settings icon
share icon
Swali

Tutaweza jifunza yapi kutoka kwa uhai wa Sulemani?

Jibu


Sulemani alikuwa mfalme wa tatu na wa tamati katika wa ufalme wa Israeli, akiwa nyuma ya Mfalme Sauli na Mfalme Daudi. Alikuwa mtoto wa Daudi na Bathsheba, mke wa kwanza wa Uria Mhiti aliyekuwa ameuawa na Daudi ili kujificha uhuni wake na Bathsheba pale mumewe aliongoza vita. Sulemani alinakiri Wimbo Ulio Bora, kitabu cha Mhubiri, na kadhaa katika kitabu cha Mithali. Uandishi wake wa Mhubiri unapata pingamizi na wengi, ila Sulemani ni wa pekee "mtoto wa Daudi" atakayekuwa "mtawala katika Israeli" (si tu Yuda) "Yerusalemu" (Mhubiri 1: 1, 12), na mafundisho ya mwandishi yanayofaa Sulemani kamili. Sulemani akaongoza kwa miaka 40 (1 Wafalme 11:42).

Yapi yaliyo ya maana katika uhai wa Sulemani? Alipoingia katika mamlaka, alimtafuta Mungu, na Mungu akamjalia kumwomba kile alichokihitaji kutoka kwake. Sulemani alinyenyekea jinsi alivyokosa namna ya kuongoza vema na kumwuliza Mungu hekima aliyokuwa akihitaji ili kuongoza wana wa Mungu pasipo maoneleo. Mungu alimjalia hekima na mali Zaidi yake (1 Wafalme 3: 4-15; 10:27} "Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima" (1 Wafalme 10:23). Mungu alimjalia Sulemani amani pande zote wakati wa uongozi wake wote (1 Wafalme 4: 20-25).

Maonyesho mazuri kuhusu hekima ya Sulemani ni kuamua kutoelewana kati ya mama ili kutambua mmiliki kamili wa mwana mchanga (1 Wafalme 3: 16-28). Sulemani akapendekeza kukatanisha mwana mara mbili hata akiwa hai, akifahamu kuwa mama mtoto angeonelea kupoteza kwa mtu mwingine kuliko kuona akikatwa hadi kufa. Sulemani hakuwa tu na busara kwa uongozi wake bali hekima pia. Busara yake ilitambulika kwa wakati wake. Malkia wa Sheba alienda maili 1,200 ili kuhakikisha yaliyoenea kuhusu busara yake (1 Wafalme 10). "Naye Sulemani akamumbulia maswali yake yote, wala hakukuwana neno alilofichiwa mfalme asimwambie." Naye malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Sulemani na nyumba aliyoijenga,na chakula cha meza pake, na watumishi wake walivyokaa na kusimamia kwao wangoje wake na mavazi yao na wanyweshaji wake,na daraja yake ya kupandia hadi nyumba ya Bwana,roho yake ilizimia "(1 Wafalme 10: 3-5). Sulemani hakuwa na ujuzi tu, bali aliweka hekima yake katika hatua kama ufalme wake ulivyofanya.

Sulemani alinakiri mithali na nyimbo nyingi (1 Wafalme 4:32) na kukamilisha majengo mingi (1 Wafalme 7: 1-12, 9: 15-23). Sulemani vile vile aliunda meli na akajaliwa tani za dhahabu kutoka Ofiri pamoja na Hiramu, kiongozi wa Tiro, kama mshirikishi (1 Wafalme 9: 26-28; 10:11, 22). Ni kama jngo kuu alilolifanya Sulemani lilikuwa ni kukamilisha hekalu la Kiyahudi kama alivyoamuliwa na kudokezewa na baba yake, Daudi (1 Wafalme 6, 1 Mambo ya Nyakati 22)

Sulemani alimiliki wake 700 masuria 300, wengi walikuwa wageni waliomwelekeza katika kuabudu miungu hadharani kwa uzee wake,na kumchukiza Mungu zaidi (1 Wafalme 11: 1-13).1 Wafalme11: 9-10, "BWANA akamghadhibikia Suleimani kwa sababu moyo wake umegeuka naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili ,akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana. " Mungu alimdokezea Sulemani kwamba atauchukua uongozi kutoka kwake, ila, kwa sababu ya Daudi, hakutenda hivyo wakati wa uhai wa Sulemani. Alitoa ahadi ya kutoangamiza uongozi wote. Mda ule ule, Mungu aliwaruhusu wapinzani kwa Sulemani waliompa mashaka Sulemani maisha yake yaliyosaslia (1 Wafalme 11: 14-25). Yeroboamu, aliyetarajiwa kuwa kiongozi wa kwanza wa Israeli, pia alijiingiza katika upinzani dhidi ya Sulemani,ila akatoroka baadaye (1 Wafalme 11: 26-40). Uongozi ulitawanywa kwa Rehoboamu, mwana wa Sulemani (1 Wafalme 12).

Kuna mengi tunayojifunza kutoka kwa uhai wa Sulemani. Mosi,tukimtafuta Mungu kwa iamani tutampata (1 Wafalme 3: 3-7). Pili, wale wanaomthamini Mungu atawathamini pia (1 Wafalme 3: 11-13; 1 Samweli 2:30). Tatu, Mungu atatujalia kutimiza aliyotuitia ikiwa tutamwegemea Yeye (1 Wafalme 3, Warumi 12: 3-8, 2 Petro 1: 3). Nne, kuishi katika imani ni mbio, si polepole.Ila kuanza kwema si kutamatisha kwema (1 Wafalme 3; 11). Tano, tunafaa kumwuliza Mungu kuinua mioyo yetu kumwelekea (1 Wafalme 8: 57-58), ila tutaenenda kinyume na mapenzi yake kama tutaamua kukiuka aliyoyasema. Sita, walio wandani wetu wataathiri uhai wetu wa kiroho (Kutoka 34:16, 1 Wafalme 11: 1-8; Danieli 1; 3 Wakorintho 15:33), hivyo tunafaa kumakinika na wale tunaowaenzi na kuwa karibu yetu. Saba, uhai mbali na Mungu utakuwa usio na maana, bila kujali kiwango cha masomo, majukumu yaliyofanyika, raha za juu sana, na mali mingi mno (Mhubiri 1: 2).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tutaweza jifunza yapi kutoka kwa uhai wa Sulemani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries