo. Yohana alikuwa tu mtumwa aliyekuja mbele kueneza ukweli na alitumwa na Mungu. Ujumbe wake ulikuwa mwepesi na rahisi: "Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia" (Mathayo 3: 2). Alifahamu kuwa, pale tu Yesu aonekanapo mahali pale, majukumu ya Yohana yangefika tamati. Kwa kujitolea kwake kutengeneza njia ya Yesu, akinena, "Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua" (Yohana 3:30).

Pengine hamna kielelezo thabiti cha kunyenyekea kuzidikinachodhihirika miongoni mwa Yesu na Yohana kwenye Mathayo 3: 13-15. Yesu aliwasili akitoka Galilaya ili apate kubatizwa na Yohana kwenye Mto Yordani. Yohana kwa ukweli aligundua kuwa Mwana wa Mungu asiyejua dhambi hakuhitaji ubatizo wa toba na kuwa hakustahili kumzamisha Mwokozi wake mwenyewe majini. Ila Kristu akamjibu yaliyomkwaza kwa kuagiza ubatizo "ili sisi tupate kuwa haki yote," kumaanisha alikuwa anajifanya kujulikana Mwenyewe na wafanya dhambi ili kuwanyakulia wokovu. (2 Wakorintho 5:21). Yohana aliitikia na kukubali kubatiza Yesu kwa unyenyekevu. (Mathayo 3: 13-15). Yesu alipopanda kutoka majini, "na tazama mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama ua,akija juu yake na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye "(mistari 16-17).

Mfalme Herode akamuweka Yohana Mbatizaji gerezani baadaye. Herode alikuwa amemchumbia bibi ya kakake, Philip. Yohana bila kuogopa alikemea ndoa ile, na hilo likamkasirisha Herodias, bibi mgeni wa Herode (Luka 3: 19-20; Marko 6: 17-20). Bado akiwa kifungoni, Yohana alipata habari kuhusu yale Kristu alikuwa akitenda. Kwa kilichooneka kwamba ndoto, Yohana akawatuma wafuasi wake kwa Yesu kuthibitisha kama ikiwa kweli yeye ndiye Masihi. Yesu akawajibu kwa kuwaarifu wanaume kumwelezea kile walichokiona na kusikia-unabii ulikuwa unakamilishwa. Yesu hakuwahi kemea, bali, alipeana hakikisho kuwa ndiye Mwokozi aliyeahidiwa (Mathayo 11: 2-6; Luka 7: 18-23). Yesu baadaye akazungumzia umati kuhusu Yohana, akinena ndiye nabii aliyesemewa angetangulia kabla ya Masihi (Mathayo 11:10, Luka 7:27, angalia Malaki 3: 1). Yesu kisha akanena, "amini nawaambieni, hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji, walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni" (Mathayo 11:11; Luka 7:28).

Kama vile uhai wake, huduma ya Yohana Mbatizaji, ilifika hatima ya haraka chini ya mtawala Herode. Kwa jambo la kisasi lisilotajika, Herodiasi akawa na njama na binti yake kupata Yohana kuangamizwa. Binti ya Herodia alinengua kwa ajili ya Herode na walioketi naye kwa ajili ya chajio usiku mmoja, na Herode akafurahishwa Zaidi akamwongelesha, "niombe lolote utakalo,nitakupa" (Marko 6:22).Binti akashauriana na mama yake kabla ya kuitikia kuwa aliitaji kichwa cha Yohana Mbatizaji kwa kombe (mstari wa 25). Herode alimwogopa Yohana, "akijua kuwa ni mtu wa haki na mtakatifu" (mstari wa 20), na akawa na pingamizi kumuua nabii, ila alikuwa ametoa kiapo chake kumpati binti lolote aliloitisha. Kwa maana Yohana alikuwa bado ametiwa mbaroni kwa gereza, ilikuwa si jukumu ngumu kutuma mtu kukata iyo kichwa cha Yohana, jambo lililotendeka hivyo (Marko 6: 27-28). Hii ilikuwa jambo la kuhuzunisha na hatima ya aibu ya mtu aliye wa imani hivyo.

Kuna masomo kadhaa ya kusoma kutoka kwa uhai wa Yohana Mbatizaji. Mosi ni kuwa kujitolea na kwa moyo wote kumwamini Yesu Kristo si vigumu. Yohana alingamua kuwa Masihi angekuja. Haya aliyaamini kwa dhati na akatumia muda wake "kutengeneza njia kwa kurejea kwa Kristu (Mathayo 11:10). Ila njia hikuwa nyepesi kutayarisha. Kila kujao alipata wapingamizi waliokosa kuchangia katika kurejea kwa Masihi. Kwa mahojiano makali kutoka kwa Mafarisayo, Yohana aliwaajuza aliyoamini: "Mimi nabatiza kwa maji... katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi. ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake "(Yohana 1: 26-27). Yohana alikuwa na imani kwa Kristo, na kuamini kwake kukamweka thabiti kwa njia zake hadi alipoona Kristu akirejea, "Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!" (Yohana 1:29).tunafaa kuwa na hii imani thabiti kama waumini

Ikiwa si rahisi kufahamu aliyokuwa akihisi Yohana akiwa angali kifungoni, hata ivyo akaonekana kuwa na taabu. Ila Yohana akatuma waraka kwa kristu kwa juhudi za kupata kweli. Kama ka Waumini tunafaa kuwa na msimamo wetu kujaribiwa, na tusiweze kuyumbisha imani yetu, au, kama Yohana, kushikilia Kristu, tutafute ukweli na kusimama thabiti kwenye imani yetu hadi tamati.

Chochote kitakachowezekana, uhai wa Yohana ni kielelezo chenye tunafaa kutumia katika kupata uhai Kikristo na kuitwa kwetu kwa huduma. Yohana kwa uhai wake aliutumia kuwaleta wengine kwa Yesu Kristo; alisalia kuwa makini kwa lengo alilopata kutoka kwa Mungu. Yohana vile vile alifahamu manufaa ya kuungama dhambi ili kuishi uhai ulio kamili na haki. Pia alikuwa si mwoga kunena ukweli, na kama mtumishi wa Mungu, hata ilipomaanisha kuita waja kama Herode na Mafarisayo kwa hulka zao za madhara.

Yohana alionwa bora kwenye huduma ya kiteule, ila sisi, kadhalika, wanaitwa kushiriki ukweli wa Kristu na wengine (Mathayo 28: 18-20; Yohana 13: 34-35; 1 Petro 3:15; 2 Wakorintho 5:16 -21). Tunafaa kufuata kielelezo cha imani na uaminifu wa kweli kwa Mungu vile tutaishi na kueneza ukweli wake kwa namna yoyote ile uhai tuliopewa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tunajifunza yapi kutoka kwa uhai wa Yohana Mbatizaji?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries