settings icon
share icon
Swali

Tutajifunza yapi kutoka kwa uhai wa Yeremia?

Jibu


Yeremia nabii aliishi kwenye nyakati za hatima za nchi ya Israeli la iliyosambaratika. Hakika alikuwa nabii wa mwisho aliyetumwa na Bwana kutangaza injili katika taia la kusini, lililokuwa na makabila ya Yuda na Benyamini. Bwana mara mingi aliwaonya Waisraeli kukoma hulka zao za uzinzi, ila hawakutia maanani, hivyo akasambaratisha makabila yote 12, akituma 10 kaskazini walipotekwa mateka chini ya Waashiri. Basi Bwana akamwamrisha Yeremia kuwapa Wayuda onyo la mwisho kama hajawafurusha kutoka taifa, awaangamize nchi na kuwafurusha kuelekea matekani kwa utawala usiomjua Mungu wa Babeli. Yeremia, aliyemwaminifu, aliyemtii Bwana,alitumiwa kuamrisha Waisraeli kuwa, kwa makosa yao wasiyoungama, Bwana wao aliwageuka na alipanga kuwaondoa kutoka nchi kwenye mikono ya taifa la waasi.

Yeremia alikuwa karibu miaka 17 alipoitwa na Mungu, bila shaka, alikuwa na vita vya ndani kuhusu hatima ya taifa lake, na akawasihi kusikiliza. Yeye anatambulika kuwa "nabii anayeomboleza," kwa maana alilia machozi ya kuhuzunika, na si kwa maana alifahamu kilichokuwa karibu kutendeka, bali kwa maana bila kufahamu jinsi alivyojikaza, taia halikumsikiliza. Zaidi, hakufarijika kama mwanadamu. Bwana alimwonya dhidi ya kupata mchumba wala kuwa na wana (Yeremia 16: 2), na wandani wake walimtenga. Hivyo, kujumuisha na gurudumu la hukumu lililokaripia, lazima alijihisi mpweke sana. Bwana alifahamu kuwa hii ilikuwa mwendo mwafaka kwa Yeremia, kwa maana hakukoma kumweleza mambo yangekuwa magumu muda usio mrefu, na watoto wachanga, vijana, na watu wazima waliofariki "vifo vya uchungu", miili yao isiweze kuzikwa, na nyama zao zilisambaratishwa na ndege (Yeremia 16: 3-4).

Kawaida, taifa la Israeli waligeuka kuwa wagumu sana kwa sababu ya madhara ya dhambi kuwa hata hawakuwwa na imani na Mungu tena, hata kumuogopa tena. Yeremia akatangaza injili miaka 40, na mara si moja aligundua mafanikio ama kurahisisha kwa nyoyo na akili ya wakaidi, na waabudu miungu. Manabii mbadala wa Israeli walitambua mafanikio fulani, angaa kwa wakati mchache, ila si Yeremia. Alinenea ukuta wa mawe; ingawa, maneno yake hayakuenda hasara. Walifananishwa lulu kutupiwa nguruwe, kadhalika waliwashika wote waliowasikia na kukaidi kusikia waliyoyasema.

Yeremia alingangana kuahamisha watu kutafakari tatizo lao lilikuwa kukosa kuamini, na imani kwa Mungu, kuongeza na kukosa kuogopa iliyowafanya kukchukulia Mungu kimsaa. Si vigumu kudanganyika kuingia katika kuhisi kutokuwa salama, hasa pale hatumhusishi Mungu. Nchi ya Israeli, ilivyo mataifa mengi enzi hizi, waliasi kumtanguliza Mungu,na wakapata mbadala Yake na sanamu, ambazo hazingewafanya kuwa na hisia za kukosa wala kuwahukumu na makosa yao. Bwana aliwakomboa taifa lake kutoka utumwani Misri, akatenda mifano mingi wakishuhudia, na hata kusambaratisha maji baharini kwa ajili yao. Hata baada ya matendo hayo ya miujiza, walirudia njia zao potovu walipojifunza kule Misri, zaidi kufanya ahadi kwa malkia wa mbinguni wa uongo zaidi ya kutenda mila na ibada nyingine zilizokuwa pamoja na za wa Misri na dini. Bwana baadaye aliwageuza kwa uabudu miungu, wakinena," basi, zithibitisheni nadhiri zenu, zitimizeni nadhiri zenu"Yeremia 44:25).

Yeremia akapoteza imani. Akajitosa kwenye ile hali ambako wafuasi wanaweza kuwa wamekwama walipojihisi kuwa juhudi zao zilikuwa hazitoi tofauti na muda unaisha. Yeremia kihisia alichoka hadi kufikia mahali pa kumshuku Bwana (Yeremia 15:18), ila Bwana hakuwa amemalizana naye. Yeremia 15:19 inanakiri funzo kwa kila aaminiye kutafakari nyakati zile anahisi mpweke, bila wa maana na imani inayumbayumba: "Kwa sababu hiyo Bwana asema hivi: 'Ukirudi ndipo mimi nitakapokurejeza, upate kusimama mbele zangu nawe ukitoa kilicho cha thamani katika kilicho kibovu utakuwa kama kinywa change; nao watakurudia wewe bali hutawarudia wao."Bwana alikuwa akisemea Yeremia, rudi kwangu, nami nitakurejeshea raha ya wokovu wako. Haya ni sawia na yale yaliyonukuliwa na Daudi pale alipokiri makosa yake na Bathsheba (Zaburi 51:12).

Tunayojifunza kutoka kwa uhai Yeremia ni faraja ya kufahamu kuwa, vile tu kwa kila aaminiye, hata manabii wakuu wa Mungu wangepata kukataliwa, mawazo, na kupoteza tumaini katika kumfuata Mungu. Hii ni kawaida katika ukuaji wa kiroho, kwa maana nafsi zetu za kithambi dhidi ya asili yetu ya kisasa, kile kilichozaliwa kutoka kwa Roho wa Mungu, kama ilivyo kwa Wagalatia 5:17: "Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana hata hamwezi kufanya mnayotaka. "Ila alivyogundua tunangamua kuwa uaminifu wa Mungu wetu hauna hatima; hata tunapokosa imani naye, Yeye anabaki thabiti (2 Timotheo 2:13).

Yeremia alipata jukumu la kuokoa kisichojulikana, taarifa isiyopendeza kwa Israeli, moja iliyomletea matatizo akilini mwake, na hata kumletea kutengwa na jamii yake. Bwana anena kuwa ukweli wake huchukuliwa kuwa"usiomaana" kwa wapotovu, ila kwa watumwa ni maneno ya uzima (1 Wakorintho 1:18). Anena kuwa muda utafika pale umati hautashikilia kweli (2 Timotheo 4: 3-4). Walioko Israeli wakati wa Yeremia hawangetaka kutii yale aliyowaambia, na onyo l kila mara la kuangamizwa liliwakasirisha. Hii ni sawana dunia ya sasa, ilivyo walioamini wanaomfuata Mungu kwa uelekezi anatoa onyo kwa wapotovuna wanaoangamia kwa hukumu inayokuja (Ufunuo 3:10). Hata nkama wengi hawasikilizi, tunafaa kuvumilia katika kusema ukweli ili kunyakua kadhaa kutoka kwa hukumu inayotisha itakayokuja.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tutajifunza yapi kutoka kwa uhai wa Yeremia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries