settings icon
share icon
Swali

Kutokana na uhai wa Ruthu tunajifunza yapi?

Jibu


Ruthu aliyekuwa mmoja wa wanawake wa Moabu ila alihusiana na Israel kupitia Loti, mwana wa mwanawe Ibrahimu. (Ruthu 1: 4; Mwanzo 11:31; 19:37). Ruthu alikuwa nyakati za waamuzi. Aliolewa na mwana katika jamii ya Israeli wangali huko Moabu, ila baadaye wakweze wawili na mumewe waliaga dunia.Hivyo Ruthu alifaa kuamua kuishi kwake, Moabu, ama kuondoka pamoja na mama mkwe Naomi hadi Yuda mahali ambapo hakuweza kupafahamu.

Ruthu hakumpenda tu ila kumhurumia pia mama mkwe mno,kwani alikuwa amefiwa si tu na mmewe ila hata na watoto wake. Shemeji ya Ruthu, Orpa,aliamua kubaki na jamaa zake kule Moabu,ila Ruthu hakuwa na uwezo kumwacha mkwewe ama Mungu wa Waisraeli aliyekuwa amefanya kujuana naye. Wote Ruthu na mkwewe walianza safari kurudi Yuda katika jiji la Bethlehemu,na hapo walichagua kuishi. Ushuhuda wa Ruthu ulijulikana kote,na Boazi, aliyekuwa na ardhi huko karibu,alipopata hiyo habari,ilivyonakiriwa Ruthu 2: 11-12: "Naye Boazi akajibu akamwambia, 'Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo,tangu alipokufa mumeo;na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako,na nchi yako uliyozaliwa,ukawafikilia watu usiowajua tangu hapo.Bwna akujazi kwa kazi yako,nawe upewe thawabu kamili na Bwana,Mungu wa Israeli,ambaye umekuja kukimbilia chini ya mabawa yake. '"

Ilivyo kuwa tamaduni katika Israeli ni kuwa mume alimiliki mke wa nduguye aliyekuwa ameaga ndio waendeleze jamii naye.Maana mkwewe wa pekee Ruthu alikuwa ameaga,walikuwa wajitunze wenyewe na Naomi. Ruthu alienda kila kujao mashambani ili kutafuta lishe yake na Naomi. Alibahatika kibarua shambani kwa Boazi, bila ufahamu kuwa ni mmoja wa mbari yao Naomi. Boazi aliporejea masdkani alimtupia jicho Ruthu,na akamuliza kiongozi wa wafanyikazi kumhusu. Mfanyikazi akamwelezea Boazi kumhusu Ruthu na uaminifu wake kwa Naomi na jitihada zake kule mashambani. Boazi binafsi aliamuru Ruthu kusalia kwenye shamba zake na sako kwa bako na wake waliokuwemo,na kumhakikishia kuwa amewathaathirisha vijana kula wasimtenge na kumpa idhini kunywa maji waume walikuwa wameteka popote alihisi kiu ( Ruthu 2: 8-9). Ruthu alisujudia na kuinamia hadi chini,akamwambia jinsi gani amepata kibali machoni pake hata angali mgeni pale,ndipo Boazi akamwambia alivyoelezwa aliyomfanyia mkweo (Ruthu 2: 10-13). Boazi aliendeleza kudhihirisha wema, akampa lishe na kuamuru wafanyikazi wake kuacha mavuno mengine nyuma ili aweze kuokota (Ruthu 2: 14-16).

Ruthu alipomwelezea Naomi amlipokuwa ameokota, Naomi alijawa na furaha na akasema kuwa Boazi ni mmoja wa mbari yake,kukokana na familia ya Elimeleki, mumewe Naomi; hivyo, Boazi alifaa kuwa mfanyikazi wa Ruthu. Ilifaa mno kwa Ilikuwa Waisraeli kueneza jina la kila familia ya Israeli, hii ilimpa Ruthu haki kukata rufaa kwa Boazi kutimiza hiyo kazi. Naomi akamwambia Ruthu aendelee kuenda shamba la Boazi, na alifanya hivo hata mwisho wa mavuno ya shayiri na ya ngano pia (Ruthu 2: 18-23).

Katika mavuno ya shayiri, Naomi alimwambia Ruthu aende kwa Boazi alipokuwa akipepeta shayiri la mno kumsihi kuwa mmoja wa wakulima wake. Ruthu alimiliki akili wazi na roho ya kufundishika akampa mkweo sikio na kutenda alivyoagiza (Ruthu 3: 2-5). Ruthu alitii alivyoagizwa na Naomi kwenye anuani hiyo. Boazi aliitikia kwa kumpendelea ila alifahamu aliyekaribu sana wa kiume ambaye angekuwa mwanzo kukomboa Ruthu na urithi wa jamii yake. Mume huyo alifaa kuulizwa mwanzo kama bado hajamchukua Ruthu kama mke. Siku iliyofuata, Boazi alipatana na jamaa huyo aliyetoa idhini kisheria haki zake zote kwa Ruthu na Naomi na urithi wao.

Ruthu na Boazi punde wakafunga harusi na kupata mwana wa kiume anayeitwa Obed. Nao wanawake wa pale walifurahi, walipoona uaminifu wa Mungu na kumwambia Naomi, "Na ahimidiwe Mungu asiyekuacha leo hali huna wa jamaa aliye karibu;jina lake huyu na liwe kuu katika Israeli,Naye atakurejezea uhai wako kwa maana mkweo ambaye akupenda naye anakufaa kuliko watoto saba ndiye aliyemzaa"(Ruthu 4: 14-15).

Ruthu alimtegemea Bwana, na akamjalia uaminifu wake sio tu kumpa mume ila pia kumpa mwana (Obed), mjukuu (Yese), na mjukuu wake Daudi, mtawala wa Israeli (Ruthu 4:17). Zaidi ya tunuku hizi (Zaburi 127: 3), Mungu akamjalia Ruthu baraka ya zinazodokezwa katika kizazi cha Yesu (Mathayo 1: 5).

Ruthu ni onyesho la namna Mungu anavyobadilisha hulka na kuipa mwongozo ambao ameonelea Yeye. Tunampata akitenda mpango wake kwa hulka ya Ruthu,jinsi atendavyo na wanawe wote. (Waroma 8:28). Hata kama alikuwa na asili isiyomjua Mungu kule Moabu,alipopata kumjua Mungu wa Israeli, alidhihirisha ushuda wa Mungu katika maisha yake katika imani. Ingawa aliishi kwa ugumu kabla ya kujuana na Boazi, alietegemea kuwa Mungu angewalinda jamii yake. Zaidi, Ruthu ni dhihirisho ya uaminiu na kutenda kazi kwa bidii. Twafahamu kuwa Mungu humtunuku mwaminifu: "Lakini pasipo Imani haiwezekani kumpendeza kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao." (Waebrania 11: 6).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kutokana na uhai wa Ruthu tunajifunza yapi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries