settings icon
share icon
Swali

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Nuhu?

Jibu


Tunasikia kuhusu Nuhu kwa mara ya kwanza katika Mwanzo 5, ambayo inaanza na "hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu." Hiki ni kirai cha kurudiarudia katika Mwanzo, na sura ya 5 inaelezea kwa kina mstari wa Mungu wa Sethi kinyume na mstari wa kidunia wa Kaini (Mwanzo 4:17-24). Kuchukulia hakuna kuvunjika wa kizazi, Nuhu anawakilisha kizazi cha kumi kutoka kwa Adamu. Akaunti ya kizazi cha Nuhu inasema, "Lameki akaishi miaka 182, akazaa mwana. Akamwita jina lake Nuhu, akinena, 'Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani BWANA'"(Mwanzo 5:28-29).

Kuanzia mwanzo, tunaona kwamba Nuhu atakuwa wa kipekee kwa kuwa yeye ndiye mwanachama pekee wa kizazi hiki ambaye jina lake linafafanuliwa. Baba yake, Lameki, anasema kwamba mwanaye, Nuhu, ataleta faraja ("Nuhu" inaonekana kama neno la Kiebrania kwa "mapumziko au faraja"). Tunajifunza kwa haraka kile Nuhu angewafariji kutoka katika Mwanzo 6:1-8, ambapo tunaona matokeo yasio na vikwazo ya kuanguka kwa vile udhalimu unaongezeka duniani kote. Mungu anashitaki rasmi mwanadamu na maneno haya: "BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake mbaya tu siku zote" (Mwanzo 6:5). Mungu aliamua "nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya" (Mwanzo 6:7) . Bado, hata katika hali hii, kuna matumaini: "Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA" (Mwanzo 6:8). Licha ya uovu ulioenea ambao ulikuwa ukiongezeka kwa kiasi kikubwa duniani, kuna mtu mmoja ambaye anasimama imara-mtu ambaye maisha yake yanasifiwa kwa mkono wa neema ya Mungu juu yake. Nuhu alipata neema na Bwana. Mungu alikuwa karibu kutuma hukumu juu ya ulimwengu kwa uovu wake, lakini Yeye anaeneza neema Yake ya kuokoa kwa Nuhu na familia yake.

Mwanzo 6:9 inaashiria mwanzo wa hadithi ya mafuriko, na ni hapa kwamba tunajifunza zaidi kuhusu maisha ya Nuhu. Tunajifunza kwamba Nuhu alikuwa mtu mwenye haki, asiye na hatia katika kizazi chake, na kwamba alitembea pamoja na Mungu. Mtu anaweza ona kwa karibu uendeleaji wa kiroho katika maelezo haya ya maisha ya Nuhu. Kwa kusema Nuhu alikuwa mwenye haki, tunajua kwamba alikuwa mtiifu kwa amri za Mungu (kama vile alivyoweza na kuelewa kwa wakati huo). Yeye hakuwa na hatia katika kizazi chake, wa kipekee kati ya watu wa siku yake. Walipokuwa wakijihusisha na upotofu, Nuhu alikuwa akiishi maisha ya mfano. Hatimaye, Nuhu alitembea pamoja na Mungu, ambayo inamweka kwa kitengo sawa na babu yake mkubwa, Henoko (Mwanzo 5:24); hii inamaanisha si tu maisha ya utii, lakini moja ambayo ina uhusiano wa kusisimua na wa karibu na Mungu.

Tunaona maisha ya utiifu ya Nuhu yalionyeshwa kwa nia yake ya kutii bila swali amri ya Bwana kuhusu safina (Mwanzo 6:22; 7:5, 9; 8:18). Zingatia kwamba Nuhu na kizazi chake labda hawakuwa wamewahi ona mvua mbeleni, lakini Mungu anamwambia Nuhu ajenge chombo kikubwa cha kuvukia bahari mahali hakuna maji mengi. Uaminifu wa Nuhu kwa Mungu ulikuwa hivyo kwamba aliitii haraka. Maisha ya Nuhu yasio na hatia yanafanywa dhahiri vile anamtii Bwana katika siku ya gadhabu inayokaribia. Mtume Petro anatuambia kwamba Nuhu alikuwa "ishara ya haki" (2 Petro 2:5), na mwandishi wa Waebrania anasema kwamba "alihukumu ulimwengu" (Waebrania 11:7) kupitia matendo yake ya haki. Kuchelewa kwa muda mrefu kwa hukumu ijayo, Nuhu aliendelea kumtii Bwana kwa uaminifu. Kama ushahidi wa kutembea kwake pamoja na Mungu, baada ya gharika, Nuhu alijenga madhabahu na kutoa sadaka kwa Mungu (Mwanzo 8:20). Kuabudu kulikuwa sehemu kuu ya maisha ya Nuhu.

Mbali na hadithi ya mafuriko na nakshi ya ulevi wake ulioandikwa katika Mwanzo 9:20-27, hatujui mengi kuhusu maisha ya Nuhu. Hakika, ulevi sio tu tukio lisilofaa katika maisha ya Nuhu. Kama sisi sote, Nuhu alizaliwa na asili ya dhambi. Tukio la ulevi wake lilijumuishwa katika hadithi, zaidi ya uwezekano, kuelezea chuki kati ya Wakanaani na Waisraeli. Licha ya tukio hili, tunaona kwamba Nuhu alitajwa kama mmoja wa watu wachache wa pekee wenye haki katika historia ya watu wa Mungu. Mara mbili katika Ezekieli 14, Mungu anasema kupitia nabii kwamba hata kama Nuhu, Danieli, na Ayubu walikuwepo katika nchi, Mungu hangezuia watu kutoka hukumu. Hiyo ni kampuni ya haki ya kuwa ndani (Danieli na Ayubu). Pia tunajua kwamba Nuhu amejumuishwa kama mfano wa imani katika Waebrania 11, dalili nyingine kwamba Nuhu alichukuliwa mfano wa uaminifu na kwamba alikuwa na aina ya imani ambayo inampendeza Mungu (Waebrania 11:6).

Baada ya kusema hayo yote, tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Nuhu? Kuzungumza kwa wazi, Nuhu ni mfano wa maisha ya imani. Waebrania 11:7 inasema juu ya Nuhu, "Kwa Imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari ya mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makossa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani." Nuhu hakuhitaji "kumjaribu" Mungu kabla ya kuingia katika tendo; Mungu aliamuru, naye akatii. Huu ulikuwa mfano hasa wa maisha ya Nuhu. Nuhu alikuwa sehemu ya mstari wa Mungu wa Sethi, ambaye kwake kulisemwa, "Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia jina la BWANA" (Mwanzo 4:26). Nuhu alikuwa matokeo ya utii wa kizazi na uaminifu kwa Mungu. Ikiwa tunapaswa kuiga maisha yetu kwa ya Nuhu, hakuna amri bora zaidi ya kufuata kuliko kuwa "wenye haki, wasio na hatia katika kizazi chetu, na kutembea pamoja na Mungu." Kwa maneno mengine, kuwa sawa na Mungu, kuwa sawa na wengine, na kuwa na uhusiano wa heshima na wa ibada na Mungu. Unaweza karibu kusikia maneno ya Yesu yanarudiwa hapa wakati anajibu swali la mwanasheria kuhusu amri kuu (Mathayo 22:37-39).

Kuzungumza kiteolojia, tunaweza pia toa baadhi ya masomo kutoka maisha ya Nuhu. Kwanza kabisa, maisha ya Nuhu yanatuonyesha ukweli wa milele kwamba tunaokolewa kwa neema kupitia imani (Waefeso 2:8). Nuhu hakuwa mfano wa mtu binafsi kwa sababu alikuwa na uwezo wa njia fulani wa kupitia mapungufu ya asili ya dhambi tunayomiliki sisi wote. Neema ya Mungu ilikuwa juu yake, mbali nayo Nuhu angeweza kuangamia pamoja na wengine wote watenda dhambi katika mafuriko. Nuhu pia ni mfano mkuu kwamba Mungu anaokoa wateule Wake. Tunaona kwamba Mungu alikuwa na subira kuhusu hukumu inayokuja huku Nuhu akijenga safina (1 Petro 3:20; 2 Petro 2:5). Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa waumini kutoka kwa majaribu. Ukweli huu umeandikwa kwa wazi katika 2 Petro 3:8-9, vile tunavyojifunza kwamba Bwana ataahirisha hukumu ya mwisho mpaka wateule wote wafikie toba.

Hatimaye, maisha ya Nuhu hutumika kama kumbukumbu kwamba hukumu juu ya dhambi itakuja. Siku ya Bwana itakuja (2 Petro 3:10). Yesu anatumia maisha ya Nuhu kama kutabiri vile itakavyokuwa wakati Mwana wa Adamu atakaporudi katika hukumu ya mwisho (Mathayo 24:37-38; Luka 17:26-27). Kama hivyo, tunahitaji kufuata mfano wa Nuhu na kuwa "ishara ya haki" na tusikize maneno ya Paulo: "Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu"(2 Wakorintho 5:20). Kama Nuhu, sisi ni wajumbe wa Kristo katika siku hizi za mwisho. Hukumu ya Mungu inakuja, lakini Yeye anatoa upatanisho kupitia Yesu Kristo. Lazima tuchukue ujumbe huu wa upatanisho kwa wengine.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Nuhu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries