settings icon
share icon
Swali

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Nehemia?

Jibu


Ezra na Nehemia walikuwa wa hirimu au rika lilelile, na wote wawili waliandika kuhusu kujenga upya kwa Yerusalemu, ambao ulifanyika takribani miaka sabini baada ya kuangamizwa na Wababeli chini ya Nebukadneza. Ezra aliandika kuhusu kujenga upya kwa hekalu chini ya Zerubabeli, huku Nehemia aliandika juu ya kujenga upya kwa kuta za Yerusalemu. Kutoka nyakati za zamani, miji iliyopo Mashariki ya Kati ilizungukwa na kuta za mawe na malango ambayo ililindwa kwa ajili ya ulinzi wa wananchi. Wanaume muhimu wa kila mji wangekusanyika kwenye lango ambako wangeweza kufanya biashara ya jiji, kushiriki habari muhimu, au tu kupitisha wakati.

Akaunti ya Nehemia inaanza mwaka wa 445 KK, na tarehe hii ni muhimu kwa sababu nabii Danieli, wa hirimu wa Ezra na Nehemia, aliandika unabii wa "wiki 70 za miaka" (Danieli 9:24-27) kulingana na tarehe maalum -- Machi 15 , 445 KK. Tarehe hii ni muhimu kwa mwanzo wa unabii kwa kuwa inaanzisha wakati wa kinabii, ambao unatamatika na kuja kwa pili kwa Yesu Kristo. Unabii huu uliandikwa muda mrefu kabla ya Yesu kuja kwa mara ya kwanza, lakini uliendelea kwa miaka hiyo ukiongoza hadi "kukatwa" Kwake. Inatoa maelezo kuhusu mpinga Kristo, jinsi atakavyoingia kwenye mandhari ya ulimwengu, na jinsi atakavyopinga Israeli katika shambulio lake la mwisho juu ya Mungu na watu Wake. Kwa sasa tunaishi kati ya wiki y a 69 na 70.

Unabii wa Danieli unapatikana katika Danieli 9:25: "Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu." Nehemia hakujua kwamba alikuwa akitimiza unabii ulioandikwa na Danieli.Nehemia, ambaye pia alikuwa mateka huko Babiloni wakati huo, alianza maandishi yake kwa sala ya kuombea watu wake, Israeli, kama vile Danieli alivyowaombea mara kwa mara kwa niaba yao, akisihi Mungu kuwahurumia na kuwarudisha katika nchi yao. Nehemia alitaja tarehe maalum, chini ya msukumo wa Roho Mtakatifu, ili kuweze kuwa na rekodi iliyoandikwa kuhusu utoaji wa amri ya kujenga upya Yerusalemu.

Kabla ya kuomba ruhusa ya mfalme ili kujenga upya kuta za Yerusalemu, Nehemia aliomba, na Mungu akajibu ombi lake. Alipokuwa akiondoka Babeli, alikutana na baadhi ya wanaume wa Kiarabu ambao walimdhihaki kwa kile alichokuwa karibu kufanya. Nehemia 2:20 inaandika taarifa yake, ambayo inasimama hata leo kama agano kwa yule aliye na haki kwa mji unaojulikana kama Yerusalemu: "Ndipo nikawajibu, nikawaambia, Mungu wa mbinguni, yeye atatufanikisha; kwa hiyo sisi, watumishi wake, tutaondaka na kujenga; lakini ninyi hamna sehemu, wala haki, wala kumbukumbu, katika Yerusalemu."

Nehemia aliendelea katika kutafuta kwake kujenga upya Yerusalemu. Mungu alitoa wafanyakazi wote waliohitajika, na kujenga kukaanza. Hata hivyo, hawakukosa maadui-wale ambao walitaka kusimamisha ujengaji upya. Lakini Mungu aliingilia kama alivyofanya na Musa (Kutoka 14:14). Nehemia 4:20 inaandika, "Basi mahali popote mtakaposikia sauti ya baragumu, enendeni huko, mkatujie; Mungu wetu atatupigania!" Huu ulikuwa mpango wa Mungu ulioandaliwa mapema wa kuwaleta watu Wake kutoka utumwa na kuwarudisha katika nchi yao ili kuabudu tena katika Hekalu.

Tunaweza kujifunza masomo muhimu kutokana na maisha ya Nehemia katika kurejesha na kudumisha uhusiano na Mungu. Vile watu waliporudi kujenga upya mji, utaratibu wa kwanza wa biashara ulikuwa kuhakikisha kwamba walielewa Sheria ya Musa. Hivyo Ezra, kuhani, alitumia saa nyingi kusoma Sheria mbele ya kusanyiko, akihakikisha kwamba walielewa kile Mungu alichotaka. Nehemia 8:18 inaandika kile kinapaswa kuwa sehemu ya maisha ya kila muumini, usomaji wa kila siku wa neno la Mungu: "Tena siku baada ya siku, tangu siku ya kwanza hata siku ya mwisho, Ezra akasoma katika Kitabu cha Torati ya Mungu. Wakafanya sikukuu muda wa siku saba; na siku ya nane palikuwa na kusanyiko la makini, kama alivyoagizwa."

Nehemia anasimama kama agano la uaminifu na uvumilivu. Aliishi mbali sana na nyumba yake, bado hakukata kamwe tumaini kwamba siku moja atarudi kwake. Alitumia muda mwingi wa maisha yake katika uhamishoni katika nchi ya kipagani, bado hakuyumbayumba kamwe katika imani yake na tumaini lake katika Mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Alikuwa mpiganaji wa maombi, akiweka kila kitu mbele ya Bwana katika sala, akisihi kwa niaba ya watu wake, na alipewa thawabu kwa bidii yake na uvumilivu. Nehemia aliwajali sana watu wake kiasi kwamba hakuwahi acha tumaini la marejeo yao, si kwa nchi yao tu, bali kwa Mungu ambaye kwanza alimwita mhenga wao, Ibrahimu, kutoka eneo moja na akafanya agano naye, moja ambalo Nehemia aliamini lingeweza kusimama milele.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Nehemia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries