settings icon
share icon
Swali

Je, tunapaswa kujifunza nini kutokana na maisha ya Yakobo?

Jibu


Maisha ya Yakobo yalianza kwa mapambano. Walikuwa mapacha naye Esau ndani ya tumbo. Yakobo aling'ang'ania nafasi na akazaliwa huku akishika kisigino cha ndugu yake. Jina la Yakobo linatafsiriwa kama "anayedanganya" (Mwanzo 25:26). Wakati mama yake, Rebekah, aliuliza Mungu kilichokuwa kinatendeka wakati wa ujauzito, Mungu alimwambia kuwa kulikuwa na mataifa mawili ndani ya tumbo lake ambayeo yangegawanyika. Mmoja angeweza kuwa mwenye nguvu zaidi kuliko mwingine, mzee angetumikia mdogo (Mwanzo 25:23).

Yakobo na Esau walikua pamoja huku wakiishi maisha ya uhamaji. Esau akawa mwindaji mzuri na aliyependa kuwa nyikani wakati Yakobo "alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa hemani." (Mwanzo 25:27). Esau, ambaye alikuwa mwindaji, alipendwa na baba yake. Basi akampenda Esau, kwa sababu alikula mawindo yake aliyoleta nyumbani, na Rebeka akampenda Yakobo.(Mwanzo 25:28). Upendeleo huu wenye kuangamiza ulifuata familia katika kizazi kilichofuata, hasa kwa Yusufu mwana wa Yakobo. Upendeleo huo ni sawa ule wa Yakobo kwa Yusufu. Ulifanya ndugu zake kuwa na kinyongo na karibu kugharimu Yusufu maisha yake.

Isaka alipokuwa mzee na macho yake kufifia, alifikiri alikuwa karibu kufa chake na akafanya mipangilio na Esau kumpa baraka za mtoto wa kwanza (Mwanzo 27: 1-4). Rebeka aliposikia hayo, alipanga mpango wa kumdanganya Isaka kumbariki Yakobo badala yake. Hivyo basi, Yakobo alipata baraka za baba yake badala ya Esau. Basi Esau aliweka nadhiri kuwa atamwua Yakobo mara tu wakati wa maombolezo ya kifo cha baba yake yatakapokamilika (Mwanzo 27:41). Hata hivyo, baba yake hakufa kwa takribani miaka ishirini nyingine (Mwanzo 35: 27-29).

Hata hivyo, Rebeka alijua mpango wa Esau na akamwonya Yakobo. Rebeka pia akamwambia Isaka kwamba Yakobo ajitafutie mke kutoka kwa watu wake, hivyo Isaka akamtuma Yakobo kwa mjomba wake Labani aliyeishi nyumbani kwa baba zao Harani (Mwanzo 27:43). Wakati wa safari ya Yakobo, alikuwa na ndoto kuhusu ngazi mbinguni na Mungu juu yake na malaika wakipaa na kushuka. Twasira hii inaonyeshwa katika maneno ya Yesu kwa mwanafunzi wake Nathanaeli (Yohana 1:51). Mungu alimpa Yakobo uhakikisho wa uwepo wake na alirejelea ahadi yake kwa Ibrahimu (Mwanzo 28: 13-15). Matokeo ya tukio hili, Yakobo alibadilisha jina la mahali hapo kuwa "Betheli," maana yake ni "nyumba ya Mungu," na akaapa kumtumikia Mungu.

Baada ya Yakobo kutukia katika Harani, Labani alimlipa kwa ajili ya kazi aliyokuwa akifanya ya kuchunga mifugo wake. Yakobo alijitolea kumtumikia Labani kwa miaka saba ili kumapata Raheli, binti wa Labani, ambaye alimpenda sana. Hata hivyo, Yakobo aligundua kwamba mjomba wake Labani alikuwa mdanganyifu sana kama yeye tu. Usiku kabla ya siku ya harusi ya Yakobo, Labani alibadilisha binti yake mkubwa, Lea, kwa Raheli (Mwanzo 29: 23-25). Hata hivyo, Labani alikubali kumpa Yakobo Raheli pia, ikiwa Yakobo angemaliza wiki ya harusi akiwa na Leah kabla ya kumchukua Raheli kuwa mkewe, na kisha kumfanyia kazi kwa miaka nyingine saba. Yakobo alikubali mpango huu. Wanawakehao wawili walibakia kuwa wake wa Yakobo, lakini Yakobo alimpenda Raheli kuliko Leah (Mwanzo 29:30), chanzo cha mgogoro wa familia.

Wakati Raheli alipokuwa tasa, Lea alimzaa mwana wa kwanza wa Yakobo, Reubeni. Kisha akafuatiwa kuzaliwa kwa wana kumi na mmoja zaidi kutoka kwa Lea, Rachel, na watumishi wao wawili. Wana hawa wakawa waanzilishi wa kabila kumi na mbili za Israeli. Baada ya kuzaliwa kwa Yusufu, mtoto wa kwanza wa Raheli na kumi na moja ya Yakobo, Yakobo alimwomba Labani kumrudisha nyumbani kwake. Labani alimwomba Yakobo kubaki, akamwambia aitishe mshahara wake aliotaka. Yakobo aliomba tu kondoo mbuzi na mbuzi waliokuwa na madoadoa na marakara kutoka kwa mifugo yote ya Labani aliyochunga ili kuifanya mifugo yake mwenyewe. Haijulikani jinsi au kwa nini ilifanyika, lakini Yakobo aliweka fito zilizokuwa na marakaraka mbele ya mifugo walipokuwa wakitunga mimba, na ilisababisha kuzaa kwa Wanyama waliokuwa na madoadoa na marakaraka ambao aliwatenga kuwa wake. Yakobo alifanya hivyo tu na wanyama wenye nguvu ili mifugo wake wawe wenye nguvu wakati Labani alikuwa na mifugo dhaifu (Mwanzo 30: 31-43). Yakobo aligundua kwamba mwana wa Labani hakumtazama vyema, alikuwa amebadilika. Ndipo Mungu alimwamuru Yakobo kurudi nchi ya baba yake akiwa na ahadi yake, "Na nitakuwa pamoja nawe" (Mwanzo 31: 3). Yakobo aliondoka Harani pamoja na wake wake na watoto wake na mifugo yote mingi aliyokusanya. Labani alipogundua kwamba Yakobo alitoweka, akamfuata. Lakini Mungu alimjia Labani katika ndoto na kumwambia "Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari." (Mwanzo 31:24). Labani alimwuliza Yakobo kwa nini aliondoka kwa siri na alizungumza juu ya nguvu zake kumdhuru Yakobo isipokuwa kwa onyo la Mungu. Pia alimshtaki Yakobo kwa kuiba sanamu zake za nyumbani. Akiendeleza urithi wa udanganyifu, Rachel ambaye alikuwa amechukua sanamu bila kujulikana na Yakobo, alizificha kutoka kwa macho ya baba yake wakati wa kuzitafuta. Labani na Yakobo hatimaye waliachana baada ya kuapa kiapo kutoingilia ardhi ya mtu mwingine.

Baada yake, Yakobo alipokuja kukabiliana na nduguye, Esau. Ingawa miaka ishirini ilipita tangu kuonana, kumbukumbu ya tishio la Esau kumwua Yakobo hakumtoka akilini (Mwanzo 32:11). Yakobo akatuma wajumbe mbele yake na zawadi, akawaambia waambie Esau kwamba atafuata baadaye. Wajumbe walirudi kwa Yakobo wakamwambia Esau alikuwa anakuja kumlaki pamoja na watu mia nne. Yakobo aliogopa kwamba Esau alikuwa akija kumwangamiza, basi akagawanya familia yake katika makundi mawili, akiwa na matumaini angalau kundi moja litaponea. Yakobo aliomba Mungu amwokoe, akimkumbusha Mungu kwamba alimtuma Yakobo kurudi katika nchi ya Abrahamu na ameahidi kumfanya afanikiwe na wazao wake wengi (Mwanzo 32: 9-12). Yakobo alichagua zawadi zaidi kwa Esau, ambazo zilipelekwa na watumishi wake, akitumaini kumtuliza moyo Esau. Usiku huo aliwatuma wake wake na wana wake mbali naye. Alipokuwa peke yake katikati ya usiku na akiogopea maisha yake, Yakobo alipigana na mtu ambaye baadaye aligundua kuwa alikuwa Mungu (Mwanzo 32: 22-31). Mtu huyo alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja alipokuwa akishindana naye. Yakobo bado alikataa kumruhusu mtu huyo aende. Aliomba baraka na akaambiwa, "Jina lako hautaitwa tena Yakobo, ila Israeli, kwa sababu umeshindana na Mungu na wanadamu nawe umeshinda" (Mwanzo 32:28). Yakobo akamwuliza jina lake na kisha akaelewa kuwa alikuwa Mungu. Yakobo aliita mahali hapo Penueli, akifahamu kwamba alikuwa amemwona Mungu uso kwa uso na bado Mungu aliokoa nafsi yake. Mechi hii ya kukabiliana na pia mabadiliko ya jina ya ilikuwa mwanzo mpya kwa Yakobo. .

Kuungana tena na Esau haikuwa mashambulizi aliyoyaogopa: "Esau akaja mbio kumlaki na kumkumbatia Yakobo na kumwangukia shingoni yake na kumbusu, nao wakalia" (Mwanzo 33: 4). Esau alijitolea ya kuandamana na Yakobo mahali mpaka walikuwa wanaenda lakini Yakobo alikataa huku akisema kwamba familia yake ni kubwa. Yakobo pia alikata pendekezo la Esau la kuwacha baadhi ya wanaume wake pamoja na kikundi chake. Inaonekana kwamba Yakobo hakumwamini ndugu yake Esau kikamilifu, kwa hivyo, badala ya kukutana na Esau huko Seiri, Yakobo alichukua familia yake njia nyingine ambako hatimaye walinunua ardhi na kukaa katika El-Elohe-Israeli au "Mungu wa Israeli ni mwenye nguvu." Ingawa Yakobo alikuwa amepewa jina jipya, Yakobo ambaye alikuwa mdanganyifu alikuwa bado alikuwa na tahadhari kwa wengine ambao wangeweza kuwa wanajaribu kumlaghai. Tunapata kuona kwamba mawazo ya wale wanaopanga kulaghai daima wanashuku kusudi la wengine na hawawezi kutulia kabisa

Mwanzo 34 ina kumbukumbu ya ubakaji wa Dina, binti wa pekee wa Yakobo, na pia inaelezea jinsi ndugu zake Simeoni na Lawi walilipiza kisasi kwa jamii nzima ya mbakaji huyo. Mara nyingine tena, tunaona jinsi udanganyifu wa wazazi ulipitishwa kwa watoto walipowashinda adui yao kwa njia ya udanganyifu. Yakobo alikasiririka na wanawe na kwa kumtii mwongozo wa Mungu, alihamisha familia yake kurudi Betheli (Mwanzo 35: 1) ambapo Mungu alimtokea Yakobo na kuthibitisha baraka yake (Mwanzo 35: 9-13). Katika mkutano wa Mungu na Yakobo, alipokea ahadi ya kwamba wafalme na mataifa mengi watatoka kwake na kwamba nchi ambayo Mungu aliwaahidi babu zake itakuwa urithi wake (Mwanzo 35: 11-12).

Yakobo na familia yake baadaye wakahamia kutoka Betheli hadi Ederi. Walipokuwa njiani, Raheli alimzaa mwanawe wa pili Benyamini, mwana wa kumi na wawili wa Yakobo. Raheli akafa pindi alipojifungua. Yakobo aliungana tena na baba yake, Isaka, huko Mamre. Baba yake alipopokufa, Yakobo na Esau walimzika.

Yakobo pia alikuwa na upendeleo kama vile mama yake. Raheli alikuwa mke wake aliyependa sana, na pia alipenda sana wana wake-Yosefu na Benyamini. Kwa kweli, Yusufu alipendwa sana hadi ndugu zake wakawa na wivu na kumwuza katika utumwa. Lakini Mungu alikuwa pamoja na Yusufu, na hatimaye alifanikiwa huko Misri na akaokoa familia yake pamoja na Yakobo kutoka kwa makali ya njaa. Yakobo alikufia Misri na kwa ombi la Yusufu akapakwadawa asioze (Mwanzo 49: 29-50: 3). Yusufu na ndugu zake walipeleka mwili wa Yakobo Kanaani ili kuzikwa pamoja na Abrahamu, Sara, Isaka, Rebeka, na Lea. Kabla ya kifo chake, Yakobo alikuwa amewabariki wana wake kumi na wawili na akaomba kuzikwa ndani ya pango ambalo Ibrahimu alinunuliwa kwa mazishi. Yakobo pia alibariki wana wawili wa Yusufu, huku akitoa baraka ya kufungua mimba kwa mwana mdogo. Tofauti na baba yake ambaye alikuwa amedanganywa katika kutoa baraka ya kufungia mimba kwa Yakobo, Yakobo alikusudia kutoa baraka isiyo ya kawaida.

Kuna ufanani wa kushangaza katika maisha ya Abrahamu, Isaka, na Yakobo ni. Katika hadithi zao tunaona umuhimu wa familia na ushawishi wa mfano. Mada kama udanganyifu, upendeleo, ugomvi wa familia, baraka zisizotarajiwa, upatanisho, na imani inaonekana katika hadithi hizi. Zaidi, tunaona kwamba Mungu ni mwaminifu kwa ahadi zake. Yeye anachagua kukamilisha madhumuni ya ufalme wake kupitia watu wenye dhambi ambao wanakubali kumwamini. Anaweza kuwafanya wapya watu hao wenye dhambi -kumpa Abramu jina lake Abrahamu, Yakobo jina lake Israeli, na kuwafanya viumbe wapya wale wanaoamini katika Yesu Kristo (2 Wakorintho 5:17). Ingawa mwelekeo wetu wa dhambi bado unaweza kutukera, katika Kristo tunapata msamaha wa dhambi zetu na nguvu za kushinda. Tunakaribishwa kushiriki katika kazi ya Mungu duniani. Tuna majina mapya na tunaweza kuamini ahadi za Mungu ambaye anajidhihirisha kuwa mwaminifu kila wakati.

Jina la Yakobo, "mdanganyifu," linadhibitishwa katika maisha Yakobo. Lakini pia alikuwa Israeli, ambaye Mungu alifanya ahadi kwake na aliendelea kuwa mwaminifu kwake. Mungu alimtokea Yakobo, na Yakobo aliamini ahadi za Mungu. Licha ya makosa ya Yakobo, Mungu alimchagua awe kiongozi wa taifa kubwa ambalo linashiriki jina lake hadi leo. Lakini kwa hili, haiwezekani kwamba tutajua mengi juu ya Yakobo, ambaye anaonekana kuwa katikati ya matukio wakati wahusika muhimu ni wale walio karibu naye. Hakuna hekima kubwa au ujasiri katika maisha ya Yakobo ambayo tunaweza kuzungumzia, na tunamwona kama chombo kidogo cha Mungu. Ikiwa tunajaribiwa kufikiria hivyo, kwa sababu hatujatambuliwa katika kufanya matendo makuu kwa ajili ya Mungu, kwamba hatuna umuhimu kwake, basi tunapaswa kuzingatia maisha ya Yakobo na kujua kwamba, licha ya kushindwa kwetu, Mungu anaweza pia kututumia katika mpango Wake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, tunapaswa kujifunza nini kutokana na maisha ya Yakobo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries