settings icon
share icon
Swali

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Petro?

Jibu


Simoni Petro, pia anajulikana kama Kefa (Yohana 1:42), alikuwa mmoja wa wafuasi wa kwanza wa Yesu Kristo. Alikuwa mwanafunzi asiyeogopa kusema ukweli na mwenye shauku, mmoja wa marafiki wa karibu zaidi wa Yesu, mtume, na "nguzo" ya kanisa (Wagalatia 2:9). Petro alikuwa mwenye shauku, mwenye msimamo wa nguvu, mwenye msukumo, na, wakati mwingine, jeuri. Petro alikuwa na nguvu nyingi na pia kushindwa kadhaa katika maisha yake. Bado, Bwana ambaye alimchagua aliendelea kumuumba kuwa hasa vile alitarajia Petro awe.

Simoni Petro alikuwa awali kutoka Bethsaida (Yohana 1:44) na aliishi Kapernaumu (Marko 1:29), miji yote miwili ikiwa pwani ya Bahari ya Galilaya. Alikuwa ameoa (1 Wakorintho 9:5, Marko 1:30), na yeye na Yakobo na Yohana walikuwa washirika katika biashara yenye faida ya uvuvi (Luka 5:10). Simoni Petro alikutana na Yesu kupitia nduguye Andrea, ambaye alikuwa amemfuata Yesu baada ya kusikia Yohana Mbatizaji akitangaza kwamba Yesu alikuwa Mwana-Kondoo wa Mungu (Yohana 1:35-36). Andrea alienda mara moja kumtafuta ndugu yake kumleta kwa Yesu. Baada ya kukutana na Simoni, Yesu akampa jina jipya: Kefa (Kiaramu) au Petro (Kigiriki), ambalo linamaanisha "mwamba" (Yohana 1:40-42). Baadaye, Yesu alimwita rasmi Petro kumfuata Yeye, akifanya unasaji wa ajabu wa samaki katika mfuatano huo (Luka 5:1-11). Mara moja, Petro aliacha vitu vyote kufuata Bwana (mstari wa 11).

Kwa miaka mitatu iliyofuata, Petro aliishi kama mwanafunzi wa Bwana Yesu. Akiwa kiongozi aliyesaliwa asili, Petro akawa msemaji wa bila kupingwa kwa wale kumi na wawili (Mathayo 15:15, 18:21, 19:27, Marko 11:21, Luka 8:45, 12:41, Yohana 6:6; 13:6-9, 36). Muhimu zaidi, ni Petro ambaye alikiri kwanza Yesu kama "Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai," ukweli ambao Yesu alisema ulifunuliwa kwa Petro na Mungu (Mathayo 16:16-17).

Petro alikuwa sehemu ya mviringo wa ndani wa wanafunzi wa Yesu, pamoja na Yakobo na Yohana. Hawa watatu tu walikuwapo wakati Yesu alimfufua binti wa Yairo (Marko 5:37) na wakati Yesu alibadilishwa mlimani (Mathayo 17:1). Petro na Yohana walipewa kazi maalum ya kuandaa chakula cha Pasaka ya mwisho (Luka 22:8).

Katika mifano kadhaa, Petro alijidhihirisha kuwa wa haraka kwa kiwango cha pupa. Kwa mfano, ni Petro ambaye aliacha mashua na kutembea juu ya maji kuenda kwa Yesu (Mathayo 14:28-29) — na papohapo akaondoa macho yake kwa Yesu na kuanza kuzama (mstari wa 30). Alikuwa Petro ambaye alimchukua Yesu kando ili kumkemea kwa kusema juu ya kifo chake (Mathayo 16:22) — na alikosolewa kwa haraka na Bwana (mstari wa 23). Alikuwa Petro aliyependekeza kusimamisha vibanda vitatu ili kuheshimu Musa, Eliya, na Yesu (Mathayo 17:4) — na akaanguka chini kwa kimya cha hofu kwa utukufu wa Mungu (mistari 5-6). Alikuwa Petro ambaye alichomoa upanga wake na kumkata mtumishi wa kuhani mkuu (Yohana 18:10) — na mara moja aliambiwa arudishe silaha alani mwake (mstari wa 11). Alikuwa Petro ambaye alijisifu kwamba hatamkana Bwana, hata kama kila mtu mwingine angefanya (Mathayo 26:33) — na baadaye akamkataa mara tatu kwamba hata hakumjua Bwana (mistari 70-74).

Kupitia mema na mabaya ya Petro, Bwana Yesu alibaki Bwana wake mwenye upendo na mwongozo Mwaminifu. Yesu alimhakikishia Simoni kama Petro, "Mwamba," katika Mathayo 16:18-19, akiahidi kwamba atakuwa muhimu katika kuanzisha Kanisa la Yesu. Baada ya kufufuliwa Kwake, Yesu alimtaja Petro hasa kama mtu aliyehitaji kusikia habari njema (Marko 16:7). Na, akirudia muujiza wa unasaji wa samaki wengi, Yesu aliweka hoja maalum ya kumsameha na kumrejesha Petro na kumteua tena kama mtume (Yohana 21:6, 15-17).

Siku ya Pentekoste, Petro alikuwa msemaji mkuu kwa umati wa watu huko Yerusalemu (Matendo 2:14ff), na Kanisa likaanza na kumiminika ndani kwa waumini wapya takribani 3,000 (mstari wa 41). Baadaye, Petro aliponya mwombaji kiwete (Matendo 3) na akahubiri kwa ujasiri mbele ya Wakuu wa Makuhani (Matendo 4). Hata kukamatwa, kupigwa, na vitisho havikuweza kupunguza uamuzi wa Petro wa kuhubiri Kristo aliyefufuka (Matendo 5).

Ahadi ya Yesu kwamba Petro atakuwa msingi katika kujenga Kanisa ilitimizwa kwa hatua tatu: Petro alihubiri siku ya Pentekoste (Matendo 2). Kisha, alikuwepo wakati Wasamaria walipokea Roho Mtakatifu (Matendo 8). Mwishowe, aliitwa nyumbani mwa jemedari wa jeshi la Kirumi Kornelio, ambaye aliamini pia na kupokea Roho Mtakatifu (Matendo 10). Kwa njia hii, Petro "alifungua" dunia tatu tofauti na kufungua mlango wa Kanisa kwa Wayahudi, Wasamaria, na Mataifa.

Hata kama mtume, Petro alipata uchungu wa kukua. Mara ya kwanza, alikuwa amekataa kuchukua injili kwa Kornelio, Mtaifa. Hata hivyo, alipoona Warumi wakipokea Roho Mtakatifu kwa njia ile ile aliupokea, Petro alihitimisha kwamba "Mungu hana upendeleo" (Matendo 10:34). Baada ya hapo, Petro alitetea kwa nguvu sana nafasi ya Mataifa kama waumini na alikataa katakata kwamba hawakuhitaji kufuatana na sheria za Kiyahudi (Matendo 15:7-11).

Tukio lingine la ukuaji katika maisha ya Petro linahusisha ziara yake Antiokia, ambapo alifurahi ushirika wa waumini wa Mataifa. Hata hivyo, wakati Wayahudi wengine wa kisheria walifika Antiokia, Petro, ili kuwatuliza, akaondoka kutoka kwa Wakristo wa Mataifa. Mtume Paulo aliona hii kama unafiki na kuiita hivyo mbele ya Petro (Wagalatia 2:11-14).

Baadaye katika maisha, Petro alitumia wakati pamoja na Yohana Marko (1 Petro 5:13), ambaye aliandika Injili ya Marko kulingana na kumbukumbu za Petro za wakati wake na Yesu. Petro aliandika barua mbili zenye msukumo, 1 na 2 Petro, kati ya AD 60 na 68. Yesu alisema kwamba Petro angekufa kifo cha shahidi wa dini (Yohana 21:18-19) — unabii uliotimizwa, labda, wakati wa utawala wa Nero. Desturi inayo kwamba Petro alisulubiwa kichwa chini huko Roma, na, ingawa hadithi inaweza kuwa ya kweli, hakuna ushahidi wa maandiko au wa kihistoria kwa maelezo ya kifo cha Petro.

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Petro? Hapa kuna masomo machache:

Yesu anashinda hofu. Ikiwa kutoka nje ya mashua hadi kwenye bahari isukasukayo au kuingia kwenye kizingiti cha nyumba ya Mataifa kwa mara ya kwanza, Petro alipata ujasiri katika kumfuata Kristo. "Katika pendo hamna hofu. Lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu ... "(1 Yohana 4:18).

Yesu anasamehe kutokuwa na uaminifu. Baada ya kujivunia juu ya uaminifu wake, Petro alimkataa kwa ari Bwana mara tatu. Yesu kwa upendo alimrejesha Petro kwa kutumikia. Petro alikuwa mshindwa wa zamani, lakini, pamoja na Yesu, kushindwa si mwisho. "Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa, kwa maana hawezi kujikana mwenyewe" (2 Timotheo 2:13).

Yesu hufundisha kwa uvumilivu. Tena na tena, Petro alihitaji kukosolewa, na Bwana aliitoa kwa uvumilivu, msimamo, na upendo. Mwalimu Mkuu anataka wanafunzi wako tayari kujifunza. "Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoienda ..." (Zaburi 32:8).

Yesu anatuona kama anavyotaka sisi tuwe. Mara ya kwanza walipokutana, Yesu alimwita Simoni "Petro." Alikuwa mvuvi mkali na asiyejali, machoni mwa Yesu, mwamba imara na mwaminifu. "... Yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza ..." (Wafilipi 1:6).

Yesu anatumia mashujaa wasiotarajiwa. Petro alikuwa mvuvi kutoka Galilaya, lakini Yesu alimwita kuwa mvuvi wa binadamu (Luka 5:10). Kwa sababu Petro alikuwa tayari kuacha yote aliyokuwa nayo kumfuata Yesu, Mungu alimtumia kwa njia kubwa. Petro alipokuwa akihubiri, watu walishangaa kwa ujasiri wake kwa sababu alikuwa "hana elimu" na "kawaida." Lakini basi walitambua kwamba Petro "alikuwa pamoja na Yesu" (Matendo 4:13). Kuwa pamoja na Yesu kunafanya tofauti zote.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Petro?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries