settings icon
share icon
Swali

Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Yakobo nduguye Yesu?

Jibu


Yakobo alikuwa mwana wa Mariamu na Yusefu na hivyo kuwa ndugu wa kambo wa Yesu na alikuwa kakaye Yusefu, Simoni, Yuda, na dada zao (Mathayo 13:55). Katika Injili, Yakobo anatajwa mara chache sana, lakini kwa wakati huo hakuelewa huduma ya Yesu kamili na hakuwa ameamini (Yohana 7: 2-5). Yakobo alikuwa mmoja wa mashahidi wa kwanza wa ufufuo wa Yesu (1 Wakorintho 15: 7). Kisha aliishi Yerusalemu na kuwa sehemu ya kundi la waumini waliossli katika chumba cha juu (Matendo 1:14). Kutoka wakati huo na kuendelea, ushawishi wa Yakobo ndani ya kanisa la Yerusalemu ulianza kuongezeka.

Yakobo bado alikuwa Yerusalemu wakati Saulo aliyeokoka hivi karibuni alipowaziri na kukutana naye pamoja na Petro (Wagalatia 1:19). Miaka michache baadaye, wakati Petro alitoroka gerezani, alimwambia Yakobo kuhusu muujiza wake wa kutoroka (Mdo. 12:17). Wakati Baraza la Yerusalemu litakutana, Yakobo ndiye mwenyekiti (Matendo 15: 13-21). Yeye pia ni mzee wa kanisa, aliyeitwa "nguzo kuu" katika Wagalatia 2: 9. Baadaye, Yakobo anaongoza mkutano mwingine tena huko Yerusalemu, wakati huu ni baada ya safari ya tatu ya umisionari ya Paulo. Inaaminika kwamba Yakobo aliuawa mwaka AD 62, ingawa hakuna rekodi ya kibiblia ya kifo chake.

Yakobo ndiye mwandishi wa barua ya Yakobo, ambayo aliiandika kati yam waka wa AD 50 na AD 60. Yakobo anajijitambulisha mwenyewe kwa jina hilo lakini anajielezea mwenyewe kama "mtumwa wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo" (Yakobo 1: 1). Barua yake inaangazia zaidi maadili ya Kikristo kuliko teolojia ya Kikristo. Mada yake ni utekelezaji wa imani-ushahidi wa nje wa uongofu wa ndani.

Utafiti wa maisha ya Yakobo hutoa masomo muhimu kwetu. Uongofu wake unatoa ushuhuda wa nguvu sana ambao ulitokana na kushuhudia ufufuo wa Yesu: Yakobo aligeukia kutoka kuwa mpinzani na kuwa kiongozi katika kanisa kulingana na mkutano wake na Kristo aliyefufuka. Usemi wa Yakobo katika Halmashauri ya Yerusalemu katika Matendo 15: 14-21 inaonesha kutegemea kwake katika maandiko, nia yake ya kuwe na amani katika kanisa, msisitizo wake juu neema badala ya sheria, na kujali kwake Waumini Mataifa, ingawa yeye mwenyewe alihudumia Wakristo Wayahudi peke yake. Pia la mhimu kutambua ni unyenyekevu wake Yakobo – haikuwai kutumia nafasi yake kama jamaa wake Yesu kama msingi wa kuwa na mamlaka. Badala yake, Yakobo anajionyesha kama "mtumishi" wa Yesu, hakuna lingine zaidi. Kwa ufupi, Yakobo alikuwa kiongozi mwenye huruma ambaye kupitia kwake kanisa lilibarikiwa sana.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Yakobo nduguye Yesu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries