settings icon
share icon
Swali

Tutajifunza yapi kutoka kwa uhai wa Sarai?

Jibu


Sarai uhai wake ulianza pale Uria isiyomjua Mungu, ulioko mji wa Wakaldayo, ambayo ilikuwa panapojulikana kwa hizi enzi kuwa Iraq. Alijulikana kama binti wa baba yake, vile vile, mchumba wa Abramu, atakayeitwa Abrahamu baadaye. Sarai na Abramu walimiliki baba mmoja ila mama tofauti, kama ilivyonakiriwa Mwanzo 20:12. Kwenye enzi zile, ukoo ulihifadhiwa zaidi kuliko siku hizi, na kuoleana kati ya mandugu hikuwaathiri wana wao kwenye jamiii husika. Fauka ya hayo, kwa maana jamii zilipendelea kuishi kwa pamoja katika jamii, ilichukuliwa kawaida kupata mchumba kutoka kwa jamiizo.

Abramu alipopatana na Bwana aishiye mara ya kwanza, alimwamini (Mwanzo 12: 1-4; 15: 6) na akaandamana naye, huku akitii sheria yake ya kuacha jamii yake na kuenda mahali hajapata kufahamu tena. Sarai akaondoka wakaandama pamoja.

Mwendo wao uliwafikisha mahali palipojulikana kama Harani (Mwanzo 11:31). Baba ya Abramu, Tera, alipotesa uhai katika jiji hili, na Abramu, Sarai, na Loti mwana wa Haruni wakaendelea na mwendo wao,huku wakiacha Bwana awatangulie na kuwapa mwongozo. Kwa kukosa majengo na maeneo ya kisasa,mwendo wao pengine ulikumbwa na taabu tele,ikishamiri kwa wake. Walipokuwa kwenye mwendo,kukawa na ukosefu wa lishe kwenye mji,na kuwafanya Abramu na Sarai kuelekea Misri (Mwanzo 12:10). Walipotenda vile, Abramu akaofia kwamba Wamisri watamtoa uhai kwa maana Sarai alipendeza na wangeonelea kumtwaa kama mchumba. Sababu ile,akamwamuru Sarai kudanganya kila mmoja kuwa yeye ni dadake Abramu- na hata kama ilikuwa ni kweli alithamiria kuwaambia uongo. Sarai alitwaliwa kwenda makao ya Farao, na Abramu akahudumiwa vema kwa ajili yake. Bali Bwana akasambaratisha mle mwa Farao, hapo udanganyifu wa wapenzi hao ukaweka wazi. Farao akamrejesha Sarai kwa Abramu na akawafurusha (Mwanzo 12). Sarai na Abramu wakaja hadi kwa mji unaotambulika kuwa Israeli. Walijipatia utajiri mwingi wakiwa bado wakiwa mwendoni, basi Loti na Abramu wakaelewana kutengana ili kundi kubwa la mifugo waliokuwa nao kupata mahali pa kutosha pa kupata lishe (Mwanzo 13: 9).

Sarai aliyekuwa tasa, neno lililompatia huzuni na kutengwa kakita jamii. Abramu akakumbwa na mawazo kuwa hangepata wa kumrithi.Ila Bwana akampatia Abramu maono pale alipomahidi mtoto wake na kuwa uzao wake ungekuwa mwingi kama zilivyo nyota mawinguni.(Mwanzo 15).Vile vile Bwana akaahidi kizazi chake mji wa Kanaani. Taabu ni kuwa Sarai alisalia kuwa tasa. Karne moja tangu Bwana atoe iyo ahadi,jinsi ilivyo desturi,Sarai,akaonlea kuwa Abramu apate mwana pamoj na kijakazi wake Hagar. Kijana atakayepatikana kutokana nao wawili angeetambulika kuwa wa Sarai. Abramu akaitikia, na Hagari akajaliwa kijana-Ishmaeli. Bali Hagari akaanza kumwona Sarai kama asiyefaa, na Sarai alianza kumfanyia maovu,hadi ulipozidi sana, Hagari akatoroka. Bwana akapatana na Hagari katika jangwa na kumhimiza arejee kwa Abramu na Sarai, na akaitikia alivyoamriwa (Mwanzo 16).

Ishmaeli alipozaliwa miaka kumi na mitatu baadaye, Bwana alifanikisha agano lake na Abramu, mara hii akimpatia onyesho ya kutahiriwa na jina mbadala vile vile. Abramu, lililomaanisha "baba mkuu," akajulikana Ibrahimu, kumaanisha"baba wa mataifa." Bwana aidha akabadili alivyoitwa Sarai, maanake "mfalme wangu," na kuwa Sara,lenye maana "mama wa mataifa." Bwana akamhakikishia Ibrahimu kuwa atamjalia mtoto kutumia Sara. Mtoto huyo-Isaka-atakuwa yule Bwana atafanya agano lake kudhihirika. Mungu angemtunuku Ishmaeli aidha, ila Isaka ndiye mtoto wa ambaye ahadi ya agano ingekuwa imara kupitia yeye (Mwanzo 17). Isaka inamaanisha "kicheko." Ibrahimu aliurahi kuwa, katika umri wa miaka 100, angejaliwa na mtoto kijana pamoja na Sara aliyekuwa miaka 90 na amekuwa tasa uhai wake wote. Sara vile vile akaangua kicheko kwa jambo hilo (Mwanzo 18: 9-15).

Mara tu alipomaliza ahadi zake kwa Ibrahimu na Sara kuhusu mtoto, aliteketezaSodoma na Gomora, ila akamwepusha Loti mpwa wa Ibrahimu (Mwanzo 19). Ibrahimu na Sara walisafiri kwenda Negebu na wakaishi Gerari (Mwanzo 20: 1). Ibrahimu kama mwanzo akaambia Sara adanganye kuhusu mahusiano yake,na mtawala wa Gerar akamtwaa Sara kuwa bibi yake. Bali Bwana alimlinda Sara kupitia yeye Isaka angeletwa duniani. Mtawala Abimeleki hakuwa na uhusiano naye. Bwana alimwomya Abimeleki kwenye njonzi, na mtawala hakutoa tu tabiu kwa Bwana kwa kusamehewa bali aliwapatia zawadi Ibrahimu na Sara na kuwaruhusu kuishi katika mji ule (Mwanzo 20).

Bwana akasalia kuwa mwaminifu katika ahadi Yake ya kuwajalia Ibrahimu na Sara mtoto. Wakampatia jina Isaka, na "Sara akasema, 'Mungu amenifanyia kicheko, kila anasikiaye atacheka pamoja nami.' Akasema, "Ni nani angemwambia Ibrahimu, Sara atanyonyesha wana? maana nimemzalia mwana katika uzee wake." (Mwanzo 21: 6-7).Japo mbeleni alicheka kwa kukosa kuamini na kisiri, Sara mara hii alicheka kwa furaha na kutaka hali yake kuwa maarufu kwa wengi. Bwana amekuwa mwaminiufu katika ahadi zake na kumpa baraka.

La kusikitisha ni kuwa, uhasama baina ya Sara na Hagari haukuisha. Isaka alipowachishwa matiti, Ibrahimu akaandaa sherehe. Ila Ishmaeli, mtoto wa Hagari, aliendelea kumkejeli Isaka. Sara alimwarifu Ibrahimu kumfurusha Hagar na Ishmaeli na kuwa Ishmaeli hafai kupewa mali pamoja na Isaka. Abrahamu akashikwa mawazo kwa jambo hilo, ila Bwana akamjulisha kutenda jinsi alivyomwambia Sara kuwa uzao wao ungetambulika katika Isaka. Ibrahimu akamfurusha Hagari na Ishmaeli, na Bwana akakutana na mahitaji yao (Mwanzo 21: 8-21). Baada ya haya kutimizika Bwana akampa Ibrahimu majaribu kwa kumwambia amtoe mtoto wake Isaka dhabihu. Abrahamu alikuwa radhi kuitikia agizo hilo kwa mtoto wake wa pekee, akiaminia Mungu angeweka ahadi zake kwa namna fulani (Mwanzo 22; Waebrania 11: 17-19).

Sara aliyekuwa mzuri wa uso,na mrembo (Mwanzo 12:11), na aliyejaa roho ya utu; alitenda dhambi,jinsi tutendavyo. Alijaribu kumtangulia Mungu na kujaribu kutenda shughuli Zake binafsi kwa ujinga wake alipomwamuru kijakazi wake, Hagari, kwa Ibrahimu kupata mwana aliyekuwa ameahidiwa na Bwana. Katika tendo hilo,alichochea uhasama ambao umekaa kwa miaka 4,000 (Mwanzo 16: 3). Alicheka kwa kukosa kuamini, alipokuwa umri wa 90, alipomsikia malaika akimweleza Ibrahimu kwamba angepata ujauzito (Mwanzo 18:12), ila alipata mwana wa ahadi na kuishi miaka 30 zaidi, akakata roho kwa umri wa miaka 127 (Mwanzo 23: 1).

Waebrania 11:11 inaonyesha imani kupitia Sara: "Kwa imani hata Sara, mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba alipokuwa amepita wakati wake kwa kuwa alimhesabu yeye kuwa aliyeahidi kuwa mwaminifu."

1 Petro 3: 5-6 inadokeza Sara kuwa onyesho la mke alsiyekasoro aliyemtegemea Bwana na aliyejisitili kwa kujitolea kwa mume wake. Sara bila kulazimishwa alitoka maskani mwao na kutoka kuandamana na Ibrahimu, alipouata mwelekeo wa Mungu aliyekuwa hana uzoefu naye tangu awali. Alikabiliana na mengi ilmradi kumpatia mumewe atakaye mrithi na kumlinda mumewe katika mazingira yasiyokuwa salama. Mwishowealimiliki imani kiasi kuwa yeye na mumewe, katika umri wa 90 na 100, walijaliwa mrithi wa ahadi, Isaka. Hata kama aliishi dunia isiyokuwa salama,na machanganyiko, Sara alisalia imara katika kujitolea kwa mumewe na Mungu, na hayo yakazaa nehema nyingi.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tutajifunza yapi kutoka kwa uhai wa Sarai?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries