settings icon
share icon
Swali

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Stefano?

Jibu


Matendo 6:5 inamtambulisha mtu mwaminifu wa Mungu aitwaye Stefano: "mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu." Inafaa kuzingatiwa kwamba daima kumekuwa na wale waumini waaminifu ambao upendo wao na kujitolea kwao kwa Bwana wanaonekana kung'aa daima kwa kiasi kikubwa kwamba wengine karibu nao watanatambua, na Stefano alikuwa mtu kama huyo. Hakuna kinachojulikana kuhusu maisha ya Stefano-wazazi wake, ndugu zake, au ikiwa alikuwa na mke au watoto; hata hivyo, kile kinachojulikana juu yake ni kile ambacho ni muhimu hasa. Alikuwa mwaminifu, hata wakati alipokabiliwa na kifo fulani.

Stefano alikuwa mmoja wa wanaume saba waliochaguliwa kuwa na jukumu la usambazaji wa chakula kwa wajane katika kanisa la kwanza baada ya mgogoro kutokea na mitume walitambua wanahitaji msaada. Alikuwa pia "amejaa neema na uwezo wa Mungu, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu" (Matendo 6:8). Upinzani ukatokea, lakini wanaume waliobishana na Stefano hawakuwa sawa na hekima iliyotolewa kwake na Roho Mtakatifu. Hivyo, wanaume hao waliamua kumshtaki Stefano kwa uongo, wakimwita mjadhambi na kufanya akamatwe (Matendo 6:11-14).

Matendo 7 ni rekodi ya ushuhuda wa Stefano, ambayo ni labda historia ya kina na fupi ya Israeli na uhusiano wao kwa Mungu wa yeyote katika Maandiko. Stefano hakuwa anajishughulisha kuhusu uwepo wake duniani, kuamua badala yake kusimama imara kwa upande wa Yesu Kristo, bila kujali matokeo. Mungu alimwongoza kusema kwa ujasiri, akishtaki Israeli kwa kweli kwa kushindwa kwao kumtambua Yesu, Masihi wao, kumkataa na kumwua, kama walivyomwua Zekaria na manabii wengine na wanaume waaminifu katika vizazi vyao. Hotuba ya Stefano ilikuwa ni mashtaka rasmi dhidi ya Israeli na kushindwa kwao kama watu wa Mungu waliochaguliwa ambao walikuwa wamepewa sheria, vitu vitakatifu, na ahadi ya Masihi. Kwa kawaida, mashtaka haya, ingawa kweli, hayakupokelewa vyema na Wayahudi.

Katika hotuba yake, Stefano aliwakumbusha juu ya babu yao mwaminifu, Abramu, na jinsi Mungu alivyomwongoza kutoka nchi ya kipagani hadi nchi ya Israeli, ambapo alifanya agano naye. Alizungumza kuhusu safari ya watu wake, kupitia kukaa kwa muda kwa Yusufu katika Misri hadi ukombozi wao na Musa miaka 400 baadaye. Alikumbusha jinsi Musa alivyokutana na Mungu jangwani mwa Midiani katika kichaka cha moto, na alielezea jinsi Mungu alimpa Musa uwezo wa kuwaongoza watu Wake kutoka kwa ibada ya sanamu na utumwa hadi uhuru na nyakati za kufurahi katika Nchi ya Ahadi. Katika hotuba yake yote, aliwakumbusha mara kwa mara juu ya uasi wao na ibada ya sanamu iliyoendelea, licha ya kazi kubwa za Mungu ambazo walikuwa mashahidi wa macho, na hivyo kuwashtaki kwa historia yao wenyewe, ambayo iliwakasirisha kiasi kwamba hawakutaka kusikia mengine zaidi.

Sheria ya Musa inasema kwamba dhambi ya kumtukana Mungu inastahili hukumu ya kifo, kwa kawaida kwa kupigwa mawe (Hesabu 15:30-36). Kabla ya hawa Wayahudi wenye kiburi, wasiokomboleka walifuata adhabu iliyowekwa na wakaanza kupiga mawe Stefano, Matendo 7:55-56 inaandika wakati wake wa mwisho wa maisha ya kidunia, kabla ya kupitia utaji kati ya mbinguni na dunia: "Lakini yeye (Stefano) akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu. Akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu.'"

Maneno ya Wakolosai 3:2-3 yanaweza kuwa yaliandikwa juu ya maisha ya Stefano, ingawa yanahusu waumini wote: "Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu." Maisha ya Stefano-na hata zaidi ya kifo chake-inapaswa iwe mfano wa jinsi kila muumini anapaswa kujitahidi kuishi: kujiwasilisha kwa Bwana hata wakati wa kifo; mwaminifu kuhubiri Injili kwa ujasiri; mwenye ujuzi wa ukweli wa Mungu; na kuwa tayari kutumiwa na Mungu kwa mpango na kusudi Lake. Ushuhuda wa Stefano bado unasimama kama nguzo, mwanga kwa ulimwengu uliopotea na unaokufa, pamoja na historia sahihi ya watoto wa Abramu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Stefano?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries