settings icon
share icon
Swali

Tutajifunza yapi kutoka kwa uhai wa Samsoni?

Jibu


Uhai wa Samsoni unakinzana sana. Alijulikana kuwa mwenye misuli mikubwa kimwili ila alidhihirisha unyonge kimaadili. Aliongoza kwa miaka 20 na "Mnaziri, aliyeteuliwa na Mungu tangu utotoni" (Waamuzi 13: 5), ila aliendelea kufunza torati za utawala. Roho wa Mungu alimjia mara kadhaa, huku akimpa nguvu nyingi kupambana dhidi ya Wafilisti, maasidi wa Waisraeli.Hata badala yake kuwa mpenda wake na wa kisasi.Uhai wa Samsoni unadhihirisha haja ya kunena "la" kwenye madhara ya kimwili, Mungu kutumia hata waume wasio wakamilifu kukamilisha matakwa yake,msaada wa dhambi, na nehemaya Mungu.

Maisha ya Samson — kuzaliwa kwake

Mwanzo wa Samsoni huanzia katika kutangazwa kwa kuzaliwa kwake. Mume wa Kianani aitwaye Manoa aliishi katika ndoa na mke aliyekuwa tasa (Waamuzi 13: 2). Malaika wa Mungu akamtokea yula mke akamnenea, "Lakini utachukua mimba nawe utamzaa mtoto mwanamume." (mstari wa 3). Malaika pia alimwambia ajihadhari na kutimiza torati za Naziriti akiwa angali na mimba-asinywe wala divai wala kileo ama kitu kilicho najisi. Mwanamke akamnenea Manoah, na alitoa toba kuwa malaika angewatembelea tena na kuwafundisha zaidi juu ya kuzaliwa na baadaye ya mtoto watakayempata (mstari wa 8).

Mungu akamsikia na kumjibu maombi ya Manoa. Malaika wa Mungu akamjia mke wa Manoa mara ya pili, naye akaondoka mbio kumleta mumewe. Malaika akayarudia maneno yale kwa Manoa, ambaye alitaka kufahamu jina la utambulisho wa malaika. Kwenye kumjibu, malaika akamrudishia, "Kwani wewe kuniuliza jina langu? Kwa kuwa jina hilo ni la ajabu"(Waamuzi 13:18).Kisha Manoa akamtwaa mwana mbuzi juu ya mwamba, na "mara mwali wa moto ulipopaa juu mbinguni kutoka pale madhabahuni huyo Malaika wa Bwana akapaa katika mwali wa moto" (mstari wa 20). Hapo ndipo Manoa alipongamua aliyekuwa akisema naye kuwa: "'Hakika yetu tutakufa sisi!' Akamnenea mkewe. 'kwa sababu tumemwona Mungu!' "(Mstari wa 22).

Ukweli wa maandiko ya Mungu, mkewe Manoa alimpata mwana, na wakampa jina Samsoni. Bwana alimtunuku alivyoendelea kukua.

Maisha ya Samsoni — kutoka kujaribiwa hadi dhambi

Kitabu cha Waamuzi kinaachia hapo na kuanzia pale Samsoni anatafuta mchumba. Alipendelea kumchumbia Mfilisti hata kukaidi mwelekeo wa wazazi wake nakuvunja torati ya Mungu katika kuoa kwenye wasiotahiriwa. Wazazi wake waliandamana naye kuelekea Timna ili kujiandaa katika mapambano yake.Walipokuwa njiani mwana simba akamngurumia Samsoni. "Roho ya Bwana ikamjilia kwa nguvu naye akampasua wala hakuwa na kitu chochote" (Waamuzi 14: 6). Baadaye, Samsoni akapitia kwenye ule mzoga wa simba na tazama nyuki walikuwemo ndani ya mzoga na asali,aliyotwaa akala.Hapa alikiuka torati ya Naziri: "Siku hizo zote ambazo alijiweka awe wa Bwana asikaribiemaiti" (Hesabu 6: 6). Samson alidhihirisha kuwa ametenda maovu pale alipowapatia wazazi wake asali, "lakini hakuwaambia ya kuwa ameitwaa hiyo asali katika mzoga wa simba" (Waamuzi 14: 9).

Sherehe za harusi inayosimuliwa kwenye Waamuzi 14:10 ilijawa, "unywaji." Samsoni kama Mnaziri alifaa, "kujitenga na divai na vileo" (Hesabu 6: 3). Hata hivyo mwandishi wa Waamuzi hajadhihirisha kama Samsoni binafsi alibugia vileo ama divai katika sherehe hizo,hili lilikuwa tendo lingine lilimwelekeza dhambini. Nyakati za sherehe, Samsoni alitoa kitendawili:na atakay kutambua angempa mavazi thelathini ya kitani na mavao mengine (Waamuzi 14:12). Mkewe mgeni wa Kifilisti wa Samusoni alimsaliti na kutoa jibu la kitendawili chake kwa jamaa zake. Kwa hasira, Samsoni aliwaua Wafilisti thelathini na kupeana miliki yao kwa "waliotatua" kitendawili. Mke wa Samson baadaye alipeanwa kwa mume tofauti. Matukio haya yote yalitumika na Mungu kwa malengo yake: "Hii ni la Bwana, maana alitaka kisa juu ya Wafilisti" (mstari wa 4).

Uhai wa Samsoni — Mungu ana uwezo kufanya wasiotambulika na wenye dhambi kumtimizia malengo Yake

Samsoni akiwa anajua alijitoza kwenye madhara, ila, mara kadhaa, alitumika na Mungu katika ukuu wa jina lake. Si hata makosa yetu yatazuia matakwa mema ya Mungu kutoka kutendeka. Samsoni, akiwa mwingi wa hamaki na kisasi, aliapa," hana hatia katika habari za hao Wafilisti" kwa kumchukulia mchumba wake (Waamuzi 15: 3). Akaangamiza mavuno ya Wafilisti (mistari 4-5) na walipomwua mchumbake baadaye, "alikawapiga upeo,mapigo makuu sana." (mstari wa 8).

Kwa muda Samsoni alitorokea Yuda,ila Wayahudi, waliojawa woga kuwa Samsoni alifanya mazingira maovu zaidi pamoja na Wafilisti, wakamtia mbaroni na kumpeana kwa maasimu (Waamuzi 15: 8-13). Wafilisti walipokaribia mawindo yao, "ndipo Roho ya Bwana ikamjia kwa nguvu [Samsoni]. Na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyotekelezwa kwa moto,na vile vifungo vikaanguka mikononi mwake"(mstari wa 14). Samsoni akautwaa mfupa mbichi wa taya ya punda akapiga Wafilisti 1,000 kwa mfupa huo (mstari wa 15).

Kule Gaza, Samsoni aljipatia malaya. Usiku ulipofika, wakaazi wa Gaza walifahamu kuwa Samsoni alikuwemo jijini mwao,na wakamtegea kumtoa uhai kulipokucha. Samsoni aliepa kwa kukimbia usiku wa manane, ambapo "akaishika milango ya lango la mji,na miimo yake miwili,akaingoa pamoja na komeo lakeakajitwika mabegani akavichukua hata kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni "(Waamuzi 16: 3).

Maisha ya Samsoni — madhara yanayo tokana na dhambi

Malengo ya Mungu ya kuangusha Wafilisti yalidhihirika katika njia ya Samusoni, ila Samsoni alihitajika kuwajibikia makosa aliyofanya, kisha akapata majibu ya kutokii kwake na ujinga aliokuwwa nao. Samsoni akajuana na kupendana Mfilisti aliyejulikana kama Delila. Viongozi wa Wafilisti walimuonga Delila kutambua asili ya nguvu zake nyingi Samsoni na kumsaliti hadi viganjani mwao (Waamuzi 16: 5). Delila akaanza kumbembeleza Samsoni ili kufahamu asili ya nguvu zake mingi.Alipomwelezea baadhi ya uongo,Samsoni mwishowe akadhihirisha kuwa zilitokana na kumwasi Mungu; kama vile nywele zake zilikuwa hazijawahi katwa (tazama Hesabu 6: 5). Delila aliwajuza viongozi wa Wafilisti kuhusu siri ya Samsoni na wakangoja hadi alipolala,ndipo akamwita mtu aweze kumnyoa nywele zake. Akamwamsha kwa kelele: "Samsoni, Wafilisti wanakujia!" (Mstari wa 20). Samsoni akajitwaa kupambana, "lakini hakujua kuwa Bwana amemwacha" (mstari wa 20).

Wakati wa Samsoni, uasi wa kupendelea ulifika ukingoni. Alijawa na nguvu na ujasiri hadi alipohisi kwamba ana uwezo kutotii torati yoyote; hadi ikaonekana alikuwa pale aliikiria hakumtaka Mungu tena. Hatimaye, "Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho;wakatelemka naye hadi Gaza. Wakamfunga kwa vifungo vya shaba, naye alikuwa akisagangano katika gerezani gereza "(Waamuzi 16:21). Samsoni mwishowe alilazimika kukumpana na matokeo ya makosa yake.

Maisha ya Samsoni — Mungu ana huruma

Wafilisti waliikiria kuwa wangesherehekea dhidi ya kumshinda Samsoni, na viongozi walikuwa kwenye hekalu la miungu yao, Dagoni, kumtukuza kwa kumwachilia Samsoni mikononi mwao (Waamuzi 16:23). Sherehe ziliposheheni, wakamtoa Samsoni kwenye gereza ili kuwatumbuiza. Kuegemea kwenye miamba ya hekalu la kipagani, "Samsoni akamwita Bwana akasema, 'Ee Bwana Mungu, unikumbuke. Nakuomba ukanitie nguvu nakuomba mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.'"(mstari wa 28). Mungu mwenye huruma akamjalia aliloomba Samsoni. Samsoni "akainama kwa nguvu zake zote, ile nyumba ikawaangukia hao wakuu na watu wote waliokuwa ndani yake" (mstari wa 30). Samsoni aliua wengi alipopoteza uhai-karibu 3,000 Wafilisti-zaidi ya vile alipokuwa hai.

Samsoni ametajwa katika maandiko kama mtu wa imani"jumba la imani" (Waebrania 11:32). Papo hapo, alikuwa kiumbe wa mwili, na dhambi zake nyingi zikawa fundisho kwa wenye wangechezea dhambi waepuke adhabu yake.Maisha ya Samson yanatupa onyesho kuhusu kuegemea ukuu wa Mungu, si uwezo wetu binafsi; kutoacha upendo wa Mungu, si ujeuri wetu; na kutafakari busara ya Mungu, si kujua kwetu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tutajifunza yapi kutoka kwa uhai wa Samsoni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries